Nyumbani » 14/11/2017 Entries posted on “Novemba 14th, 2017”

Mkakati wa kimataifa wa bima wazinduliwa kukabili mabadiliko ya tabia nchi:Thiaw

Kusikiliza / Madhara ya mabadiliko ya tabianchi, hasa ukame wa muda mrefu katika Afrika inasababisha kuongezeka kwa njaa ya kimataifa. Picha: UM

Mkakati wa kimataifa wenye lengo la kutoa bima kwa watu wasiojiweza na masikini zaidi ya milioni 400 ifikapo mwaka 2020 umezinduliwa leo mjini Bonn Ujerumani. Mkakati huo "bima ya mnepo kwa ajili ya mabadiliko ya tabia nchi na hatari ya majanga umeziduliwa wakati wa mkutano unaoendelea wa mabadiliko ya tabia nchi COP23 , ukizileta pamoja [...]

14/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Walinda amani 1000 wa India watunukiwa kwa huduma yao UNMISS

Kusikiliza / Walinda amani wa India watunukiwa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya kujitolea na huduma katika nchi iliyoghubikwa na vita ya Sudan Kusini. Picha: UNMISS

Walinda amani wa India zaidi ya 1000 wametunukiwa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya kujitolea na huduma katika nchi iliyoghubikwa na vita ya Sudan Kusini. Kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS tuzo hiyo inayothaminiwa sana na walinda amani, inatambua wajibu na huduma yao wakiwa kwenye operesheni za kulinda mani, operesheni [...]

14/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kutoka Tanzania hadi Sudan Kusini kusaidia ulinzi wa raia- Meja Paschal

Kusikiliza / Major Raphael Paschal - Tanzania2

Maafisa wa jeshi la wananchi wa Tanzania, JWTZ ni miongoni mwa watendaji katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani huko Sudan  Kusini, UNMISS. Maafisa hao wana majukumu mbalimbali yote yakichangia kufanikisha ulinzi wa raia na amani kwenye taifa hilo change zaidi duniani ambalo sasa limegubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwezi [...]

14/11/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Rohingya wanakabiliwa na unyanyasaji na ukatili wa kingono-IOM

Kusikiliza / Takriban nusu milioni wa wakimbizi wa Rohingya wanaoishi Kutupalong wanahofiwa kunyanyazwa na kuingizwa katika biashara ya usafirishwaji haramu wa wanadamu. Picha: Muse Mohammed / IOM

Wakimbizi wa jamii ya Rohingya waliokimbia machafuko Myanmar na kusaka hifadhi Bangladesh wananyanyaswa. Hiyo ni kwa mujibu wa Shrika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM ambalo linaendesha juhudi za kusaidia zaidi ya wakimbizi 617,000 ambao wamewasili Cox's Bazar tangu Agosti kufuatia operesheni za kijeshi Myanmar. Joel Millman ni msemaji wa IOM (SAUTI YA MILLMAN) [...]

14/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya mjane kutoka Uganda ni msumari wa moto juu ya kidonda-sehemu 2

Kusikiliza / Mjane aliyepitia madhila mengi kufuatia kifo cha mumewe, Magdalena Mbiya Namutebi. Picha: John Kibego

Wakati Umoja wa Mataifa ukichagiza nchi kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma kuelekea ukomo wa malengo ya maendelo endelevu yaani SDGs bado kuna changamoto ambazo huenda zikakwamisha ufikiaji wa malengo hayo. Wanawake na waisichana mara kwa mara wanakabiliwa na aina mbali mbali ya ubaguzi ikiwemo suala la urithi wa mali hususan katika jamii zilizoko nchi [...]

14/11/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mamlaka ya uhamiaji Libya msikiuke haki za binadamu: Zeid

Kusikiliza / Idadi ya wahamiaji waliozuiliwa nchini Limbya katika hali mbaya yaongezeka. Picha: OHCHR

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein leo ameonyesha wasiwasi wake kutokana na ongezeko kubwa la wahamiaji walio  vifungoni katika     vituo mbalimbali  nchini Libya, akisema sera ya Umoja wa Ulaya ya kusaidia ulinzi wa pwani  ya Libya ili kuzuia wahamiaji kuingia barani  humo  inakiuka haki za binadamu. Bwana Zeid amesema mateso ya wahamiaji waliofungwa [...]

