Nyumbani » 06/11/2017 Entries posted on “Novemba 6th, 2017”

Jarida sasa lapatikana kupitia Youtube #Subscribe

SUBSCRIBE UNNEWSKiswahili

Sasa waweza pia pata jarida letu kupitia Youtube @UNNewsKiswahili. Katika ukurasa wetu wa Youtube utapata Jarida la kila siku bila kusahau habari za adhuhuri ambazo hatukuweza kukuletea kwenye jarida la asubuhi. Halikadhalika video ya Wiki Hii. SUBSCRIBE ili upate habari kila wakati kutoka Umoja wa Mataifa.

06/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wiki ya polisi ikianza UM, mchango wao ni muhimu kwa operesheni za ulinzi:Carrilho

Kusikiliza / Mshauri mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya polisi Luis Carrilho.(Picha:UM/Video Capture)

Juma hili makamishina wa polisi wa Umoja wa Mataifa kutoka katika sehemu mbalimbali za operesheni za amani za Umoja huo wamekusanyika kwenye makao makuu hapa mjini New York Marekani kuanzia leo ili kuwasilisha ripoti zao kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Mshauri mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya polisi Luis [...]

06/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MINUSCA imejizatiti kusaidia CAR kupata amani

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu mkuu nchini CAR Parfait Onanga- Anyanga .(Picha:UNIfeed/video capture)

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili hali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo Mwakilishi maalum wa Katibu mkuu nchini CAR Parfait Onanga- Anyanga  amesema ombi la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kutaka kuongezwa kwa vikosi vya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, [...]

06/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uandishi wa habari uko hatarini kote ulimwenguni-UNESCO

Kusikiliza / PRESS

Uandishi wa habari uko katika hatari ya kuvamiwa kote ulimwenguni ukizingatia migawanyiko ya kisiasa na mabadiliko ya teknolojia ambayo inachagiza kuenezwa kwa haraka chuki na habari bandia ambazo mara nyingi huchangia udhibiti wa uhuru wa kujieleza. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO iliyotolewa [...]

06/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Chondechonde Hong Kong watendeeni haki wanaharakati wa demokrasia:UM

Kusikiliza / UNHRC Logo

Jopo la watalam  wa haki za kibinadamu wa  Umoja wa  Mataifa wameiasa mamlaka ya Hong Kong kuheshimu ahadi zake katika kutekeleza haki za binadamu kwa  wanaharakati wa kidemokrasia watatu watakaokata rufaa kupinga  hukumu zao tarehe 7 Novemba. Wanaharakati hao Joshua Wong, Nathan Law na Alex Chow walifungwa mwezi Agosti ambapo mmoja kati yao alihukumiwa kwa [...]

06/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ubunifu wa nguo za magome ya miti na uhifadhi wa mazingira Burundi-sehemu 1

Kusikiliza / Mwanaharakati wa mazingira  Annick Kabatesi kutoka Burundi. Picha: Annick Kabatesi

Katika  Juhudi za kuunda ajira na  kuhifadhi mazingira, msichana kutoka Burundi Annick Kabatesi ameanzisha mradi wa kutengeneza nguo zitokanazo na magome ya miti.  Nguo hizo zimetajwa kuwa zinazingatia uhifadhi wa mazingira. Bi. Kabatesi ambaye ni mwanamitindo pia amejijengea umaarufu mkubwa kwa  kutengeneza nguo hizo za magome ya miti  baada ya nguo hizo kuwavutia viongozi wakuu Serikalini. [...]

06/11/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNEP kuanzisha mafunzo ya kimtandao kuhusu ulinzi wa mazingira ya asili

Kusikiliza / Uharibifu wa wa mazingira. Picha: UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP limeanzisha mafunzo ya kimtandao kuhusu  ulinzi wa mazingira  ikiwa ni hatua muhimu katika kukomesha  migogoro juu ya rasilimali za asili  ambayo ni changamoto kubwa katika siasa ya karne ya 21 na kuhatarisha usalama wa binadamu. Hiyo ni mujibu wa Erik Solheim said ambaye ni mkurungezi [...]

