Nyumbani » 13/11/2017 Entries posted on “Novemba 13th, 2017”

Guterres asisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kongamano la ASEAN

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres akaribishwa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa huko Philippines. Picha: UN in the Philippines

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amesema utandawazi unatoa fursa mpya lakini wakati huo huo unaongeza tofauti ya usawa wa kiuchumi na kijamii, kuongeza wasiwasi na kuweka shinikizo kwa ushirikiano wa kijamii. Bwana Guterres akizungumza huko Manila Ufilipino katika kongamano la umoja wa nchi za Kusini-Mashariki mwa Asia, ASEAN amesema mabadiliko ya tabianchi yanachangia [...]

13/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Viua vijasumu ni hazima tutumie kwa uangalifu- WHO

Kusikiliza / Antibiotics-advice-630

Wiki ya kuhamasisha umma kuhusu usugu wa viua vijasumu imeanza leo ambapo shirika la  afya ulimwenguni WHO linataka jamii ifahamu umuhimu wa kupunguza matumizi ya dawa hizo kwa wanyama na binadamu kama njia mojawapo ya kuepusha matumizi yasiyo sahihi na yasiyo ya lazima. Kupitia wavuti wake, WHO inasema usugu husababisha dawa hizo kushindwa kufanya kazi [...]

13/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji 25 walioko Libya wahamishiwa Niger wakisubiri makazi ya kudumu

Kusikiliza / Wahamiaji katika kizuizini nchini Libya. Picha: Shirika la Uhamiaji wa Umoja wa Mataifa (IOM) / 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limehamisha wahamiaji 25 kutoka Libya kwenda Niger baada ya kubainika kuwa wanaishi kwenye mazingira magumu na hatari zaidi. Msemaji wa UNHCR huko Geneva, Uswisi Cécile Pouilly amesema miongoni mwao ni wanawake 15 na watoto wanne ambapo sasa wanasubiri maombi yao ya kuhamishiwa nchi ya tatu yaweze [...]

13/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ibara kwa Ibara- Tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Ibara kwa Ibara- Tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi disemba mwaka 2018 linatimiza miaka 70. Tamko hilo ni msingi wa haki za binadamu ulimwenguni na lilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1948. Kwa kutambua umuhimu wake, ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inaanza kampeni ya kulipigia chepuo. Nasi [...]

13/11/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

ILO yapendekeza sera kutokomeza ajira kwa watoto ifikapo 2025

Kusikiliza / ILO yatoa wito wa kutokomeza ajira kwa watoto ifikapo 2025. Picha: ILO

Ripoti ya shirika la kazi duniani  ILO imesema kuimarisha ulinzi wa kisheria, usimamizi wa soko la ajira, ulinzi wa kijamii na upatikanaji wa elimu bora na mazungumzo baina ya jamii, serikali na wadau ni muhimu katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa watoto. Ripoti hiyo kwa jina, kumaliza ajira kwa watoto ifikapo 2025: Tathmini ya [...]

13/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ubunifu wa nguo za magome ya miti na uhifadhi wa mazingira Burundi-Sehemu ya II

Kusikiliza / Annika

Katika  Juhudi za kuunda ajira na  kuhifadhi mazingira, msichana kutoka Burundi Annick Kabatesi ameanzisha mradi wa kutengeneza nguo zitokanazo na magome ya miti.  Nguo hizo zimetajwa kuwa zinazingatia uhifadhi wa mazingira. Bi. Kabatesi ambaye ni mwanamitindo pia amejijengea umaarufu mkubwa kwa  kutengeneza nguo hizo za magome ya miti  baada ya nguo hizo kuwavutia viongozi wakuu Serikalini. [...]

13/11/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uharibifu unaochangiwa na migogoro unaathiri elimu Afrika:UNICEF

Kusikiliza / Mtoto anasoma kitabu karibu na Mlango wa shule ya muda nchini Sudan Kusini. Picha: UNICEF

Shule zisizo salama au zilizoharibiwa, kutokuwepo kwa waalimu na safari za hatari kuelekea shuleni ni miongoni mwa uharibifu unaochangiwa na migogo ambao unaathiri mustakbali wa elimu kwa vijana barani Afrika, kwa mujibu wa utafiti mpya wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Matokeo ya utafiti huo uliofanyika katika nchi nne, Jamhuri ya [...]

13/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahanga wa ugaidi tunyanyuke tusonge mbele- Ndeda (VIDEO)

Kusikiliza / James Ndeda

Kuelekea hotuba kuu itakayotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres huko London, Uingereza baadaye wiki hii, mmoja wa wahanga wa tukio la kigaidi nchini Kenya mwaka 1998, ametoa ujumbe wake kwa magaidi. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Huyu ni James Ndeda akizungumza na Idhaa hii jijini New York, Marekani, [...]

13/11/2017 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Zeid kuanza ziara El Salvador tarehe 15 mwezi huu

Kusikiliza / Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'aad al-Hussein. UN/Jean-Marc Ferré

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid zaRa’ad Al Hussein  atatembelea El Salvador kwa mwaliko wa serikali kuanzia tarehe 15 hadi 16 mwezi huu ili kujadili maendeleo na changamoto zinazohusu haki za binadamu nchini humo. Bwana Zeid ambaye atakuwa Kamishna Mkuu wa kwanza wa haki za binadamu kutembelea El Salvador, atakutana [...]

13/11/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM uko tayari kusaidia waathirika wa tetemeko Iran-Iraq

Kusikiliza / UN Photo/John Isaac

Umoja wa Mataifa uko tayari kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Jumapili jioni mpakani mwa Iran na Iraq na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa endapo utahitajika kufanya hivyo. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, akiongeza kuwa ameshtushwa na athari zake, huku akitoa pole [...]

13/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Msaada kutoka kwa papa Francis kusaidia familia Sudan Kusini

Kusikiliza / Uzalishaji wa mboga Yei nchini Sudan Kusini. Picha: UN

Familia zinazokabiliwa na njaa nchini Sudan Kusini zitaweza kuhimili hali hiyo kufuatia msaada wa vikasha vya mboga  vilivyotolewa na kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis wakati huu ambapo uhakika wa chakula unatarajiwa kuwa mashakani zaidi miezi michache ijayo. Zaidi ya watu elfu 30 huko Yei, jimbo la Equatoria kati watanufaika kutokana msaada huo wa Euro 25,000 zilizotolewa na Papa Francis [...]

13/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maarifa na ujuzi wa watu wa asili kutumika kukabiliana na majanga: Kimaren

Kusikiliza / Watu wa asili wa jadi, waandaa kinywaji cha Kava. Picha: UNFCCC

Mkutano wa 23 wa mabadiliko ya tabianchi COP23, ukiwa unaendelea mjini Bonn Ujerumani, jamii ya watu wa asili wameeleza kuwa ujuzi na maarifa ya jamii hizo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi utatumiwa  kuwezesha kukabailiana na majanga. Selina Jerobon na maelezo zaidi. (Taarifa ya Selina) Katika mahojiano na Elie Chansa wa redio washirika Wapo redio [...]

13/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi 80 wanakutana kutathimini operesheni za ulinzi wa amani: UM

Kusikiliza / Atul Khare (Picha: UN Photo/Loey Felipe)

Wawakilishi na mawaziri wa ulinzi kutoka takribani nchi 80 duniani wanakutana kuanzia leo mjini Vancouver Canada ili kutathimini masula ya operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa. Akizungumzia umuhimu wa mkutano huo Atul Khare msaidizi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya msaada mashinani amesema (KHARE-1) "Mkutano huu ni muhimu [...]

13/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031