Feltman ahitimisha ziara yake nchini Myanmar

Kusikiliza /

Picha kutoka angani ikionyesha maelfu ya waRohingya wakivuka karibu na kijiji cha Anjuman Para kuelekea kambini Kutapalong nchini Bangladesh. Picha: UNHCR/Roger Arnold

Mkuu wa masuala ya kisiasa katika Umoja wa Mataifa Jeffrey Feltman amehitimisha ziara yake ya siku nne nchini Myanmar hii leo kufuatia mwaliko wa serikali. Akiwa Yangon na Nay Pyi Taw, amekutana na wawakilishi wa serikali na maafisa mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka vyama vya umma.

Katika ziara yake ya Oktoba 13 hadi 17, Feltman ameshuhudia kutiwa saini kwa makubaliano ya kihistoria nchini Myanmar ya kusitisha mapigano yakitiwa saini na mashirika husika.

Mazungumzo mengi ya mkuu huyo yalijikita katika hali kwenye jimbo la Rakhine na hatma ya maelfu ya wakimbizi waliokimbilia Bangladesh kufuatia mashambulizi ya Agosti mwaka huu.

Feltman amekumbusha wito wa Katibu Mkuu kwa watoa huduma kuruhusiwa kufikisha misaada eneo la Kaskazini mwa jimbo la Rakhine na kwamba wakimbizi waruhusiwe kurudi kwa hiari nyumbani kwa njia salama na yenye heshima.

Umoja wa Mataifa umeelezea utayari wake wa kushirikiana na Myanmar na Bangladesh katika juhudi zake za kutafuta suluhu kwa ajili ya wakimbizi na watu walioathirika na ghasia na ufurushwaji wa hivi majuzi.

Bwana Feltam atawasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa , wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unahaha kutoa misaada kwa jamii ya Warohingya.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031