Nyumbani » 17/10/2017 Entries posted on “Oktoba 17th, 2017”

Somalia yapokea vifaa vya tiba ya dharura baada ya shambulio la Jumamiosi: WHO

Kusikiliza / Msaada kutoka mashirika mbalimbali na serikali ya Kenya yawasilishwa nchini Somalia kusaidia waathirika wa mashambulizi ya mabomu. Picha: AMISOM

  Shirika la afya ulimwenguni WHO limewasilisha vifaa vya tiba na huduma ya dharura ikiwemo damu ya kuokoa maisha baada ya shambulio la bomu Jumamosi Oktoba 14 mjini Moghadishu. Takribani watu 300 wameuawa na mamia kujeruhiwa katika shambulio hilo. Vifaa vingine vilivyowasili ni pamoja na vikasha vya kupimia kundi la damu, vifaa vya kuwahudumia waliokumbwa [...]

17/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ushiriki wa baba mtoto anapozaliwa una faida zake

Kusikiliza / Akina mama kwenye hospitali ya rufaa ya Hoima baada ya kijifungua. Picha: UM/John Kibego

Ni kawaida barani Afrika kushuhudia mama anapotaka kujifungua kuwa hospitali peke yake, tofauti na mataifa mengi yaliyoendelea ambapo baba ana nafasi yake katika kushuhudia mwanae akizaliwa. Nchini Uganda mambo yameanza kubadilika na wanaume wametambua umuhimu wa kuwa sanjari na kina mama au wake zao wanapojifungua. Kwa undani zaidi ungana na mwandishi wetu John Kibego katika [...]

17/10/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Feltman ahitimisha ziara yake nchini Myanmar

Kusikiliza / Picha kutoka angani ikionyesha maelfu ya waRohingya wakivuka karibu na kijiji cha Anjuman Para kuelekea kambini Kutapalong nchini Bangladesh.  Picha: UNHCR/Roger Arnold

Mkuu wa masuala ya kisiasa katika Umoja wa Mataifa Jeffrey Feltman amehitimisha ziara yake ya siku nne nchini Myanmar hii leo kufuatia mwaliko wa serikali. Akiwa Yangon na Nay Pyi Taw, amekutana na wawakilishi wa serikali na maafisa mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka vyama vya umma. Katika ziara yake ya Oktoba 13 hadi 17, Feltman ameshuhudia [...]

17/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwelekeo wa kikosi cha kikanda Sudan Kusini unatia matumaini- Lacroix

Kusikiliza / Kikosi cha  ulinzi cha kikanda, RPF kikiwasili huko nchini Sudan Kusini. Picha: UM/Isaac Billy

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limejulishwa kuwa harakati za kupeleka kikosi cha  ulinzi cha kikanda, RPF huko nchini Sudan Kusini, zinaendelea na zinatia matumaini. Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amesema hayo leo alipohutubia Baraza hilo ikiwa ni ripoti ya Katibu Mkuu anayotakiwa awasilishe kila [...]

17/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kiusalama nchini CAR bado si shwari-OCHA

Kusikiliza / Mlinda amani wa Umoja wa Matifa anahakikisha usalama wa raia wanaokimbia makazi yao kufuatia Vurugu nchini CAR. Picha: UM/Martine Perret

Hali ya kiusalama nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR hususan maeneo ya Mashariki na Kusini-Mashariki mwa nchi inaendelea kuzorota na kusababisha idadi ya wakimbizi wa ndani kuongezeka na kufikia laki sita huku wakimbizi waliokuwa wamerejea nyumbani kutoka Cameroon wakilazimika kukimbia tena. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa [...]

17/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi warohingya wapatao 15000 wakwama mpakani mwa Bangladesh

Kusikiliza / Maelfu ya wakimbizi kutoka Rohingya wanavuka mpaka karibu na kijiji cha Anzuman Para, Palong Khali, Bangladesh. Picha: © UNHCR / Roger Arnold

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limeshtushwa na hali isiyoridisha ya kibinadamu kwa  maelfu ya wakimbizi wapya Rohingya waliokwama kwenye mpaka kati ya Bangladesh na Myanmar. Msemaji wa UNHCR huko Geneva, Uswisi, Andrej Mahecic amesema Jumapili usiku pekee waliingia wakimbizi kati ya 10,000 hadi 15,000 wakipitia mpaka wa Anjuman Para wilaya ya [...]

17/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shule ya msingi Zimbabwe yashinda tuzo ya elimu kwa kilimo endelevu

Kusikiliza / Green Oasis_shule ya msingi ya Sihlengeni_Zimbabwe. Picha: © Sihlengeni Primary School

Nchini Zimbabwe shule moja ya msingi imeshinda tuzo ya elimu kwa maendeleo endelevu kutokana na mfumo wake wa kilimo kinachohifadhi mazingira na wakati huo huo kujipatia kipato. Shule hiyo iitwayo Sihlengeni iliyoko wilaya ya Umzingwane, kwenye jimbo kame zaidi la Matebele imeshinda tuzo hiyo iambatanayo na donge nono la dola 50,000 inayotolewa kwa pamoja na shirika [...]

17/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi na wahamiaji waendelea kushikiliwa mateka Libya

Kusikiliza / Wakimbizi na wahamiaji wanalala sakafuni katika kituo cha kizuizini cha Tariq al-Sikka huko Tripoli, Libya. © UNHCR / Iason Foounten

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, linaendelea na jitihada za kusadia mahitaji ya dharura kwa  wakimbizi zaidi ya 14,500 wanaosadikiwa kutekwa na magenge ya wahalifu katika maeneo mbalimbali ya mji wa Sabratha huko Libya . Bwana  Andrej Mahecic ambaye ni msemaji wa UNHCR, akizungumza leo Mjini Geneva amethibitisha kupata taarifa kutoka serikali [...]

17/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Pengo la usawa wa kiuchumi lachangia pengo la usawa wa afya ya uzazi kwa wanawake:UNFPA

Kusikiliza / Uzinduzi wa ripoti mpya huko Maldives. Picha: UNFPA

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA inasema pengo la usawa kwa wanawake katika afya ya uzazi linahusiana na kutokuwepo kwa usawa wa kiuchumi. Flora Nducha na tarifa kamili (TAARIFA YA FLORA) Akifafanua kuhusu ripoti hiyo inayotanabaisha kuhusu hali ya idadi ya watu duniani mwaka 2017 [...]

17/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tushikamane tutokomeze umaskini- Guterres

Kusikiliza / Siku ya kutokomeza umaskini2

Leo ni siku ya kutokomeza umaskini duniani ambapo maudhui ni kujibu wito wa Oktoba 17 mwaka 1992 wa kutokomeza umaskini uliotokana na azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Akizungumzia siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres ametaka mshikamano zaidi ya watu milioni  800 duniani walio katika maisha ya ufukara. Amesema [...]

17/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana katika malengo ya maendeleo Afika ni chachu ya mafanikio:EAC

Kusikiliza / Bwana Charles Njoroge naibu Katibu Mkuu wa shirikisho la kisiasa katika jumuiya ya Afrika Mashariki (ECA) akihojiwa na UN News Kiswahili mjini New york Marekani. Picha na UN News Kiswahili/ Grace Kaneiya

Vijana sio tu taifa la kesho, bali pia ni muhimili wa leo katika kutimiza ajenda ya umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu SDG's na ajenda ya Afrika ya 2063. Hayo ni kwa mujibu wa Bwana Charles Njoroge naibu Katibu Mkuu wa shirikisho la kisiasa katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) anayehudhurika mikutano ya wiki [...]

17/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930