Nyumbani » 09/11/2017 Entries posted on “Novemba 9th, 2017”

Jarida la leo kwenye YOUTUBE #SUBSCRIBE

SUBSCRIBE UNNEWSKiswahili

Sasa waweza pia pata jarida letu kupitia Youtube @UNNewsKiswahili. Katika ukurasa wetu wa Youtube utapata Jarida la kila siku bila kusahau habari za adhuhuri ambazo hatukuweza kukuletea kwenye jarida la asubuhi. Halikadhalika video ya Wiki Hii. SUBSCRIBE ili upate habari kila wakati kutoka Umoja wa Mataifa. Leo tumeangazia kitendo cha nchi kuendelea kuagiza vyakula kutoka [...]

09/11/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Huduma ya afya kwa wazee yaleta nuru Tanzania

Kusikiliza / Idadi ya wazee. Picha: UM

Upatikanaji wa huduma ya afya ni changamoto katika jamii nyingi na hali inakuwa mbaya zaidi kwa wazee kwani mara nyingi licha ya uwepo wa sera, mara kwa mara kundi hili linakabiliwa na ubaguzi. Katika Makala hii tunaelekea mkoani Kagera nchini Tanzania tukiangazia uboreshaji wa huduma ya afya kwa wazee, moja ya kipengele cha malengo ya maendeleo [...]

09/11/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu CAR inazidi kuzorota – MINUSCA

Kusikiliza / MINUSCA walinda amani

Naibu mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini Jamhuri ya Afrika Kati, CAR Najat Rochdi leo katika mkutano na waandishi wa habari  kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani  ametoa tathamini ya hali ya kiusalama na kibinadam nchini humo. Bi Rochdi  amesema hali ya kiusalama na hali ya kibinadamu CAR inazidi kuzorota kutokana migogoro ya wenyewe kwa [...]

09/11/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ibara kwa Ibara- Tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Azimio11

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi disemba mwaka 2018 linatimiza miaka 70. Tamko hilo ni msingi wa haki za binadamu ulimwenguni na lilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1948. Kwa kutambua umuhimu wake, ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inaanza kampeni ya kulipigia chepuo. Nasi [...]

09/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Yemen itatumbukia kwenye janga la njaa kama vizuizi haviondolewi

Kusikiliza / OCHA-Yemen2

Mkuu wa ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa, OCHA Mark Lowcock, amesema iwapo vizingiti vilivyowekwa nchini Yemen havitaondolewa, nchi hiyo sasa inatumbukia kwenye janga la njaa. Amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhutubia kikao cha faragha cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, jijini New York, [...]

09/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

China yaipatia WFP fedha kusaidia wakimbizi Niger

Kusikiliza / Waathirika wa Boko Haram wakimbia kusaka hifadhi. UM

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limekaribisha msaada wa dola milioni 1 kutoka serikali China katika kuchangia shughuli za dharura shirika hilo. Fedha hizo zinalenga kupunguza mateso ya wakimbizi wa ndani na wahamiaji katika eneo la Diffa huko Niger. Sory Ouane ambaye ni mkurugenzi wa WFP Niger amesema fedha hizo zitasaidia juhudi za kuimarisha [...]

09/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya ICC waruhusu kuanza uchunguzi dhidi ya uhalifu nchini Burundi:

Kusikiliza / Jengo la Mahakama ya ICC. Picha: ICC-CPI-20171109-PR1342

Majaji watatu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC leo wameweka hadharani waraka wa kumruhusu mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo kuanzisha uchunguzi dhidi ya uhalifu uliotekelezwa Burundi au na raia wa Burundi walioko nje tangu 26 Aprili 2015 hadi 26 Oktoba 2017. Majaji hao Chang-ho Chung , Antoine Kesia-Mbe Mindua na Raul C. Pangalangan, wamesema [...]

09/11/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Walinda amani wauawa DRC, MONUSCO yaonya ADF

Kusikiliza / Walinda amani wa UM wapiga doria baada ya mashambulizi na mauaji wa wenzao. Picha; MONUSCO

Walinda amani wawili wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO wameuawa na wengine wamejeruhiwa kufuatia shambulio la hivi karibuni kwenye kitongoji cha Mamundioma, karibu na mji wa Beni, jimbo la Kivu Kaskazini. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC na mkuu [...]

09/11/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mpango waanziwa Gambia kusaidia uhamiaji uwe bora zaidi

Kusikiliza / Kutoka kushoto kwenda kulia, wakiwa na bendera: Fumiko Nagano, Mkuu wa Ujumbe wa Gambia IOM; Mai Ahmed Fatty, Waziri wa Mambo ya Ndani; Attila Lajos, Balozi wa EU na Bulli Dibba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani. Picha:  (IOM) 2017

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya na serikali ya Gambia wanatekeleza mpango wa ulinzi na ujumuishaji wa wahamiaji katika jamii. Mpango  huo wa miaka mitatu unagharimu zaidi ya dola milioni 4.5 na unatekelezwa wakati huu ambapo idadi kubwa ya raia wa Gambia wanaokimbia nchi hiyo kusaka hivyo [...]

09/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNAMID yatakiwa kulinda mali na wafanyakazi wa UM kwa gharama yoyote

Kusikiliza / Walinda Amani wa mpango wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika wa kulinda Amani Darfur Sudan UNAMID. Picha: UNAMID

Walinda Amani wa mpango wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika wa kulinda Amani Darfur Sudan UNAMID, wametakliwa kuhakikisha mbali ya kulinda raia wanawalinda wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na mali za Umoja huo kwa gharama yoyote. Mwandishi wa UNAMID Luteni selemani Semunyu na ripoti kamili. (TAARIFA YA SELEMANI) Agizo hilo limetolewa na naibu [...]

09/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uagizaji wa vyakula duniani waongezeka licha ya ongezeko la uzalishaji- FAO

Kusikiliza / Wakulima watayarisha bidhaa za chakula kwa ajili ya kusafirisha. Picha: FAO

Wakati bei za bidhaa za chakula zimeimarika kwa muda duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limesema gharama ya uagizaji chakula kutoka nje ya nchi imeongezeka mwaka huu wa 2017 na kufikia  karibu dola bilioni 1.5, ikiwa ni ongezeko la  asilimia 6 kutoka mwaka uliopita. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA) FAO inasema uagizaji [...]

09/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kesi ya ukatili kwa watoto DRC yaanza kusikilizwa leo huko Bukavu

Kusikiliza / Mahakama ya kijeshi huko Bukavu jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Picha: MONUSCO

Mahakama ya kijeshi huko Bukavu jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC leo alhamisi inaanza kusikiliza kesi ya watuhumiwa 18 wanaoshtakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kibinadamu dhidi ya watoto wapatao 51. Yadaiwa kuwa watu hao waliokuwa wamejihami walitenda uhalifu huo kati ya mwezi mei mwaka 2013 hadi mwaka 2016 kwenye [...]

09/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031