Nyumbani » 08/11/2017 Entries posted on “Novemba 8th, 2017”

Uhalifu dhidi ya wahamiaji Libya unaweza kuwajibishwa kupitia ICC

Kusikiliza / Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, Fatou Bensouda akitoa taarifa leo kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Libya. Picha na UM/Eskender Debebe

Uhalifu dhidi ya wahamiaji waliofungwa au kusafirishwa kwa njia haramu kupitia Libya unaweza kuwajibishwa chini ya mamlaka ya  mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC. Kauli hiyo imetolewa na mwendesha mashtaka wa ICC, Bi Fatou Bensouda, akihutubia kikao cha Baraza la Usalama kilichokutana leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kujadili hali nchini Libya. Bi [...]

08/11/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Programu ya uanagenzi ya ILO yaleta nuru kwa vijana Tanzania

Kusikiliza / Wanagenzi 2 TZ 1

Shirika la Kazi Duniani ILO kwa kushirikiana na Serikali ya Norway wamesaidia vijana kwenye ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika kuboresha stadi zao katika biashara na pia kuwapa fursa za ajira katika sekta mbalimbali kama vile za hoteli na utalii. Hii ni sehemu ya uanagenzi wa kuhakikisha wanafunzi wanapata mafunzo ya kinadharia na vitendo [...]

08/11/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Brazil inatakiwa kuendeleza vita dhidi ya utumwa wa kisasa UM

Kusikiliza / Idadi kubwa ya watut wanakabiliwa na changamoto ya utumwa kisasa kote ulimwenguni. Picha: ILO

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa  leo wametoa wito kwa serikali ya Brazil kuchukua hatua za haraka katika  mapambano  dhidi ya utumwa wa kisasa unaodhoofisha kanuni za ushirika. Urmila Bhoola ambaye ni mtalaam huru wa haki za binadam wa Umoja wa Mataifa amesema, vitendo vya utumwa wa kisasa vinaongeza nchini humo na [...]

08/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM inasikitishwa na athari za kibinadamu kufuatia ukatili Ukraine Mashariki

Kusikiliza / Raia nchini Ukraine wahaha kusaka suluhu ya amani. Picha: UNHCR

UM wasikitishwa na athari za kibinadamu kufuatia ukatili  huko kraine Mashariki. Umoja wa Mataifa umeelezea masikitiko yake kufuatia ongezeko la ukatili karibu na maeneo yenye miundombinu ya kusambaza maji, umeme na gesi katika jimbo la Donetsk huko Ukraine Mashariki. Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa na mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Ukraine Neal Walker amesema katika taarifa yake [...]

08/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wanaotawanywa na mabadiliko ya tabia nchi inaongezeka:UNHCR

Kusikiliza / Wakazi wa Sudan wanaohama kufuatia mafuriko. Picha: UNAMID

Idadi ya watu wanaotawanywa na athari za mbadiliko ya tabia nchi ikiwemo ukame, mafuriko, vimbunga na majanga mengine inaongezeka , kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa leo kwenye mkutano wa mabadilko ya tabia nchi COP23 unaoendelea nchini Ujerumani. Akizungumza na UN news kandoni mwa mkutano huo [...]

08/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNESCO yalaani mauaji ya mfanyakazi wa Televishen ya Shamshad Afghanistan

Kusikiliza / UNESCO limesisitiza usalama wa waandishi wa habari. Picha: UNESCO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova , leo amelaani vikali mauaji ya mfanyakazi wa televisheni ya Shamshad, yaliyotokea jana mjini Kabul  Afghanistan baada ya mtu mwenye silaha kuvamia ofisi za televisheni hiyo na kujeruhi pia wafanyakazi wengine kadhaa. Bokova ametuma salamu za rambirambi kwa [...]

08/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zambia yazindua mkakati wa ujumuishaji wananchi katika sekta ya fedha

Kusikiliza / Idadi ya wanawake wanaojiunga rasmi na sekta ya kifedha inaongezeka kwa kasi Zambia. Picha: World Bank Zambia

Serikali ya Zambia hii leo kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wamezindua nyaraka tatu muhimu zenye lengo la kuendeleza na kuimarisha sekta ya kifedha nchini humo. Uzinduzi wa nyaraka hizo, mkakati wa ujumuishwaji wa wananchi kwenye sekta ya fedha, sera ya uendelezaji wa sekta ya fedha na ripoti kuhusu uwezo wa kifedha  umefanyika mjini Lusaka, [...]

08/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Urusi yageuza madeni ya Msumbiji kutoa mlo mashuleni:WFP

Kusikiliza / Wanfunzi wapokea chakula shuleni. Picha: WFP

Mpango wa kubadili madeni kati ya Shirikisho la Urusi na serikali ya Msumbiji umeweka ahadi ya dola milioni 40 za Marekani, ambazo zitatumiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) ili kusaidia Serikali ya Msumbiji kutoa mlo mashuleni  kwa watoto 150,000 nchini humo kwa zaidi ya miaka mitano ijayo. Mbali [...]

08/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kijitabu chazinduliwa kuimarisha afya kwenye sekta ya kilimo cha ndizi

Kusikiliza / Wakulima wa ndizi. Picha: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kwa kushirikiana na serikali  ya Ecuador leo wamezindua kijitabu cha maelekezo chenye lengo la kuboresha mazingira ya kazi na afya ya wafanyakazi wanaozalisha ndizi. FAO kupitia taarifa yake inasema mahitaji ya ndizi ni makubwa duniani na kutokana na hali hiyo wamiliki wa sekta hiyo hutumia kila mbinu kupunguza [...]

08/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna mwamko wa masomo ya STEM kwa vijana-Olwendo

Kusikiliza / Kambi za Sayansi katika STEM (Kenya) za kushauri Wasichana kwamba wanaweza masomo ya sayansi. Picha: © UNESCO/ Alice Ochanda

Masuala ya kisayansi na hususan masomo ya sayansi yamewapa vijana motisha na hivi sasa kundi hilo linaonekana kuwa na mtazamo chanya kuhusu masomo hayo kwani wametambua fursa zinazoweza kupatikana kikazi kufuatia kujikita na masomo hayo. Hii ni kauli ya Dkt Joseph Ouko Olwendo, mhadhiri katika chuo kikuu cha Pwani nchini Kenya anayehudhuria mkutano wa masuala [...]

08/11/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tanzania na kasi ya kuimarisha viwanda ili vichochee ukuaji uchumi

Kusikiliza / Mvuvi huko Zanzibar2

Tanzania imetaja mambo inayozingatia hivi sasa katika mwelekeo wake wa kukuza sekta ya viwanda nchini humo kama njia mojawapo ya kuchochea uchumi. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango nchini humo Dkt. Khatibu Kazungu amesema hayo huko Moroni, Comoro anakoshiriki mkutano wa 21 wa kamati ya wataalamu wa serikali ya Tume ya Uchumi [...]

08/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031