14/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali Yemen yaendelea kudorora-UNHCR

Kusikiliza / Watoto nchini Yemen, maisha yao yako hatarini kutokana na mzozo unaoendelea nchini humo. (Picha:OCHA/G.Clarke_Maktaba)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeelezea kusikitishwa kwake na hali inayoendelea kudorora Yemen kufuatia kuendelea kufungwa kwa mipaka ya kuingia nchi hiyo kupitia ardhi, bahari na anga tangu tarehe 6 mwezi huu. Kwa kipindi cha wiki moja kufungwa kwa mipaka kumezuia kuwasilishwa kwa misaada ya kibinadamu na bidhaa za mauzo na  pia kudhibiti safari za watoa [...]

14/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Keating ajadilia amani na usalama na wanawake viongozi Somalia

Kusikiliza / Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa UNSOM Michael Keating, ni mwenyeji wa mkutano wa wanawake viongozi wa Somalia. Picha: UNSOM

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa mpango wa Umoja huo nchini Somalia UNSOM Michael Keating, leo amekuwa mwenyeji wa mkutano wa wanawake viongozi wa Somalia kuzungumzia azimio nambari 1325 la baraza la usalama kuhusu wanawake, amani na usalama. Amessisitiza kwamba mchango wao na wanawake wengine katika jamii ni muhimu [...]

14/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hewa chafuzi kutoka kwenye kilimo itaendelea kwa mwiba kwa tabianchi- FAO

Kusikiliza / Kilimo, misitu na shughuli nyingine za matumizi ya ardhi hutoa tani zaidi ya bilioni 10 za gesi chafuzi. Picha: FAO / Daniel Hayduk

Shirika la chakula na kilimo, FAO limesema kiwango cha hewa chafuzi kutoka katika shughuli za kilimo kitaongezeka siku zijazo na kuleta madhara katika tabianchi. Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva amesema hayo leo huko Bonn, Ujerumani kwenye mkutano wa 23 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP23. Kwa mantiki hiyo [...]

14/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Guterres akutana na Aung San Suu Kyi huko Manila

Kusikiliza / WaRohingya wana wasiwasi kufuatia mashambulizi yaliyofanyinka katika eneo la nchini Myanmar. Picha: UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko ziarani barani Asia amekuwa na mazungumzo na kiongozi mkuu wa Myanmar, Daw Aung San Suu Kyi. Mazungumzo hayo yamefanyika huko Manila, Ufilipino, kando mwa kikao cha viongozi wa umoja wa nchi za kusini na mashariki mwa Asia, ASEAN. Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema viongozi hao [...]

14/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Siku ya kisukari duniani yaangazia wanawake na mustakhbali wao

Kusikiliza / Msichana nchini Jordan ambaye anaugua ugonjwa wa kisukari akijidunga dawa aina ya insulin ili kuweza kuweka sawa kiwango cha sukari mwilini mwake. ((Picha:WHO/ Tania Habjouqa)

Leo ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha dunia kuhusu ugonjwa wa kisukari ambapo shirika la afya ulimwenguni, WHO na wadau wake wanaangazia mustakhbali wa afya ya wanawake katika zama za sasa zilizogubikwa na ugonjwa huo. Flora Nducha na ripoti kamili. (Taarifa ya Flora) WHO inasema wakati wa ujauzito kiwango cha juu cha sukari mwilini huhatarisha [...]

14/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taarifa sahihi zatuwezesha kulinda raia wakati muafaka- Meja Paschal

Kusikiliza / Major Raphael Paschal - Tanzania2

Mchambuzi wa taarifa za wakimbizi wa ndani kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS amesema ukosefu wa taarifa sahihi ni moja ya vikwazo katika kazi yao ya ulinzi wa raia. Akihojiwa na UNMISS, huko mjini Juba nchini Sudan Kusini, Meja Raphael Paschal kutoka Tanzania ametolea mfano ripoti za kubakwa kwa wakimbizi hao [...]

14/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Athari za mabadiliko ya tabianchi hutofautiana kulingana na jinsia: Edna

Kusikiliza / Uhaba wa maji2

Athari za mabadiliko ya tabianchi zinatofautiana kulingana na jinsia na hivyo zahitaji utatuzi muafaka amesema Edna Kaptoyo, Afisa Programu wa mtandao wa jamii asilia nchini Kenya. Katika mahojino na reedio ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabiachi COP23, unaoendelea mjini Bonn, Ujerumani, Bi Kiptoyo ametolea ufafanuzi [...]

14/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031