Nyumbani » 10/11/2017 Entries posted on “Novemba 10th, 2017”

IOM yasaidia wakimbizi kurejea nyumbani CAR

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani 698 kutoka kambi ya muda karibu na kituo cha ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini CAR wanahamishwa. Picha: IOM

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM limekamilisha shughuli ya kuhamisha wakimbizi wa ndani 698 kutoka kambi ya muda karibu na kituo cha ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR, MINUSCA waliochukua hifadhi kufuatia mashambulizi ya 2016 mji wa Kaga Bandoro. Zaidi ya wakimbizi 20,000 kutoka [...]

10/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utamaduni na burudani vyang'aa mkutano COP23

Kusikiliza / COP23 Makala

Mkutano wa 23 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP23 umefanyika wiki hii huko Bonn, Ujerumani, lengo kuu ni kuchagiza mbinu za kukabili mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaendelea kuwa mwiba kwa wakazi wengi duniani. Kando na vikao kumefanyika pia burudani,basi ungana na Grace Kaneiya katika Makala ifuatayo

10/11/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ibara kwa Ibara- Tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Ibara_Tamko. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Kila mtu anastahili kuwa na haki zote na uhuru wote ambao umeelezwa katika tamko hili bila ubaguzi wa aina yoyote kama vile rangi, taifa, jinsia, lugha, dini, siasa, fikra, asili ya taifa la mtu, miliki , kuzailiwa au kwa hali nyingine yoyote. Halikadhalika hakuna ubaguzi utakaotendwa kwa misingi ya kisiasa, kimamlaka au hadhi ya kimataifa [...]

10/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki: Harara

Kusikiliza / Neno la wiki_Harara

Wiki hii tunaangazia neno "Harara" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Bwana Sigalla anasema neno “Harara” lina maana nyingi, ya kwaza ni jinsi mtu anavyohisi kuwashwawashwa kwnye ngozi ya mwili, pili ni hali ya mtu kuwa na hasira mbaya ya ghafla, tatu ni hali [...]

10/11/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Madhara ya mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri tuchukue hatua- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Picha: UM/Video capture

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaja mambo matano atakayopatia kipauembele wakati wa mkutano wa 23 wa mabadiliko ya tabianchi huko Bonn, Ujerumani. Guterres ametaja mambo hayo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini New York, Marekani kabla ya kuanza ziara yake Asia ambayo pia itampeleka hadi Ulaya atakakakoshiriki COP23. Amesema mambo hayo [...]

10/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF na WHO kutoa chanjo dhidi ya surua huko Bangladesh

Kusikiliza / Watoto ma wamama wapanga foleni katika vito vya afya kupokea chanjo dhidi ya surua. Picha: © UNICEF Bangladesh/2014/Kiron

Ongezeko la hofu ya kuwepo kwa wagonjwa wa surura miongoni mwa wakimbizi wapya wa Rohingya waliowasili hivi karibuni nchini Bangladesh, imesababisha mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la kuhudumia watoto, UNICEF na lile la afya, WHO pamoja na serikali ya Bangladesh kuimarisha jitihada za chanjo dhidi ya ugonjwa huo kwenye kambi   za wakimbizi. UNICEF imesema karibu [...]

10/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kuna umuhimu wa kubadili mifumo ya mlo Asia Pasifiki- FAO

Kusikiliza / Wakati usalama wa chakula umeongezeka kwa mamilioni ya watu katika mkoa wa Asia-Pasifiki, njaa na utapiamlo bado iko juu. Picha: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO leo limesema hatua za haraka za kuimarisha lishe na kubadili mifumo ya mlo ni muhimu kwa ajili ya kuwa na chakula bora na chenye afya katika eneo la Asia Pasifiki. Kwa mujibu wa ripoti ya FAO ya mwaka 2017 kuhusu mtazamo wa kikanda juu ya uhakika wa chakula [...]

10/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Haki ya choo India iende sambamba na huduma za maji na kujisafi

Kusikiliza / Haki za binadamu za kupata maji safi na huduma za kujisafi. Picha: UM

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za kupata maji safi na huduma za kujisafi amesema mtazamo wa haki za binadamu unahitajika katika kutokomeza vitendo vya watu kujisaidia hadharani nchini India. Léo Heller ambaye leo kahitimisha ziara ya wiki mbili nchini humo amesema tamko lake linazingatia ukweli kwamba hivi sasa mkakati wa [...]

10/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatua lazima zichukuliwe kusaka suluhu ya wakimbizi:UNHCR

Kusikiliza / Toufic na Rabia walikimbia vurugu huko Al-Qusayr, Syria. © UNHCR / Annie Sakkab

Duru ya mwisho ya majadiliano ya mkakati wa kimataifa kuhusu wakimbizi itafanyika wiki ijayo Novemba 14 na 15 mjini Geneva Uswis , kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kutoa wito wa mapendekezo ya jinsi gani ya kushirikiana kimataifa jukumu la wakimbizi. Majadiliano hayo yatajikita katika kupiga jeshi juhudi za kupata suluhu [...]

10/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tanzania na kasi ya maendeleo endelevu SDGs: Mero

Kusikiliza / SDGs2

Tanzania inatekeleza kwa kasi ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu SDGs kwa kuchukua hatua kadhaa ikiwemo ya awali ya kutafsiri malengo hayo kwa lugha ya Kiswahili na kuelimisha wananchi mashinani namna ya kutumia fursa zilizopo. Selina Jerobon na ripoti kamili. (Taarifa ya Selina) Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa mjini New York, [...]

10/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNISFA imedhamiria kukomesha unyanyasaji na ukatili wa kingono

Kusikiliza / Wanawake waliopitia ukatili wa kingono. Picha: UM

Wakati mkutano wa wiki ya polisi ukiendela hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa  mjini New York Marekani, afisa mshauri wa polisi kwenye mpango wa Umoja wa Mtaifa eneo la Abyei mpakani mwa Sudan na Sudan Kusini UNISFA amesema, mpango huo umedhamiria kukomesha vitendo au nia ya kutekeleza unyanyasaji na ukatili wa kingono. Flora [...]

10/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031