Nyumbani » 19/10/2017 Entries posted on “Oktoba 19th, 2017”

Mwendokasi waleta nuru Dar es salaam, Tanzania

Kusikiliza / Maisha ya kawaida barabarani TZ. Picha: UM/Video capture

Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania ni makao makuu ya kibiashara ya taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo kwalo bandari yake pia  hutumiwa na nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa. Mji huu una wastani wa ukuaji wa asilimia 7 kwa mwaka  kwa mujibu takwimu za Benki ya  Dunia [...]

19/10/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Amani ya kudumu Afrika itapatikana kwa kujumuisha wa mashinani- Balozi Mulamula

Kusikiliza / Balozi Liberata Mulamula, Mkuu wa Idara ya masomo ya Afrika kwenye Chuo Kikuu cha George Washington, nchini Marekani akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Wiki ya Afrika kwenye Umoja wa Mataifa ikikaribia ukingoni jijini New York, Marekani, imeelezwa kuwa jitihada za pamoja zisizoengua watu wa mashinani ndio muarobaini wa amani, utulivu na maendeleo barani humo. Balozi Liberata Mulamula, ambaye ni Mkuu wa Idara ya masomo ya Afrika kwenye Chuo Kikuu cha George Washington, nchini Marekani amesema hayo wakati wa [...]

19/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa kimataifa ni nyota ya jaha baada ya shambulio Somalia

Kusikiliza / Naibu mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini  Somalia Vincent Lelei. Picha: UM/Sabir Olad (maktaba)

Raia wa Somalia wameandamana katika mitaa yam ji mkuu Moghadishu kupinga ukatili wa itikadi kali baada ya shambulio kubwa kabisa la bomu kuwahi kutokea nchini humo na kukatili Maisha ya watu zaidi ya 300 mwisho wa wiki iliyopita. Umoja wa Mataifa na washirika wake wamekuwa wakiisaidia serikali kukabiliana na athari na mahitaji makubwa yaliyosababishwa na [...]

19/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yakutana na viongozi kukomesha magongwa yasioambukizwa NCD

Kusikiliza / Wanafunzi katika riadha. Picha: WHO

Viongozi wa Serikali na asasi  za kiraia ulimwenguni wameweka bayana katika mkutano wa kimataifa huko Montevideo, nia yao ya pamoja, kutokomeza magonjwa yasiyo ambukizwa kama vile magonjwa ya moyo na mapafu, saratani na ugonjwa wa kisukari ambayo yanawatesa watu wa kila rika duniani. Roadmap Montevideo ni mkutano wa situ tatu , uliotoa kipaumbele  katika ajenda [...]

19/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afrika tuache kuiga mipango miji isiyojali mazingira yetu- Malonza

Kusikiliza / Mjini Mogadishu barani Afrika. Picha: um/Stuart Price

Huko mjini Kigali nchini Rwanda leo kumefanyika uzinduzi wa ripoti ya Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Africa, ECA, kuhusu ukuaji wa miji na viwanda ikieleza kuwa ukuaji miji ukitumika vyema unaweza kuwa kichocheo cha maendeleo. Selina Jerobon na taarifa kamili. (Taarifa ya Selina) Yaelezwa kuwa ifikapo mwaka 2035, nusu ya wakazi wa [...]

19/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wachanga 7,000 walifariki dunia kila siku mwaka 2016- Ripoti

Kusikiliza / Mtoto mchanga3

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF inaonyesha kuwa mwaka jana watoto 15,000 walifariki dunia kila siku maeneo mbalimbali ulimwenguni kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika. Ikipatiwa jina viwango na mwenendo wa vifo vya watoto ya mwaka 2017, ripoti inasema asilimia 46 kati yao hao ni watoto wachanga ambao walifariki dunia [...]

19/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930