Kimataifa njaa imeongezeka kwa mara ya kwanza baada ya muongo:FAO

Kusikiliza /

Mtoto muathirika wa maradhi yasababishwayo na utapiamlo nchini Somali ahudumiwa katika makazi yao nchini Somalia. Picha: UNICEF/Rich

Idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani imeongezeka kwa mara ya kwanza baada ya muungo na kufikia watu milioni 815 duniani , limesema leo shirika la chakula na kilimo FAO.

Tangazo hilo limeenda sanjari na wito wa baba mtakatifu Francis wa kuzitaka serikali kushughulikia suala la uhamiaji uliosababishwa na kutokuwepo uhakika wa chakula unaohusishwa na mabadiliko ya tabia nchi na vita.

Wito huo umeungwa mkono na afisa wa FAO mjini Geneva Uswis Bi Carolyn Rodrigues-Birkett, anayeanza kwa kueleza FAO na washirika wake wanachukua hatua gani kushughulikia mizizi ya tatizo hilo hasa vijijini.

(SAUTI YA CAROLYN)

"Ni lazima tuongeze juhudi zetu mara mbili kwa sababu idadi ya watu walio na lishe duni imeongezeka kutoka milioni 777 hadi milioni 815, baada ya tatizo hilo kupungua kwa miaka mingi. Hii inasababishwa na kuongezeka kwa migogoro na athari za mabadiliko ya tabia nchi na mdororo wa uchumi katika baadhi ya sehemu duniani."

 

 

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930