Nyumbani » 07/11/2017 Entries posted on “Novemba 7th, 2017”

Serikali ya Syria na Daesh walitumia silah za maangamizi-JIM Ripoti

Kusikiliza / Bwana Edmund Mulet, ambaye ndiye mkuu wa  JIM akihutubia Baraza la Usalama. Picha: UM/Cia Pak

Kikosi kazi  cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na shirika la kupinga matumizi ya silaha za maangamizi OPCW kijulikanacho kama JIM  leo kimewasilisha ripoti yake  ya uchunguzi kuhusu matumizi ya silaha za kemikali  nchini Syria kwenye kikao cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York  Marekani na kusema pasi shaka silaha hizo [...]

07/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hali ya mjane kutoka Uganda ni msumari wa moto juu ya kidonda-sehemu 1

Kusikiliza / Mjane aliyepitia madhila mengi kufuatia kifo cha mumewe, Magdalena Mbiya Namutebi. Picha: John Kibego

Wakati Umoja wa Mataifa ukichagiza nchi kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma kuelekea ukomo wa malengo ya maendelo endelevu yaani SDGs bado kuna changamoto ambazo huenda zikakwamisha ufikiaji wa malengo hayo. Wanawake na waisichana mara kwa mara wanakabiliwa na aina mbali mbali ya ubaguzi ikiwemo suala la urithi wa mali hususan katika jamii zilizoko nchi [...]

07/11/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Jarida la leo kutoka Youtube #SUBSCRIBE

SUBSCRIBE UNNEWSKiswahili

Sasa waweza pia pata jarida letu kupitia Youtube @UNNewsKiswahili. Katika ukurasa wetu wa Youtube utapata Jarida la kila siku bila kusahau habari za adhuhuri ambazo hatukuweza kukuletea kwenye jarida la asubuhi. Halikadhalika video ya Wiki Hii. SUBSCRIBE ili upate habari kila wakati kutoka Umoja wa Mataifa. Leo tumeangazia COP23 kutoka Bonn, Ujerumani, Benki ya Dunia [...]

07/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamii asilia zijengewe uwezo wa kunepa dhidi ya tabianchi: Pingos Forum

Kusikiliza / COP23 wjadili mabadiliko ya tabianchi. Picha: WMO

Mkutano wa 23 nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP23, umeingia siku ya pili hii leo mjini Bonn Ujerumani, mwelekeo ukiwa ni kuhakikisha wakazi wa dunia wananusuriwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi yakiwemo majanga ya asili. Selina Jerobon na ripoti zaidi. (Taarifa ya Selina) Hii leo mada iliyogubika mijadala katika COP23 ni [...]

07/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Acheni kutumia viuavijasumu ili kuzuia usugu wa dawa:WHO

Kusikiliza / Kuku, WHO linasema wafugaji wasitumie Viua Vijasumu kwa mifugo wenye afya nzuri. Picha: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO linapendekeza wakulima na sekta ya chakula kuacha matumizi ya viuavijasumu au antibiotics mara kwa mara ili kukuza haraka mifugo na kuzuia magonjwa kwa wanyama wenye afya. Mapendekezo hayo mapya ya WHO yaliyotolewa leo yanalenga kusaidia kulinda uwezo wa dawa za viuavijasumu ambazo ni muhimu kwa matumizi ya binadamu kwa kupungua [...]

07/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maiti 26 za wanawake waliosafirishwa kiharamu zawasili Italia:IOM

Kusikiliza / Meli za usafirishaji wa wahamiaji na waokoaji Mediterranan. Picha: IOM

Maiti za wanawake 26 wanaosadikiwa kufanya safari ya kuelekea barani Ulaya kwa kupitia wasafirishaji haramu zimewasili nchini Italia, huku idadi ya wahamiaji kwa mwaka huu 2017 ikikarinia 155,000 na vifo Zaidi ya 2900. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, likisema asilimia 70 ya wahamiaji [...]

07/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yazindua huduma ya VVU katika vituo vya wakimbizi Sudan Kusini

Kusikiliza / Mwanamke muathirika wa polio anajibu maswali kuhusu HIV huko Bentiu nchini Sudan Kusini. Picha: IOM

Maelfu ya watu sasa watapata huduma ya ushauri, kupima na tiba dhidi ya virusi vya ukimwi, VVU nchini Sudan Kusini kufuatia shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM kuzindua huduma hizo katika vituo vya kulinda raia vya Bentiu, Malakal na Wau mwezi uliopita. Vituo hivyo vinalenga kusaidia takriban watu 171,000 na jamii zinazowahifadhi. IOM imesema [...]

