Idadi ya wanaotawanywa na mabadiliko ya tabia nchi inaongezeka:UNHCR

Kusikiliza /

Wakazi wa Sudan wanaohama kufuatia mafuriko. Picha: UNAMID

Idadi ya watu wanaotawanywa na athari za mbadiliko ya tabia nchi ikiwemo ukame, mafuriko, vimbunga na majanga mengine inaongezeka , kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa leo kwenye mkutano wa mabadilko ya tabia nchi COP23 unaoendelea nchini Ujerumani.

Akizungumza na UN news kandoni mwa mkutano huo mjini Bonn, Marine Frank afisa wa programu ya mabadiliko ya tabia nchi idara ya ulinzi wa kimataifa kwenye shirika la UNHCR amesema watu hao ni wakimbizi kama walivyo wakimbizi wengine na wanastahili kusaidiwa, kulindwa na kupewa haki na kila uchao idadi yao inaongezeka.

Ameongeza kuwa mipango ipo na kuna baadhi ya nchi imeshaanza kuitekeleza, lakini sio nchi zote , hivyo amehimiza kuwa ni muhimu kwa jumuiya ya kimataifa na serikali kutilia maanani kikanda na kimataifa mipango hiyo  ya ulinzi wa watu hao ambayo ni

(MARINE CUT)

"Vibali vya ulinzi wa kibinadamu au visa, mipango ya muda mfupi ya kuishi na ulinzi, na pia sheria za uhamiaji ambazo zinaweza kuwalinda watu hawa lakini tatizo ni kwamba sio nchi zote zimejumuisha hayo katika sheria zake, hiyo lengo sasa ni kuhimiza matumizi ya mipango hii katika nchi. "

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930