Nyumbani » 23/10/2017 Entries posted on “Oktoba 23rd, 2017”

Wananchi wa CAR wasema wanachotaka wao ni amani tu

Kusikiliza / Minusca

Wakazi wa mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wamesema wanachotaka wao hivi sasa ni amani ili waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida baada ya miaka minne ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Wakazi hao wamesema hayo wakati wakizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa huko Bangui, mji mkuu wa CAR wakati [...]

23/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tutaangalia mitaala yetu ili isaidia kukabili mabadiliko ya tabianchi- Balozi Mulamula

Kusikiliza / Balozi Liberata Mulamula, mkuu wa Idara ya masomo ya Afrika kwenye Chuo Kikuu cha George Washington nchini Marekani akihojiwa na Assumpta Massoi.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/J.Msami)

Mabadiliko ya tabianchi na athari zake kijamii ilikuwa ni moja ya mada wakati wa wiki ya Afrika iliyotamatishwa hivi karibuni kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Mathalani washiriki waliangazia siyo tu mabadiliko hayo yanavyoatishia amani na usalama bali pia mwenendo wa uhamaji hususan wakulima na wafugaji. Miongoni mwa wazungumza wakuu wakati wa wiki hiyo [...]

23/10/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tukizembea tutahitaji miaka 100 kutokomeza ndoa za utotoni- UNICEF

Kusikiliza / Dada mwenye umri wa miaka 15 na mwanae Husseina. Dada alitekwa na Boko Haram na kutunga mimba mikononi mwa kundi hilo.(Picha: UNICEF/UN0118457/)

Bila Ripoti mpya ya shirika la kuhudumia watoto ulimwenguni  UNICEF inasema bila hatua zaidi kuchukuliwa, dunia itahitaji miaka 100 zaidi ili kutokomeza ndoa za utotoni katika maeneo ya Afrika ya kati na magharibi. Ripoti hiyo iitwayo Hatma ya ndoa za utotoni inasema licha ya kuongezeka maradufu kwa kiwango cha kutokomeza ndoa hizo, bado ukuaji mkubwa [...]

23/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Doria zaendelea CAR kusimamia amani

Kusikiliza / Walinda amani wa MINUSCA wapiga doria mjini Bangui.(Picha:UNIFEED/Video Capture)

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA wanaendelea na doria za mchana na usiku hasa kwenye mji mkuu, Bangui. Ghasia zimeendelea kuibuka maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kutishia mchakato wa amani ambao umewezesha kuundwa kwa serikali. Makundi yaliyojihami ambayo yamegawanyika kwa misingi ya [...]

23/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

AMISOM yaendesha mafunzo kukabiliana na utumikishwaji watoto vitani Somalia

Kusikiliza / AMISOM yaendesha mafunzo kwa ajili ya kudhibiti utumikishwaji wa watoto vitani.(Picha:UNIFEED/Video Capture)

Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia, AMISOM umefanya mafunzo kwa ajili ya kuzuia uandikishwaji wa watoto jeshini nchini Somalia Mafunzo hayo ya siku 12 yalifanyika mjini Nairobi, Kenya yakiwaleta pamoja wahusika kutoka mamlaka ya kitaifa ya usalama nchini Somalia na maafisa wa serikali ya shirikisho. Akizungumzia mafunzo hayo, mkuu wa masuala ya ulinzi, haki za [...]

23/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yataka wafuasi wa UDPS DRC waachiwe huru

Kusikiliza / Mkuu wa MONUSCO, Maman Sidikou.(Picha:UM/Kim Haughton)

Ujumbe wa la Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC,  (MONUSCO) umelaani vikali kitendo cha vikosi vya usalama nchini humo kukamata idadi kubwa ya wanachama wa chama cha upinzani cha UDPS, katika mji wa Lubumbashi, jimbo la Haut-Katanga. Wanachama hao wa UDPS walikamatwa jana Jumapili wakati wakihudhuria mkutano kwenye makao makuu ya [...]

23/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 335 zachangishwa kusaidia warohingya huko Bangladesh

Kusikiliza / Wakimbizi wa Rohingya wakielekea Bangladesh. Picha: UNHCR/Roger Arnold

Harakati za kusaidia janga linalokumba waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar zimepatiwa usaidizi hii leo kufuatia mchango wa dola milioni 335 kutoka kwa wahisani. Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi ametaja kiasi hicho cha fedha huko Geneva, Uswisi hii leo mwishoni mwa mkutano wa kuchangisha fedha za [...]

23/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yapongeza usaidizi wa UM nchini humo

Kusikiliza / Mradi wa kilimo cha umwagiliaji ulioanzishwa na UNDP kwa ushirikiano na serikali la Tanzania umesaidia wakulima ma maembe kuongeza mazao na hatimaye riziki. Picha: UNDP

Kuelekea siku ya Umoja wa Mataifa hapo kesho Oktoba 24, serikali ya Tanzania imepongeza mchango mkubwa wa chombo hicho katika kufanikisha maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Assumpta Massoi na taarifa kamili. (Taarifa ya Assumpta) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa nchini Tanzania Dkt. Susan Kolimba ametoa pongezi hizo akihojiwa na [...]

23/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa na AU wafuatilia kwa karibu uchaguzi Kenya

Kusikiliza / 493693Voting_625

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika, AU, Moussa Faki Mahamat, wanaendelea kufuatilia kwa ukaribu mchakato wa uchaguzi nchini Kenya zikiwa zimesalia siku chache kwa mujibu wa ratiba ya marudio ya uchaguzi huo tarehe 26 mwezi huu. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa kufuatia [...]

23/10/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Doria za mchana zaleta nuru CAR- Kapteni Vianney

Kusikiliza / Kapteni Vianney, mmoja wa Walinda amani wa UMoja wa Mataifa anapiga doria nchini CAR. Picha: UM/Video capture

Huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSCA umesema uwepo wake umesaidia kuleta utulivu na wananchi wanaweza kushiriki shughuli za maendeleo. Selina Jerobon na maelezo zaidi. (Taarifa ya Selina) Mmoja wa walinda amani kutoka Rwanda, Kapteni Jean-Marie Vianney amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa [...]

23/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

FAO yaanzisha kampeni ya chanjo kwa mifugo huko Mosul

Kusikiliza / FAO limezindua kampeni ya dharura ya chanjo kwa  wanyama katika eneo la Mosul  jimbo la Ninewa nchini Iraqi. Picha: FAO

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa , FAO limezindua kampeni ya dharura ya chanjo kwa  wanyama katika eneo la Mosul  jimbo la Ninewa nchini Iraqi, ambalo hivi karibuni limekombolewa  kutoka  kwenye kundi la wanamgambo la Kiislamu  (ISIL). Kampeni hiyo inaotekelezwa kwa ushirikiano na Wizara ya Kilimo ya Iraq, inalenga kondoo milioni 1, [...]

23/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031