07/11/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Venezuela heshimu haki za binadamu – IPU

Kusikiliza / IPU Logo

Umoja wa mabunge duniani, IPUumeeleza wasiwasi wake juu ya uamuzi wa Mahakama Kuu nchini Venezuela ya kutaka bunge la nchi hiyo liondoe kinga ya hadhi ya ubunge kwa mbunge Freddy Guevara, ambaye ni Naibu Spika wa bunge hilo. Habari zinasema kuwa Guevara ambaye ni mwanasiasa wa upinzani na mashuhuri nchini Venezuela anatakiwa kufunguliwa mashtaka kwa [...]

07/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tanzania iimarishe sekta ya maji ili kuchochea maendeleo- Ripoti

Kusikiliza / Msichana anasimama katibu na mradi wa maji ulioharibika nchini Tanzania Picha: World Bank Tanzania

Tanzania inahitaji kuboresha haraka usimamizi wa vyanzo vyake vya maji ili uhaba wa maji usiwe kikwazo cha maendeleo. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Benki ya Dunia iliyozinduliwa jijini Dar es salaam, Tanzania ikisema kuwa uhaba wa maji hivi sasa unatokana na ongezeko kubwa la mahitaji. Mathalani ripoti imesema kiwango cha matumizi ya [...]

07/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mfululizo wa mashambulizi Yemen unasikitisha-OHCHR

Kusikiliza / Familia waathirika wa mashambulizi nchini Yemen. Picha: OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasiwasi wake kufuatia mfululizo wa mashambulizi nchini Yemen katika kipindi cha wiki moja iliyopita ambapo makumi ya raia wameuawa wakiwemo watoto. Ofisi hiyo imetaka pande husika kwenye mzozo huo kuzingatia sheria ya kimataifa ambayo inalinda raia wakati wa mzozo na mashambulizi dhidi ya raia au [...]

07/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna ongezeko kubwa la mashambulizi dhidi ya dini Afghanistan: UNAMA

Kusikiliza / Moja ya majengo yaliyoshambuliwa na wapiganaji wenye silaha nchini Afghanistan. Picha: UNAMA / F. Mzoezi

Kuna ongezeko kubwa dhidi ya mahali pa kuabudu, viongozi wa dini na waumini nchini Afghanistan ikiwemo mashambulizi kwenye misikiti ya Waislam wa Shia na waumini wao. Taarifa hizo zimo katika ripoti maalumu iliyotolewa leo na mapango wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA ikiorodhesha ongezeko la mashambulizi hayo na athari zake kwa raia. Tangu Januari [...]

07/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR yakamilisha awamu ya kwanza ya kuhesabu warohingya

Kusikiliza / Mfanyakazi wa kujitolea wa UNHCR anaendelea na shughuli za kusajili waRohingya huko Bangladesh. Picha: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,UNHCR, limekamilisha awamu ya kwanza ya kuhesabu kaya za waislamu wa kabila la Rohingya huko nchini Bangladesh. Hadi sasa zaidi ya kaya laki moja na elfu ishirini zimehesabiwa huku ikidhihirika kuwa theluthi moja ya kaya hizo ziko hatarini zaidi kutokana na ukosefu wa huduma za msingi. Msemaji wa [...]

07/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkataba wa amani Sudan Kusini ndio muarobaini wa yote- Akodjenou

Kusikiliza / Mtoto ambaye ni mkimbizi wa ndani akiezeka paa la nyumba yao huko Yei kufuatia mzozo nchini mwao Sudan Kusini2

Mratibu wa kanda wa masuala ya wakimbizi nchini Sudan Kusini, Arnauld Akodjenou amesema mkataba wa amani  nchini humo ndio muarobaini wa mzozo unaoendelea nchini humo wakati huu ambapo wananchi wamechoshwa na machungu waliyopitia. Akihojiwa na radio Miraya ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, Bwana Akodjenou amesema simulizi za wakimbizi walio ndani [...]

07/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031