Nyumbani » 02/11/2017 Entries posted on “Novemba 2nd, 2017”

Jukwaa la ujasiriliamali na uwekezaji lakunja jamvi Bahrain

Kusikiliza / Miroslav Lajčák, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa(kulia), anapokea taarifa ya matokeo kutoka kwa Hashim Hussein, Mkuu wa UNIDO ITPO-Bahrain na Katibu Mtendaji wa WEIF 2017 (kati), huku Samir Aldarabi, Mkurugenzi wa UNIC-Manama akitizama. Picha: UM/ UN News center

Jukwaa la Umoja wa Mataifa limekunja jamvi hii leo nchini Bahrain kwa wito wa kujumuisha ujasiriamali na ubunifu kama njia za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDG's). Washiriki 1000 kutoka nchi 90, ikiwemo asilimia 60 ya wanawake wameshiriki kwenye jukwaa hilo la kimataifa la 'ujasiriamali na uwekezaji 2017" lililofanyika katika mji mkuu Manama. Jukwaa [...]

02/11/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tuangazie yanayotuweka pamoja badala ya migawanyiko- Ruteere

Kusikiliza / Mutuma Ruteere akihojiwa na Joseph Msami wa UM2

Katika zama za sasa, siasa zinaghubikwa na mwelekeo wa baadhi ya vyama kujipatia umaarufu kupitia ajenda za kibaguzi kutoka kwa wafuasi wao. Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya haki za binadamu imekuwa ikipaza sauti kupinga mwelekeo huo ukisema kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Hoja hiyo na nyingine nyingi ni miongoni mwa [...]

02/11/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO kudhibiti hatari ya kusambaa tauni Afrika Mashariki na Kusini

Kusikiliza / Timu ya wahudumu wa WHO na Wizara ya Afya ya Seychelles waimarisha jitihada za kuzuia usambazaji wa tauni katika bandari Seychelles. Picha: WHO/E. Musa

Shirika la afya Ulimwengu limechukua hatua za haraka ikiwemo kutoa fedha, kupeleka vifaa na kutuma wataalamu nchini Madagascar huku likizisaidia nchi jirani kupunguza hatari ya kusambaa kwa ugonjwa wa tauni katika kanda nzima. Tangu Agosti 2017 visa takribani 1800 vinavyoshukiwa kuwa ni tauni vimeripotiwa Madagascar na watu 127 wameshafariki dunia kutokana na ugonjwa huo. WHO [...]

02/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Je tumeshindwa kuleta amani? Ahoji mkuu wa UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi22

Kamishna Mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR Filippo Grandi leo amehutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuhoji iwapo jamii ya kimataifa imeshindwa kuleta amani kwani mizozo na vita inafurusha watu makwao kila uchao. Ikiwa ni hotuba ya kwanza kwa mkuu wa UNHCR tangu mwaka 2009, Grandi amesema idadi ya watu [...]

02/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ISIL ni lazima ikabiliwe na makosa ya uhalifu wa kimataifa: UM

Kusikiliza / Hospitali ya Al Salam iliyoko kusini mwa Mosul. Picha: OCHA / Themba Linden

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kufuatia ukombozi wa mji wa Mosul nchini Iraq inasema kundi la kigaidi la ISIl au Daesh lilitekeleza vitendo vya ukiukwaji wa hali ya juu wa haki za binadamu ambavyo ni uhalifu wa kimataifa katika kipindi cha miezi tisa ya kampeni ya kijeshi ya ukombozi wa mji huo. Ripoti hiyo iliyochapishwa [...]

02/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa kuhara bado tishio kwa watoto Afghanistan- UNICEF

Kusikiliza / Wanafunzi wavulana wang'ang'ania pampu ya mkono kunywa maji shuleni katika jiji la Mazar, kaskazini mwa Afghanistan. Picha: UNICEF_2011(Maktaba)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema ugonjwa wa kuhara umesalia tishio miongoni mwa watoto nchini Afghanistan ingawa idadi ya vifo vimepungua kwa mara ya kwanza na kuwa chini ya 10,000 wakati huu. Saidi Adele Khodr ambaye ni mwakilishi wa UNICEF Afghanistan amesema ugonjwa huo ni tishio kwa kuwa kila siku husababisha [...]

02/11/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

FAO yachapisha kitabu cha mienendo ya uhamiaji vijijini

Kusikiliza / Kitabu cha uhamiaji katika vijiji barani Africa. Picha: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO leo kimechapisha kitabu cha ramani kinachorahisisha uelewa wa mwenenendo wa uhamiaji kwenye maeneo ya vijijini katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara. Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa FAO anayehusika na masuala ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii Kostas Stamoulis amesema hatua hiyo ni kwa kuzingatia kuwa [...]

02/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi wachangiaji wa vikosi AMISOM kulipwa fidia ya vifaa vyao:UNSOS

Kusikiliza / Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa wa AMISOM. Picha: AMISOM

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi nchini Somalia (UNSOS) kwa kushirikiana na mpango wa ulinzi wa amani wa Muungano wa Afrika nchini humo AMISOM na Muungano wa Afrika AU wamefanya warsha ya siku mbili mjini Moghadishu  kutathimini mapendekezo ya bodi inayohusika na viwango na utaratibu wa operesheni za ulinzi (SOP) kwa ajili ya kulipa [...]

02/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali zikomeshe mashambulizi dhidi ya wanahabari

Kusikiliza / UNESCO-3

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukwepaji sheria wa vitendo vya  uhalifu dhidi ya waandishi wa habari, imeelezwa kuwa maisha ya waandishi wa habari yamesalia hatarini hata wanapokuwa katika harakati za kuandika habari kwenye maeneo yao. Katika ujumbe wake wa siku hii, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi [...]

02/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNMISS itahakikisha imewafikia raia walioko vijijini-Shearer

Kusikiliza / mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa UNMISS David Shearer alipozuru mji wa Akobo.(Picha:UNMISS)

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wantarajiwa kuwafikia maelfu ya watu wasiojiweza katika maeneo ya vijijini nchini Sudan Kusini wakati mpango  wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS ukitumia mbinu mpya na ufanisi. Grace Kaneiya na taarifa kamili (TAARIFA YA GRACE) Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa UNMISS [...]

02/11/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031