Guterres na Trump wajadili usalama duniani

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Rais wa Marekani Dolnad Trump, kwenye Ikulu ya White House jijini Washington Marekani waliopokutana.(Picha:UM)

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekuwa na mazungumzo na Rais Donald Trump wa Marekani kwenye Ikkulu ya nchi hiyo huko Washington DC ambapo wamejadili mambo kadha wa kadha ikiwemo utendaji thabiti wa Umoja wa mataifa na marekebisho ya chombo hicho.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema katika mazungumzo hayo ya jana Ijumaa, wamezungumzia pia masuala yanayogusa pande mbili hizo ikiwemo mgogoro nchini Myanmar na hali katika rasi ya Korea na hali Mashariki ya Kati na vita dhidi ya ugaidi.

Viongozihao wawili wameazimia kuwa katika miezi ijayo watatute suluhu kwa pamoja katika masuala hayo na changamoto nyingine zinazokabili dunia.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930