Dola Millioni 100 zahitajika kuokoa watu kutokana na majanga

Kusikiliza /

Mabadiliko ya tabianchi yaathiri sekta ya uvuvi. Huyu ni vvuvi nchini Sudan. (Picha:World Bank/ Arne Hoel)

Shirika la umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO, linataka hatua zaidi zichukuliwe ili kufanikisha mfuko wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na pia kutoa taarifa mapema uitwao CREWS.

Mfuko huo unahitaji dola milioni 100 ifikapo mwaka 2020 ambapo WMO inataka kasi zaidi ya uchangiaji ili kusaidia nchi maskini zilizo katika hatari za kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

WMO imesema bila uwekezaji pia katika mfuko huo msaada kwa nchi maskini kukabili mabadiliko ya tabianchi itakuwa matatizo makubwa.

Uwepo wa mfuko huo ni mojawapo ya maazmio ya mkataba wa Paris na uliungwa mkono na nchi 5 ambazo ni Australia, Ufaransa, Ujerumani, Luxembourg, Uholanzi pamoja , Umoja wa Mataifa na Benki ya dunia.

 

 

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031