Madagascar bado iko katika hatari dhidi ya tauni-WHO

Kusikiliza /

Tauni na jinsi inavyoenezwa. Picha: WHO

Mkurugenzi wa masuala ya dharura wa shirika la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika Ibrahima Fall amesema hatari ya ugonjwa wa tauni nchini Madagascar bado iko juu ingawa ile ya kimataifa ni ndogo.

Hadi kufikia leo Oktoba 20 kumekuwa na visa 1,553 na 300 kati ya hivyo vimethibitishwa katika maabara huku vifo 94 vikirekodiwa

Bwana Fall amesema hata hivyo idadi ya vifo imedhibitiwa kwa asilimia 10 na wengi wa waathirika wa tauni nchini Madagascar ugonjwa upo katika mfumo wa kichomi.

Majimbo 18 kati ya 22 ya nchi hiyo hata yale ambayo mara nyingi huwa hayakumbwi na mlipuko yameathirika, na miji iliyoathirika zaidi ni mji mkuu Antananarivo na Tamatar.

Mpaka sasa WHO imeshapeleka dawa za vijiua vijasumu au antibiotics nchini humo zinazoweza kutibu wagonjwa wapatao 5000 na dozi zingine za kutosha watu takriban 100, 000 ambao wanaweza kuwa katika hatari .

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930