Nyumbani » 16/10/2017 Entries posted on “Oktoba 16th, 2017”

Kimataifa njaa imeongezeka kwa mara ya kwanza baada ya muongo:FAO

Kusikiliza / Mtoto muathirika wa maradhi yasababishwayo na utapiamlo nchini Somali ahudumiwa katika makazi yao nchini Somalia. Picha: UNICEF/Rich

Idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani imeongezeka kwa mara ya kwanza baada ya muungo na kufikia watu milioni 815 duniani , limesema leo shirika la chakula na kilimo FAO. Tangazo hilo limeenda sanjari na wito wa baba mtakatifu Francis wa kuzitaka serikali kushughulikia suala la uhamiaji uliosababishwa na kutokuwepo uhakika wa chakula unaohusishwa na [...]

16/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Bei za vyakula masokoni zimezidi kupanda kila uchao-Burundi

Kusikiliza / Bei ya vyakula yapanda. Picha: FAO

Wakati Ulimwengu ukichagiza uwekezaji zaidi kwenye chakula na  maendeleo ya vijijini  ili kukabiliana na njaa, hata hivyo katika baadhi ya maeneo watu  wameendelea kulalamikia uhaba  mkubwa wa chakula. Nchini Burundi , siku ya chakula duniani imeadhimihswa  wakati bei za  vyakula masokoni zimezidi kupanda kila uchao. Mwandishi wetu wa maziwa makuu  Ramadhani KIBUGA makuu ametembelea soko [...]

16/10/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Nitapaza sauti yangu zaidi baada ya matumaini ya elimu kwa wakimbizi: Muzoon

Kusikiliza / Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Muzoon Almellehan (mbele) akicheza na wasichana wenzake wakimbizi. Picha: UNICEF

Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Muzoon Almellehan amekwenda nchini Jordan ili kukutana na watoto ambao kama yeye walikimbia machafuko Syria na sasa wamejizatiti kwenda shule licha ya mazingira ya changamoto yanayowakabili. Hii ni mara ya kwanza Muzoon  amerejea Jordankatika nchi ambayo aliishi miaka mitatu kama mkimbizi kambini kabla [...]

16/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yasaidia utoaji wa chanjo dhidi ya homa ya manjano Nigeria

Kusikiliza / Kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano kwenye majimbo ya Kwara na Kogi nchini Nigeria. Picha: WHO

Kampeni ya siku 10 ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano inaendelea kwenye majimbo ya Kwara na Kogi nchini Nigeria. Serikali ya Nigeria ilizindua rasmi kampeni hiyo siku ya Ijumaa ikilenga watu zaidi ya Laki Nane na Nusu. Walengwa ni watoto wenye umri wa kuanzia miezi 9 hadi watu wazima wenye umri wa [...]

16/10/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Afrika inasonga mbele, changamoto ni kulinda mafanikioa- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika ufunguzi wa wiki ya Afrika kwenye Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Picha: /Cia Pak

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumza katika ufunguzi wa wiki ya Afrika kwenye Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani akisema bara hilo limepiga hatua kubwa katika siku za hivi karibuni. Ametolea mfano harakati za kupunguza umaskini, kupungua kwa idadi ya vifo vya wajawazito na watoto wachana, kupanua wigo wa vyanzo vya [...]

16/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kenya yatakiwa kuondoa marufuku ya maandamano na kukomesha ukatili wa polisi-Wataalam UM

Kusikiliza / Bendera ya Kenya: Picha: UM/Loey Felipe

Kenya imetakiwa kuondoa marufuku ya maandamano katika miji muhimu, kumaliza ukatili wakati wa maandamno na kukomesha mashambulizi dhidi ya mahakama na vyama vya umma wakati huu wa sintofahamu kuelekea uchaguzi wa rais utakaofanyika Oktoba 26. Wataalam wa Umoja wa Mataifa wamesihi Kenya kuondoa marufuku hiyo wakisema wakati huu wa uhasama wa kisiasa, ni muhimu serikali [...]

16/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO yataka makampuni ya kati na madogo kupewa mikopo

Kusikiliza / Wafanyakazi katika biashara ndogondogo. Picha: ILO

Makampuni yanayotumia mikopo ya benki kama sehemu kubwa ya mitaji yao ya kazi huwa na mishahara ya juu na tija, na hupunguza gharama, lakini makampuni madogo na ya kati (SMEs) mara nyingi hayawawezi kupata au kumudu ufadhili huo, kwa mujibu wa shirika la kazi duniani  ILO. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya ILO iliyotolewa leo [...]

16/10/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uhamiaji uwe wa hiari na si shuruti- Papa Francis

Kusikiliza / Papa Francis akizungumza katika mkutano uliofanyika kwenye makao makuu ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO huko Roma, Italia. Picha: FAO

Leo ikiwa ni siku ya chakula duniani, tukio maalum limefanyika kwenye makao makuu ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO huko Roma, Italia ambapo kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis ametaka serikali duniani kote kushirikiana ili kuhakikisha uhamiaji unakuwa ni salama na jambo la hiari si shinikizo. Taarifa zaidi na Flora Nducha. (Taarifa [...]

16/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wiki ya Afrika yaanza leo New York, ajenda za maendeleo kujadiliwa.

Kusikiliza / Wiki ya Afrika2

Wiki ya Afrika kwenye Umoja wa Mataifa ikiwa imefungua pazia leke hii leo kwa kuwakutanisha  viongozi wa bara hilo New York , Marekani kujadili mafanikio na changamoto za bara hilo, imeelezwa kuwa mipango ya maendeleo itapatiwa kipaumbele katika mijadala. Tarifa kamili na Selina Cherobon (TAARIFA YA SELINA) Akizungumza na idhaa hii katika mahojiano maalum,  Afisa Mwandamizi [...]

16/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Badilisha mwelekeo wa uhamiaji, wekeza vijijini- FAO

Kusikiliza / burundi-kilimo

Leo ni siku ya chakula duniani ambapo Umoja wa Mataifa unataka dunia iwekeze katika uhakika wa chakula na maendeleo ya vijijini ili kubadili mwelekeo wa uhamiaji utokanao na mabadiliko ya tabia nchi. Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO linasema ingawa hivi sasa kuna hama hama kubwa zaidi ya binadamu kuwahi kutokea [...]

16/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930