Nyumbani » 16/11/2017 Entries posted on “Novemba 16th, 2017”

Tanzania tunaelekea kulinda amani CAR na Sudan Kusini- Dkt. Mwinyi

Kusikiliza / FIB-Tanzania2

Mkutano wa masuala ya operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa umekunja huko Vancouver, Canada kwa lengo la kuangazia jinsi ya kuboresha operesheni hizo. Idadi kubwa ya operesheni ziko barani Afrika ambako mizozo na vita imegubika eneo hilo. Miongoni mwa washiriki alikuwa Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa kutoka Tanzania Dkt. [...]

16/11/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Dola Millioni 100 zahitajika kuokoa watu kutokana na majanga

Kusikiliza / Mabadiliko ya tabianchi yaathiri sekta ya uvuvi. Huyu ni vvuvi nchini Sudan. (Picha:World Bank/ Arne Hoel)

Shirika la umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO, linataka hatua zaidi zichukuliwe ili kufanikisha mfuko wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na pia kutoa taarifa mapema uitwao CREWS. Mfuko huo unahitaji dola milioni 100 ifikapo mwaka 2020 ambapo WMO inataka kasi zaidi ya uchangiaji ili kusaidia nchi maskini zilizo katika hatari [...]

16/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Neema ya maji safi kwa wanavijiji wa Buliisa nchini Uganda

Kusikiliza / uganda maji ndogo

Suala la maji safi na salama ni  moja ya mambo muhimu katika ajenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs yenye ukomo wake  mwaka 2030. Katika kufuatilia utekelezaji wa ajenda hiyo, mwandishi wetu nchini Uganda John kibego amepata fursa ya kutembelea wilaya ya Buliisa karibu na ziwa Albert nchini humo ambapo amezungumza na wenyeji  kufuatia tatizo la maji [...]

16/11/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunapopambana na ugaidi lazima tuheshimu haki za binadamu: Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia mkutano kwenye chuo kikuu cha masomo ya Mashariki na Afrika SOAS. Picha: UM/Video capture

Haki za binadamu bila shaka ni shememu kubwa ya suluhu ya vita dhidi ya ugaidi, amesema leo mjini London Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika hotuba yake kwenye chuo kikuu cha masomo ya Mashariki na Afrika SOAS. Ameongeza kuwa”Ugaidi unashamiri wakati watu wasiokuwa na wasiwasi wanapokutana na mitazamo tofauti na kupoteza imani [...]

16/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres awasiliana na AU kuhusu sakata nchini Zimbabwe

Kusikiliza / Bendera ya Zimbabwe. (Picha:UN/Maktaba)

Kufuatia sintofahamu inayoendelea hivi sasa nchini Zimbabwe, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema anafuatilia kwa karibu kinachoendelea huku akisihi utulivu. Vyombo vya habari vinaripoti kuwa hivi sasa jeshi nchini Zimbabwe limeshika hatamu huku Rais Robert Mugabe akiwa ameshikiliwa ndani ya nyumba yake. Kupitia msemaji wake Stephane Dujarric ambaye amezungumza na waandishi wa [...]

16/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kikosi cha kikanda Sudan Kusini kukamilika mwishoni mwa mwaka huu- UNMISS

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, David Shearer(kushoto) akihutubia waandishi wa habari. Picha: UNMISS

Kikosi cha ulinzi cha kikanda, RPF, kinachopelekwa nchini Sudan Kusini kitakuwa kimekamilika ifikapo mwisho wa mwaka huu. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, David Shearer amesema hayo hii leo akizungumza na waandishi wa habari kwenye mji mkuu Juba, akigusia kikundi hicho kinachoundwa na askari kutoka nchi za Afrika. Amesema [...]

16/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vita, umaskini vyaendelea kusababisha utapiamlo Afrika- FAO

Kusikiliza / Vita, umaskini vyaendelea kusababisha utapiamlo Afrika. Picha: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema umaskini, vita na mabadiliko ya tabianchi vimeendelea kuongeza idadi ya watu wenye utapiamlo wa kupindukia kwenye nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara. Flora Nducha na ripoti kamili. (Taarifa ya Flora) Katika ripoti yake iliyozinduliwa leo ikitathmini hali ya upatikanaji chakula na lishe kwenye eneo [...]

16/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usaidizi waendelea kwa manusura wa tetekemo la ardhi Iran na Iraq

Kusikiliza / Eneo mpakani mwa Iraq na Iran. Picha: OCHA

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limeendelea kupeleka vifaa vya matibabu kwa manusura wa tetemeko la ardhi mpakani mwa Iran na Iraq. Vifaa vya hivi karibuni zaidi ni vile vya kusaidia matibabu ya maelfu ya watu waliojeruhiwa na kukumbwa na kiwewe baada ya mkasa huo wa jumapili jioni. Mkurugenzi wa WHO anayehusika na masuala ya dharura [...]

16/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP,UNICEF,WHO watoa ombi kuondoa vizuizi vya misaada ya kibinadamu Yemen

Kusikiliza / Waathirika wa mizozo yemen. Picha: UNHCR

Wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa leo wametoa ombi lingine la pamoja la kutaka kuondolowa haraka vikwazo ili kufikisha misaada ya kibinadamu kwa mamilioni ya watu walio hatarini Yemen. Wakuu hao wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP, la kuhudumia watoto UNICEF na la afya duniani WHO wamesema vizuizi hivyo vya anga, baharini [...]

16/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Vancouver wakunja jamvi kwa ahadi 46 kusaidia operesheni za mani

Kusikiliza / Mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Mataifa wakunja jamvu Vancouver Canada. Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix na Atul Khare wakizungumza wakati wa kufunga mkutano huo jana. Picha na UN News/Matthiew wells.

Ahadi mpya lukuki za vifaa na utaalamu wa kuzifanya operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa kuwa tendaji na zenye ufanisi zaidi zimetolewa kwenye mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa operesheni za Umoja wa Mataifa mjini Vancouver Canada jumatano . Jumla ya nchi wanachama 79 walituma ujumbe wa mawaziri na wakuu wa majeshi [...]

16/11/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uislamu ni dini ya rehema na si ugaidi- Ahmed

Kusikiliza / Ahmed-2

Huko London, Uingereza hii leo kunafanyika mkutano kuhusu masuala ya ugaidi ambapo mmoja wa manusura wa tukio la ugaidi nchini Uganda amezungumza na Idhaa hii akitaka elimu zaidi kwa watoto na vijana ili wasitumbukizwe kwenye ugaidi. Nats.. Hii ni sauti ya manusura wa ugaidi Ahmed Hadji ambaye simulizi  yake inatokana na shambulio la kigaidi nchini [...]

16/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031