Nyumbani » 17/11/2017 Entries posted on “Novemba 17th, 2017”

Kwa mara ya tatu baraza la usalama lashindwa kuongeza muda wa JIM:

Kusikiliza / Wajumbe wa baraza la usalama wakipiga kura kuhusu mswada wa kuongeza muda wa JIM. Picha na UM/Kim Haunghtoun

Kwa mara ya tatu ndani ya siku mbili baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Ijumaa limeshindwa kupitisha azimio la jukumu la jopo la kimataifa linalochunguza matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria kutokana kwa sababu ya kura ya turufu ya Urusi nchi ambayo ni mjumbe wa kudumu wa baraza hilo. Jukumu la shirika la [...]

17/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuchukue hatua Mediteranea irejee katika hali yake ya awali- Guterres

Kusikiliza / kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichokutana leo kujadili changamoto za amani na usalama kwenye ukanda wa Mediteranea. Picha: UM

Fursa za kiuchumi na kijamii kwenye ukanda wa Mediteranea ambao kihistoria unatambulika kwa maendeleo ya kitamaduni, hivi sasa ziko mashakani kutokana na ukanda huo kughubikwa na matatizo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hayo akihutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichokutana leo kujadili changamoto za amani na usalama [...]

17/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watoto wapewe kipaumbele katika mjadala wa uhamiaji wa kimataifa

Kusikiliza / Watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakicheza ikionyesha kuwa wana furaha. (Picha:Amanda Nero I IOM 2017)

Wataalam huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema watoto wote wanaokumbwa katika zahma ya uhamiji wanapaswa kutambuliwa kwanza wao ni watoto bila kujali hadhi yao ya uhamiaji au ya wazazi wao. Wataalamu hao wamesema hayo katika chapisho lililotolewa leo kwa minajili ya uhamiaji wa kimataifa. Wamesema watoto ambao wanatambuliwa kuwa ni mtu [...]

17/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki: Bwela Suti

Kusikiliza / Neno-la-wiki_BWELA-SUTI

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno “Bwela Suti”.  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Nuhu anasema "Bwela Suti" ni “apron” au vazi analovaa mtu ili kuzuia uchafu wa mafuta ama vitu vyovyote vile kuharibu nguo zake, [...]

17/11/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Msafiri Zawose aendelea kupigia chepuo muziki wa asili Tanzania

Kusikiliza / Marimba. (Picha: UNESCO)

Muziki wa asili umekuwa haupatiwi kipaumbele na vijana wengi maeneo mbali mbali duniani licha ya kuwa ni sehemu ya utamaduni wao kwani unazungumzia asili yao. Lakini hali ni tofauti kwa mwanamuziki wa muziki wa asili kutoka nchini Tanzania  Msafiri Zawose ambaye licha ya vijana wenzake wengi kujikita katika muziki wa kizazi kipya almaarufu  bongo fleva [...]

17/11/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuna wasiwasi na cambodia baada ya chama cha upinzani kufutwa: Zeid

Kusikiliza / Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'aad al-Hussein. UN/Jean-Marc Ferré

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein ameonyesha hali  ya wasiwasi  juu ya kuwepo kwa uwazi na uhuru kwenye uchaguzi nchini Cambodia baada ya mahakama kuu nchini  humo  kufuta usajili wa chama kikuu cha upinzani kwa miaka mitano. Chama hicho, CNRP ambacho ni kikuu cha upinzani Cambodia kimekuwa [...]

17/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia lazima ishikamane kudhibiti matumizi ya viuavijasumu:WHO

Kusikiliza / Vifaranga vya kuku, WHO linasema wafugaji wasitumie Viua Vijasumu kwa mifugo wenye afya nzuri. Picha: WHO

Wiki ya kampeni dhidi ya matumizi ya viuajisasumu au antibiotic itamalizika Jumapili , huku shirika la afya Ulimwengu WHO  likitoa wito kwa nchi zote duniani kuchukua hatua kudhibiti matumizi mabaya na ya kupindukia ya dawa hizo. Flora Nducha na tarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA) Shirika hilo linasema matumizi mabaya na ya kupindukia ya viuavijasumu yana [...]

17/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yahofia ongezeko la mauaji ya viongozi wa kijamii Colombia

Kusikiliza / Picha ya maktaba kutoka mwaka 2008, inaonyesha watoto wa Afro-Colombia waliokimbia makazi yao katika barrio ya Familias en Acción, iliyojengwa kwenye kisiwa cha Bahari ya Pasifiki katika mji wa Tumaco nchini Kolombia. Picha: UNHCR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatiwa wasiwasi mkubwa kutokana na ongezeko la mauaji na vitisho dhidi ya watetezi wa haki za binadamu na viongozi wa kijamii katika jimbo la pwani ya Pacific nchini Colombia ambapo wahanga katika visa vingi ni kutoka jamii za watu wa asili au za Wacolombia wenye [...]

17/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Nishati ya jua yaleta ahueni kwa warohingya Cox's Bazar- IOM

Kusikiliza / Wakimbizi waRohingya nchini Bangladesh. Picha: IOM

Nishati ya jua imeleta nafuu katika utoaji wa huduma za afya kwenye wilaya ya Cox's Bazar nchini Bangladesh ambako mamia ya maelfu ya wakimbizi warohingya kutoka Myanmar wamesaka hifadhi. Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM limesema wamechukua hatua hiyo ili kuweza kutoa huduma mchana na usiku kutokana na ongezeko kubwa la watu wanaohitaji [...]

17/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nchi zachukua hatua kupambana na usugu wa vijiumbe maradhi: FAO

Kusikiliza / Viua vijasumu husaidia katika matibabu ya magonjwa katika sekta ya kuku na mifugo, lakini matumizi mabaya husababisha kuambukizwa kwa virusi vya kupambana na ugonjwa ambao ni vigumu kutibu. Picha: FAO

Juhudi za kimataifa za kupambana na kuenea kwa usugu wa vijiumbe maradhi mashambani na kwenye mfumo wa chakula zina shika kasi , kutokana na kuungwa mkono na serikali na msaada wa kiufundi unaoziwezesha nchi kukabili tatizo hilo limesema shirika la shakula na kilimo FAO hii leo. Limeongeza kwamba dawa za vijiumbe maradhi zinatumika kwa kiasi [...]

17/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Warohingya sasa watumia vyelezo kukimbia Myanmar- UNHCR

Kusikiliza / Warohingya watumia vyelezo kukimbia Myanmar. © UNHCR/Andrew McConnell

Harakati za warohingya kukimbia nchi yao Myanmar kutokana na mateso zinazidi kutia wasiwasi zaidi wakati huu ambapo wanaendelea kumiminika Bangladesh kwa kutumia usafiri unaotishia zaidi maisha yao. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema hivi sasa warohingya wanatumia vyelezo walivyojitengenezea wenyewe kwa kutumia mianzi na makopo na hivyo kuhatarisha maisha yao majini. [...]

17/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Lengo la usawa wa kijinsia liende sambamba na kutokomeza umaskini- TAMWA

Kusikiliza / TAMWA@30-2

Wakati chama cha waandishi wa habari wanawake nchini Tanzania, TAMWA hii leo kikitimiza miaka 30 tangu kuundwa chake, chama hicho kimesema malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs, yamekuwa ni kichocheo katika kumkwamua mwanamke. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga ameiambia Idhaa hii kuwa lengo namba tano kuhusu usawa wa kijinsia lilionekana kama [...]

17/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031