06/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kinga na vipimo mapema vyahitajika kudhibiti saratani kwa vijana chini ya maiaka 40:WHO

Kusikiliza / Vijana wachukua picha ya pamoja katika siku ya vijana Agosti mwaka huu. Picha: UM

Hatua za haraka zinahitajika ili kuzuia saratani miongoni mwa vijana wa umri wa miaka 20-39. Selina Jerobon na taarifa kamili (TAARIIFA YA SELINA) Wito huo umetolewa na shirika la kimataifa la utafiti wa saratani IARC ambalo ni sehemuya shirika la afya ulimwenguini WHO. Kimataifa kwa mujibu wa takwimu za ripoti mpya ya shirika hilo kulikuwa [...]

06/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchaguzi mkuu DRC sasa kufanyika disemba mwaka 2018

Kusikiliza / Wafanyakazi wa CENI DRC waendelea kusajili wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi ujao. Picha: MONUSCO

Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, CENI, imetangaza kuwa uchaguzi mkuu nchini humo sasa utafanyika mwezi disemba mwakani 2018 badala ya mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali. Radio  Okapi ambayo ni ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO imemnukuu Rais wa CENI Corneille Nangaa akitangaza mjini Kinshasa kuwa uchaguzi [...]

06/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sera za nishati, nyuklia na tindikali baharini kupewa kipeumbele COP23:IAEA

Kusikiliza / IAEA litatoa kipaumbele kwa masuala ya sera za nishati, maendeleo endelevu, uwezo wa nyuklia, mabadiliko ya tabia nchi na mustakhbali wa bahari.Picha: IAEA

Wakati mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi COP23 umen'goa nanga leo mjini Bonn Ujerumani, shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA limesmea litatoa kipaumbele kwa masuala ya sera za nishati, maendeleo endelevu, uwezo wa nyuklia, mabadiliko ya tabia nchi na mustakhbali wa bahari. Shirika hilo limesema lengo lake kuu katika mkutano huo ni kuelimisha [...]

06/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

COP23 yaanza Bonn, kazi bado kubwa kukabili mabadiliko ya tabianchi- UNFCCC

Kusikiliza / COP23 2017

Mkutano wa 23 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP23 umeanza hii leo huko Bonn, Ujerumani ikielezwa kuwa bado kuna kazi kubwa kuweza kukabili mabadilio ya tabianchi ambayo yanaendelea kuwa mwiba kwa wakazi wengi duniani. Patrick Newman na taarifa zaidi. (Taarifa ya Patrick) Nats.. Kibao hicho I am an island, mimi ni [...]

06/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mavuno ya chakula Sudan Kusini si suluhu ya janga la njaa- Ripoti

Kusikiliza / Mwanamke anavuna mtama kutoka kwa shamba yake nchini Sudan Kusini. Picha: FAO

Msimu wa sasa wa mavuno nchini Sudan Kusini hautamaliza janga la njaa linalokabili nchi hiyo wakati mzozo wa vita ukiendelea. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya uhakika wa chakula iliyotolewa leo na serikali ya Sudan Kusini kwa ushirikiano na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la chakula na kilimo FAO, lile la watoto, [...]

06/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwaka 2017 kuvunja rekodi ya kuwa na joto kali:WMO

Kusikiliza / Moshi uliosababishwa na moto wa msituni ukitanda. Picha na shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO.

Ripoti mpya ya shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO iliyotolewa leo inasema inawezekana mwaka 2017 ukawa miongoni mwa miaka mitatu iliyovunja rekodi ya kuwa na jioto kali katika historia ukighubikwa na majanga makubwa kama vimbunga, mafuriko, mawimbi joto na ukame. Ripoti hiyo ya hali ya hewa 2017 inayoainisha athari zake kwa usalama [...]

06/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031