Nyumbani » 13/10/2017 Entries posted on “Oktoba 13th, 2017”

Myanmar: Kofi Annan awasilisha mapendekezo yake UM

Kusikiliza / Rohingya

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao kuhusu hali ilivyo nchini Myanmar wakati huu ambapo idadi ya waislamu wa kabila la Rohingya waliokimbilia Bangladesh kukwepa mateso imefikia 536,000. Kikao hicho kilichoitishwa na Ufaransa na Uingereza kilikuwa cha faragha na wajumeb walipatiwa ripoti ya kamisheni ya ushauri iliyoundwa kutoa mapendekezo ya jinsi [...]

13/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utegemezi wa bidhaa unadhoofisha uchumi wa nchi zinazoendelea

Kusikiliza / Nchi zinazoendelea zimeshuhudia mapato ya  mauzo kuongezeka. Picha: UNCTAD

Kamati  Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD imetoa ripoti leo mjini Geneva Uswis , ikihusu utegemezi wa nchi tisa zinazoendelea katika mauzo ya nje ya bidhaa kati ya mwaka 2010 na 2015,  na kufanya idadi ya nchi hizo kufikifkia  91, ambayo ni theluthi mbili ya nchi 135 zinazoendelea. Hiyo ni kwa mujibu wa  [...]

13/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Azerbaijan, Misri na Indonesia lindeni watu wa kundi la LGBT-OHCHR

Kusikiliza / Picha:OIT

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema inasikitishwa na wimbi la kukamatwa kwa watu zaidi ya 180 nchini Azerbaijan, Misri na Indonesia ambao wanashukiwa kuwa  watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na waliobadili jinsia au LGBT huku wengi wao wakiripotiwa kuteswa na maafisa wa kiusalama. Kwa mujibu wa ripoti za wataalam maalum [...]

13/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya raia bado wamekwama Raqqa Syria

Kusikiliza / Wanawake, wanaume na watoto wapoteza makazi yao kufuatia mashambulizi ya ISIL. Picha: UM

Mapigano yanayoendelea katika jimbo la Raqqa nchini Syria yamewakwamisha maelfu ya watu ambao wameelezea hali ya taharuki wakati mkakati wa majeshi ya serikali ukiendelea kutaka kuwafurusha wanamgambo wenye itikadi kali wa ISIL. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limezitaka pande kinzani kuruhusu raia waliokwama kwenye mapambano hayo kuondoka, likisema wako katika hatari [...]

13/10/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WFP kutoa msaada wa dharura wa chakula kwa wakimbi wa ndani

Kusikiliza / WFP wasambaza chakula cha msaada nchini Libya. Picha: WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula (WFP) limeanza kutoa msaada wa chakula kwa familia zilizohamishwa na mapigano  ya makundi ya waasi katika mji wa  Sabratha  Magharibi ya Libya. Mkurugenzi wa WFP Lybia bw. Richard Ragan amesema tangu mwishoni mwa Septemba, watu zaidi ya 15,000 wamehamia miji iliyo karibu na mji wa Sabratha. WFP na [...]

13/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sisi ni wao.. nani alijenga kuta?

Kusikiliza / Sisi ni wao1

Zaidi ya watu milioni 63 hivi sasa ni wakimbizi ugenini au wakimbizi ndani ya nchi zao kutokana na vita, mizozo, majanga ya asili na hata yale yanayosababishwa na binadamu. Maisha ya ukimbizini ni ya shida na taabu lakini shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,  UNHCR kupitia usaidizi wa wadau linahaha kuhakikisha kuwa angalau [...]

13/10/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Chile yaingia katika orodha ya kuhifadhi wakimbizi wa Syria:UNHCR

Kusikiliza / Familia kumi na nne kutoka Siria zimekuwa wa kwanza kukaribishwa na kuhifadhiwa rasmi nchini Chile. Picha: UNHCR

Chile imekuwa taifa la karibuni kuwapa makazi wakimbizi wa Syria. Jumla ya wakimbizi 66 wakiwemo watoto 32, wanawake 16 na wanaume 18 waliwasili jana nchini humo kutokea Lebanon kama sehemu ya mpango wa kuwapa wakimbizi makazi unaongozwa na serikali ya Chile kwa msaada wa shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Mjini Santiago [...]

13/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki: Kizazi

Kusikiliza / Neno la wiki_KIZAZI

Wiki hii tunaangazia neno "Kizazi" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Bwana Sigalla anasema neno hili lina maana zaidi ya moja.  Ungana naye akuchambulie… (Sauti ya Bw. Sigalla)

13/10/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Sera thabiti zahitajika kupunguza athari za majanga- UNISDR

Kusikiliza / Uharibifu uliosababishwa na kimbunga Matthew Haiti. Picha: UM

Matetemeko ya ardhi, dhoruba kali na majanga mengine ya asili yataendelea kukumba dunia, umesema Umoja wa Mataifa katika siku ya kupunguza majanga duniani inayoadhimishwa hii leo. Selina Jerobon na taarifa kamili. (Taarifa ya Selina) Nats.. Nchini Nepal, mwanaume mmoja akikwatua kifusi kutoka kwenye mabaki ya nyumba yake.. ni baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha [...]

13/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Familia za warohingya zaanza kuorodheshwa ili kukidhi mahitaji yao:UNHCR

Kusikiliza / ROHINGYAS COUNT

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na serikali ya Bangladesh wameanza hatua ya kwanza ya mchakato wa kuorodhesha familia za takribani wakimbizi wapya 536,000 wa kabila la Rohingya na mahittaji yao. Zoezi hilo litaisaidia serikali ya Bangladesh, UNHCR na mashirika mengine yanayotoa msaada kuwa na uelwa wa ukubwa na mgawanyo wa wakimbizi [...]

13/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuanza kwa kesi dhidi ya Boko Haram Nigeria ni hatua nzuri japo kuna walakini:UM

Kusikiliza / Kesi dhidi ya Boko Haram Nigeria yaanza. Picha: UNODC

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekaribisha uamuzi wa serikali ya Nigeria wa kuanza kesi dhidi ya washukiwa wa kundi la Boko Haram wengi wao wakiwa tayari mahabusu tangu 2009. Hata hivyo ofisi hiyo imesema inatiwa hofu na idadi kubwa ya washukiwa hao ambapo 2300 wanatakiwa kupandishwa kizimbani na kesi zao kusikilizwa [...]

13/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ziko njia sahihi vita dhidi ya VVU-UNAIDS

Kusikiliza / Love Saidi anakusanya antiretrovirals ya mumewe na yake. Picha: WHO/Zakwathu Communications

Bara la Afrika limepiga hatua muhimu katika kukabiliana na virusi vya ukimwi, VVU ikilinganishwa na mabara mengine ukizingatia idadi ya maambukizi mapya, maambukizi ya mtoto kutoka kwa mama na idadi ya watu ambao wamesaka huduma ya matibabu. Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS, Michel Sidibé amesema hayo katika [...]

13/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930