Doria za mchana zaleta nuru CAR- Kapteni Vianney

Kusikiliza /

Kapteni Vianney, mmoja wa Walinda amani wa UMoja wa Mataifa anapiga doria nchini CAR. Picha: UM/Video capture

Huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSCA umesema uwepo wake umesaidia kuleta utulivu na wananchi wanaweza kushiriki shughuli za maendeleo. Selina Jerobon na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Selina)

Mmoja wa walinda amani kutoka Rwanda, Kapteni Jean-Marie Vianney amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa huko Bangui, mji mkuu wa CAR, mji ambao kwa miaka kadhaa sasa umekuwa unagubikwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

(Sauti ya Kapteni Jean-Marie)

Kapteni Vianney akalinganisha maisha ya awali na sasa ambapo wanafanya doria za mchana.

(Sauti ya Kapteni Jean-Marie)

Wakimbizi wa ndani CAR. Picha: UM

Kesho Jumanne, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ataanza ziara nchini CAR, ambapo pamoja na kutumia siku hiyo kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa, ataonyesha mshikamano na wananchi na walinda amani wa Umoja huo nchini humo.

 

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930