Ubia wa Benki ya Dunia na UNHCR kuboresha takwimu za waliofurushwa makwao

Kusikiliza /

Takwimu za wakimbizi na wahamiaji ni muhimu. Picha: UNHCR

Benki ya Dunia na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameingia ubia mpya ili kuanzisha kituo cha pamoja cha takwimu kwa ajili ya watu waliolazimika kutawanywa ili kuboresha takwimu za wakimbizi, watu waliotawanywa na jamii zinazowahifadhi.

Kituo hicho kilichotangazwa leo katika kuadhimisha siku ya takwimu duniani kitasaidia kutoa taarifa vyema na kuchukua hatua endelevu kwa ajili ya waliolazimika kutawanywa, na kusaidia juhudi za uratibu wa mtazamo wa maendeleo wa masuala ya kibinadamu

Imetokana na mfano wa UNHCR kama taasisi ya takwimu za wakimbizi, ukijumuisha utaalamu wa Benki ya Dunia na uzoefu wake vitazisaidia serikali kuboresha uwezo wa ukusanyaji wa takwimu.

Akizungumzia hatua hiyo Kamishina Mkuu wa wakimbizi bwana Filippo Grandi amesema ukubwa na upana wa zahma ya wakimbizi leo hii inamaanisha kwamba haiwezekani kuchukua hatua za kibinadamu pekee, ni muhimu sana kuliko wakati mwingine wowote kukusanya rasilimali na kuwa na mipango ya muda mrefu tangu mwanzo na takwimu sahihi zinasaidia katika hili. Kituo hicho kinatarajiwa kuwa tayari na kuanza kazi rasmi katikati ya mwaka 2018.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930