Nyumbani » 24/11/2017 Entries posted on “Novemba 24th, 2017”

MINUSCA yatoa wito wa utulivu baada ya ajali iliyomuua mwanafunzi Bangui

Kusikiliza / Logo_MINUSCA

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA umekaribbisha taarifa ya serikali ya CAR baada ya tukio la ajali ya bahati mbaya  leo asubuhi iliyokatili maisha ya kijana mwanafunzi mjini Bangui. MINUSCA imesikitishwa na kifo hicho na kuungana na serikali kutoa wito wa kudumisha utulivu miongoni mwa wananchi baada ya tukio [...]

24/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kimataifa wa muongo wa watu wa asili ya Afrika wakunja jamvi Geneva

Kusikiliza / Maasai, watu wa asili ya Kenya barani Afrika. Picha: UM

Kamishna mkuu  wa Haki za binadamu  wa Umoja wa  Mataifa Zeid Ra’ad al  Hussein amekemea unyanyaswaji wa watu wenye asili ya Afrika unaoendelea katika nchi mbalimbali  duniani huku sauti zao zikipuuzwa hata wanapoandika historia zao kwenye vitabu ili dunia iweze kujua yanayowasibu. Kamishna huyo mkuu  ametoa kauli hiyo leo huko  Geneva nchini Uswisi, katika hotuba [...]

24/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watu Zaidi ya 230 wauawa kwenye shambulio la kigaidi Misri, UM walaani

Kusikiliza / Bendera ya Misri. Picha UM

Watu takribani 235 wameuawa na wengine zaidi ya 109 kujeruhiwa kwenye shambulio la kigaidi lililofanyika leo huko Sinai nchini Misri. Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio hilo la kikatili lililowalenga waumini waliohudhuria swala ya Ijumaa kwenye msikiti wa Al Rawdah mjini Bir al -Abed. Wajumbe hao wa baraza wametuma [...]

24/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utokomezaji ukatili kwa wanawake sio jukumu la wanawake pekee bali jamii nzima: UM

Kusikiliza / Wasichana wa shule wapazia kukomesha unyanyasaji wa kijinsia huko Dar es Salaam, Tanzania. Picha: UN Wanawake / Deepika Nath

Vita ya kupinga  ukatili dhidi ya wanawake katika mifumo yote ni moja vipaumbele katika  ajenda ya Umoja wa mataifa ya  maendeleo ya mwaka 2030. Juma hili likiwa ni la maadhimisho ya siku yakutokomeza ukatili dhidi ya wanawake duniani itakayofikia kilele chake kesho  tarhe 25 Novemba ,  mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa pamoja na asasi [...]

24/11/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa haki za binadamu ziarani Mali kufuatia taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu

Kusikiliza / Mtaalam huru wa maswala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Suliman Baldo. Picha: UM/Jean-Marc Ferré

Mtaalam huru wa maswala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Suliman Baldo anatarajia kuanza ziara ya kikazi  Mali kuanzia tarehe 27 Novemba hadi 1 Desemba 2017, kutokana na taarifa ya ucheleweshaji unaoendelea katika utekelezaji wa makubaliano ya amani ya nchi humo. Bwana Baldo amesema kuna taarifa ya ukiukwaji wa haki za binadamu mkubwa [...]

24/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Asasi za kiraia zinaweza kuchangia vita dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu: Nelly

Kusikiliza / Usafirishaji haramu wa binadamu. Picha: UNICEF

Wakati Umoja wa mataifa na mashirika yake yanayohusika na masuala ya wakimbizi na wahamiaji wakiendelea kukusanya taarifa kuhusu ripoti za usafirishaji haramu wa binadamu na biashara ya utumwa dhidi ya wahamiaji nchini Libya, wanaharakati kutoka asasi za kiraia wanasema asasi hizo zikiwezeshwa zinaweza kuchangia katika vita hivyo. Leah Mushi na taarifa kamili (LEAH NA TAARIFA [...]

24/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinda amani watatu wa MINUSMA wauawa Mali na wengine kujeruhiwa

Kusikiliza / Maafisa wa UNPOL wa kikosi cha Senegal wanapiga doria nchini Mali. Picha MINUSMA / Marco Dormino

Mapema leo asubuhi walinda amani watatu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA wameuawa nawengine wengi kujeruhiwa huku baadhi wakitajwa kuwa katika hali mahtuti baada ya kushambuliwa kwenye jimbo la Menaka umesema mpango huo. Kwa mujibu wa MINUSMA shambulio hilo limetokea wakati MINUSMA na jeshi la serikali ya Mali FAMAS wakiwa katika operesheni [...]

24/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki: Kichinjamimba

Kusikiliza / Neno la wiki_KICHINJAMIMBA

Wiki hii tunaangazia neno “Kichinjamimba” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Bwana Sigalla anasema Kichinjamimba ni mtoto ambaye amezaliwa mwishoni kabisa katika idadi ya watoto wa mama.

24/11/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

UM wapongeza hatua ya kuruhusu ndege za misaada kuingia Yemeni

Kusikiliza / Waathirika wa mizozo yemen. Picha: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA limefurahishwa na  taarifa ya  ujumbe wake huko Riyad Falme za kiarabu kwamba ndege ya abiria ya shirika hilo UNHAS imeruhusiwa kuanza safari zake  kutoka Amman kwenda Sana'a nchini Yemen kuanzia kesho  Jumamosi. Kwa mujibu wa Jens Laerke msemaji wa OCHA [...]

24/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kurejea kwa Warohingya Myanmar kuzingatie viwango vya kimataifa: UNHCR

Kusikiliza / Hamida, mwenye umri wa miaka 22 (kati) na mtoto wake Mohammed, mwenye umri wa mwaka moja, wanasubiri kupata msaada wa chakula pamoja na mamia ya wakimbizi wengine wa Rohingya katika kambi ya Wakimbizi ya Kutupalong, Bangladesh. © UNHCR / Andrew McConnell

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatambua ripoti kwamba serikali ya Bangladesh na Myanmar zimefikia muafaka wa kurejea Myanmar kwa wakimbizi wa Rohingya. John Kibego na taarifa kamili (TAARIFA YA KIBEGO) Kwa mujibu wa shirika hilo takribani wakimbizi 622,000 walifungasha virago na kukimbia jimbo la Kaskazini la Rakhine nchini Myanmar tangu [...]

24/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031