FAO yazindua mradi wa dola milioni 98 kukabiliana na ugonjwa wa mnyauko wa migomba

Kusikiliza /

Mkulima anavuna ndizi kutoka shambani mwake. Picha: FAO

FAO yazindua mradi wa dola milioni 98 kukabiliana na ugonjwa mnyauko wa migomba

Shirika la chakula na kilimo duniani FAO limezindua mradi wa kimataifa utakaogharimu dola milioni 98 kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa mnyauko wa migomba, TR4. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Ugonjwa huo wa mnyauko wa migomba unasababishwa na ukungu au kuvu ni tishio kubwa katika uzalishaji wa ndizi kote ulimwenguni na huenda ukasababisha hasara na kuharibu maisha ya watu milioni 400 ambao hutegemea ndizi kama chakula chao au kama njia ya kujipatia kipato.

FAO katika taarifa yake imesema ugonjwa huo ambao husababisha majani ya ndizi kugeuka rangi na kuwa manjano na kisha kuoza na kuanguka unaweza kustahimili kwa miaka mingi kwenye udongo na kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine kupitia pembejeo za kilimo zilizoathiriwa, maji, viatu, vifaa vya kilimo na magari.

Mradi unalenga nchi 67 katika juhudi za kuzuia usambaaji na kuukabili ugonjwa kwa asilimia 60.

Wanasayansi wanakadiria kwamba ifikapo mwaka 2040, ugonjwa huo unaweza kuathiri hekari milioni 1.6 ya mashamba ya migomba ikiwa ni thamani ya dola bilioni kumi kwa mwaka.

Ugonjwa wa mnyauko wa migomba uligundulika mara ya kwanza Kusini Mashariki mwa Asia mnamo 1990 na sasa umepatikana katika maeneo mengine 19 katika nchi 10 ikiwemo Mashariki ya mbali, Asia Kusini na Msumbiji.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930