Nyumbani » 12/10/2017 Entries posted on “Oktoba 12th, 2017”

Mafanikio ya MINUSTAH Haiti kuendelezwa- Honoré

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, Sandra Honoré  akiwahutubia waandishi wa habari. Picha: UM/Rick Bajornas

Mafanikio  yaliyopatikana nchini Haiti kutokana na uwepo wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSTAH yataendelea kuimarishwa na kuendelezwa wakati huu ambapo chombo hicho kinahitimisha shughuli zake na kuzikabidhi kwa ujumbe mdogo zaidi, MINUJUSTH. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, Sandra Honoré amesema hayo leo jijini New York, Marekani [...]

12/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres apongeza uchaguzi wa amani Liberia

Kusikiliza / Barabara la Benson katika jiji la Monrovia, Liberia. Picha: Morgana Wingard / UNDP

Wakati kazi ya kuhesabu kura katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge huko Liberia ikiendelea, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amekaribisha jinsi uchaguzi huo umefanyika kwa amani. Kupitia taarifa ya msemaji wake, Bwana Guterres amewapongeza wananchi wa Liberia ambao walijitokeza kwa ari kubwa kupiga kura. Amepongeza juhudi za Tume ya Taifa ya [...]

12/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Niger inapiga hatua katika mfumo wa kutoa tahadhari kuhusu mafuriko

Kusikiliza / Wakazi wa Niger washirikiana kutatua changamoto za mafuriko. Picha: WMO

Kila mwaka mvua nyingi husababisha mafuriko nchini Niger ambapo tangu mwezi Juni mwaka huu watu 56 wamepoteza maisha na wengi zaidi wameathirika. Hiyo ni kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani na usalama wa umma nchini humo sababu kubwa ikielezwa kuwa ni kutokuwepo na mbinu za kutoa tahadhari ya mapema na kukabiliana na hali [...]

12/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Harakati za kuimarisha huduma za afya ya akili nchini Somalia

Kusikiliza / Warsha ya siku tatu ya kuwajenga uwezo maafisa wa afya kutoka katika taasisi za Baidoa nchini Somalia. Picha: UM/Video capture

Afya bora na Ustawi ni lengo namba 3 katika malengo ya mendeleo endevu SDGs, na Umoja wa mataifa unaendelea kusihi mataifa kote ulimwenguni kufanikisha lengo hili na kuhakikisha afya njema kwa wote ifikapo mwaka 2030. Kwa mantiki hiyo, Umoja wa Mataifa ukishirikiana na serikali la Somalia umefanya warsha ya siku tatu mwezi Julai mwaka huu, [...]

12/10/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Vifo vya raia wa Afghanistan kwa mwaka 2017 vyakaribia kuvunja rekodi

Kusikiliza / Kabul, katikati ya maisha ya kisiasa na kijamii ya Afghanistan. Picha UNAMA / Fardin Waezi

Vifo vya raia nchini Afghanistan kwa miezi tisa ya kwanza kwa mwaka huu vinakaribia kuvunja rekodi sababu kubwa ikitajwa kuwa ni mapigano ya ardhini. Ripoti ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa  wa usaidizi nchini Afghanistan, UNAMA imesema kuanzia  Januari mosi hadi Septemba 30 mwaka huu wa 2017, raia 2,640 waliuawa na wengine 5379 walijeruhiwa. Ingawa [...]

12/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF na Serikali ya Bangladesh kusaidia ujenzi wa vyoo kwa warohingya

Kusikiliza / Baadhi ya wakimbizi wa kabila la Rohingya kutoka Myanmar baada ya kuokolewa kwenye boti iliyozama. (Picha:UM/IOM)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ,UNICEF na Wizara ya Usimamizi wa Maafa na Usaidizi ya Serikali ya Bangladesh wamekubaliana kujenga vyoo 10,000 katika kambi ya  warohingya iliyoko wilaya ya Cox ya Bazar ili kuzuia kuzuka kwa magonjwa . Makubaliano hayo yametiwa saini kati ya mwakilishi wa UNICEF Bangladesh Edouard Beigbeder na katibu mkuu [...]

12/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Marekani yajitoa UNESCO, Bokova aeleza masikitiko yake

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova katika taarifa yake. Picha: UNESCO

Marekani imetangaza rasmi kujiondoa kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, hatua ambayo imepokewa kwa masikitiko makubwa na shirika hilo. Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova katika taarifa yake ameeleza masikitiko hayo baada ya kupokea notisi rasmi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson. Mwaka 2011, [...]

12/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNODC yachagiza mchakato wa kesi dhidi ya ugaidi Niger

Kusikiliza / Vijana nchini Niger. Picha: UNODC

Huko nchini Niger, usaidizi kutoka ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC umeongeza kasi ya kushughulikia kesi dhidi ya ugaidi wakati huu ambapo visa vya ugaidi kutoka kwa Boko Haram vinaripotiwa mara kwa mara. UNODC inasema imefanikisha hilo kwa kuajiri wafanyakazi wa kujitolea wanaotembelea watuhumiwa wa ugaidi walioko gerezani [...]

12/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uchumi wa Afrika waendelea kuchanua: Benki ya Dunia

Kusikiliza / Biashara kushamiri Afrika mashariki. Picha: IMF

Benki ya dunia imesema uchumi wa Afika Kusini mwa Jangwa la Sahara unaanza kuchanua tena kwa kasi ya wastani kasi hiyo ikiongozwa na mataifa yenye uchumi mkubwa katika kanda. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA) Katika toleo lake la hivi karibuni la Afrika pulse, Benki ya Dunia inaonyesha ukuaji wa uchumi katika eneo [...]

12/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mpango wazinduliwa kukabili TB ya wanyama inayoambukizwa binadamu

Kusikiliza / zoonotic-tuberculosis-310

Shirika la afya duniani, WHO pamoja na wadau wake wa afya ya wanyama na binadamu leo wanazindua mpango wa kwanza kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu au TB kwa wanyama ambao huambukizwa binadamu. Uzinduzi huo unafanyika nchini Mexico ambapo WHO imesema TB ya wanyama ni ugonjwa uliosahaulika licha ya kwamba binadamu huambukizwa kwa kula bidhaa [...]

12/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930