Nyumbani » 20/10/2017 Entries posted on “Oktoba 20th, 2017”

Ujumbe wa amani kupitia midundo

Kusikiliza / Tunaomba amani na maridhiano. Picha: UM/Video capture

Suala la amani ni ndoto ya wengi katika nchi zinazoshuhudia mizozo huku mara nyingi raia wasio na hatia wakijikuta katika zahma ambayo hawakuitarajia. Mzozo wa Somalia ambao umedumu kwa zaidi ya miongo miwili umesababisha Wasomali wengi kuwa wakimbizi na kuomba hifadhi katika nchi jirani. Kilicho dhahiri ni kwamba raia wamechoka na vita na wangependa uwepo [...]

20/10/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ubia wa Benki ya Dunia na UNHCR kuboresha takwimu za waliofurushwa makwao

Kusikiliza / Takwimu za wakimbizi na wahamiaji ni muhimu. Picha: UNHCR

Benki ya Dunia na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameingia ubia mpya ili kuanzisha kituo cha pamoja cha takwimu kwa ajili ya watu waliolazimika kutawanywa ili kuboresha takwimu za wakimbizi, watu waliotawanywa na jamii zinazowahifadhi. Kituo hicho kilichotangazwa leo katika kuadhimisha siku ya takwimu duniani kitasaidia kutoa taarifa vyema na kuchukua [...]

20/10/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Madagascar bado iko katika hatari dhidi ya tauni-WHO

Kusikiliza / Tauni na jinsi inavyoenezwa. Picha: WHO

Mkurugenzi wa masuala ya dharura wa shirika la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika Ibrahima Fall amesema hatari ya ugonjwa wa tauni nchini Madagascar bado iko juu ingawa ile ya kimataifa ni ndogo. Hadi kufikia leo Oktoba 20 kumekuwa na visa 1,553 na 300 kati ya hivyo vimethibitishwa katika maabara huku vifo 94 vikirekodiwa Bwana [...]

20/10/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki: Shimizi

Kusikiliza / Neno la wiki_SHIMIZI

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno “Shimizi”.  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Nuhu anasema Shimizi ni vazi ya siri ambayo wanawake wanalivalia ndani ya nguo ama wanavaa wakati wanalala. Amesema ni aina fulani ya rinda [...]

20/10/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

G5 ni rasilimali kwa waafrika- Balozi Delattre

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani katika kambi ya IDPs huko Mellia, Tchad. Picha: OCHA / Ivo Brandau

Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Oktoba Balozi François Delattre amesema kikosi cha pamoja dhidi ya ugaidi huko Sahel ni muhimu katika kupambana na ugaidi ambao hautambui mipaka. Balozi Delattre amesema hayo akizungumza na wanahabari huko Bamako, Mali ambako wajumbe wa Baraza la Usalama wameanza ziara ya kutathmini [...]

20/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watoto 12,000 wa Rohingya wakimbilia Bangladesh kila wiki-UNICEF

Kusikiliza / Mohammed Yasin mwenye umri wa miaka 8, ni miongoni mwa watoto waRohingya wanahifadhiwa katika kambi ya wakimbizi huko Bazar ya Cox. Picha: © UNICEF / UN0135698 / Brown

Mazingira duni na magonjwa vinatishia maisha ya watoto zaidi ya 320,000 ambao ni wakimbizi wa Rohingya walioingia Kusini mwa Bangladesh tangu mwishoni mwa mwezi Agosti wakiwemo wengine elfu 10 waliovuka mpaka kutoka Myanmar katika siku chache zilizopita na kila wiki wanaingia 12,000. Hayo ni kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa [...]

20/10/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WHO yachukua hatua kukomesha mlipuko wa homa ya Marburg Uganda

Kusikiliza / Dk Mark Katz anachukua sampuli ya mate kutoka kwa mwanamke mmoja kwa ajili ya kupima virusi vya Malburg. Picha: WHO / Christopher Black

Shirika la Afya ulimwenguni WHO linafanya jitihada za  kutokomeza mlipuko wa  homa ya Marburg huko mashariki mwa Uganda mpakani  mwa Kenya, ugonjwa ambao tayari umesababisha kifo cha mtu moja na mamia kadhaa wameambukizwa. WHO inasema watu hao yawezekana wamepata maambukizi ya virusi hivyo vya homa ya Marburg kwenye kituo cha afya na wakati wa mazishi [...]

20/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miji na sera muhimu katika kutokomeza umasikini na utupaji chakula:FAO

Kusikiliza / Da Silva

Miji inaweza na ni lazima ichukue jukumu muhimu katika kuleta mabadiliko yanayohitajika ili kushughulikia tatizo la njaa, utapia mlo na utupaji wa chakula. Wito huo umetolewa na mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO Jose Graziano da silva hii leo kwa mameya na wawakilishi wa miji zaidi ya 150 duniani waliokusanyika mjini Milan [...]

20/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miundombinu na kilimo ni masuala mtambuka- Kikwete

Kusikiliza / Mahojiano na Jakaya Kikwete2

Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema uchangishaji fedha kwa ajili ya miundombinu na kilimo ni lazime uende pamoja kwa sababu masuala hayo ni mtambuka. Kikwete amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani baada ya kushiriki kikao cha ngazi ya juu cha Wiki ya Afrika ambapo masuala [...]

20/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaonya juu ya madhila ya wototo kambini, Bangaladesh

Kusikiliza / Watoto washtushwa na vita Myanmar. Picha: UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, linasikitishwa na madhila yanaowakumba maelfu ya watoto kambini Kusini mwa Bangladeshi, kufuatia operesheni za kijeshi zilizoshuhudiwa majuma kadhaa yaliopita. Kwa mujibu wa ripoti mpya ya UNICEF, kufuatia operesheni ya usalama katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar zaidi ya nusu ya watu laki sita waliowasili Bangladesh katika [...]

20/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930