Nyumbani » 11/10/2017 Entries posted on “Oktoba 11th, 2017”

Kuna uwezekano mkubwa uchaguzi DRC hautafanyika mwaka huu- Sidikou

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko DRC Maman Sidikou.(Picha:UM/Kim Haughton)

Licha ya kwamba hakuna uwezekano wa kwamba uchaguzi wa wabunge na rais utafanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hatua zimepgwa katika kuandikisha wapiga kura. Hiyo ni kwa mujibu wa mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko DRC Maman Sidikou wakati akihutubia Baraza la Usalama [...]

11/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sekta ya mafuta na gesi yatoa fursa ya ajira kwa vijana Uganda-Sehemu ya kwanza

Kusikiliza / Uchimbaji wa mafuta Buliisa Uganda.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/John Kibego)

Wakati vijana wakikabiliwa na ukosefu wa ajira katika nchi nyingi, yaelezwa kuwa ni muhimu vijana wajifunze stadi mbalimbali ili waweze kupata ajira hususan katika sekta isiyo rasmi. Nchini Uganda kufuatia ugunduzi wa mafuta kumekuwa na mahitaji ya waajiriwa katika sekta hiyo. Lakini je kuna uwezekano wa vijana kuwa na stadi zinazohitajika kupata ajira katika sekta [...]

11/10/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Sayansi na teknolojia ikitumiwa vyema itasaidia SDG's:Mohammed

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu wa UM Bi Amina Mohammed akiwa na Robot Sophia kwenye mkutano kuhusu maendeleo ya sayansi ECOSOC Umoja wa Mataifa Marekani. Picha na UM/Manuel Elias

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yana fursa kubwa ya kuchagiza mchakato wa utekelezaji wa maalengo ya maendeleo endelevu au SDG's endapo changamoto zake zitashughulikiwa ipasavyo. Kauli hiyo imetolewa na naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi Amina J. Mohammed kwenye mjadala uliofanyika leo makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhusu fursa na changamoto za [...]

11/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkakati wa kimataifa wa uhamiaji ujikite na watu, uhakikishe usalama na utu kwa wote-Arbour

Kusikiliza / Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhamiaji wa kimataifa Bi Louise. Picha: UM/Ky Chung

Mchakato unaojumuisha serikali mbalimbali ili kupitisha mkakati wa kimataifa kwa ajili ya usalama, utu na mpangilio kwa ajili ya wahamiaji unaendelea leo mjini Geneva Uswisi. Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhamiaji wa kimataifa Bi Louise Arbour amezungumza katika mkutano huo na kusema wakati mchakato mzima wa kupitisha mkakati wa kimataifa [...]

11/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulizi dhidi ya Rohingya ni jama za kuwatokomeza kabisa:UM

Kusikiliza / Wakimbizi wa Rohingya wakimbia makazi yao. Picha: UM

Mashambulizi ya kikatili dhidi ya watu wa kabila la Rohingya yanayoendelea kaskazini mwa jimbo la  Rakhine yamethibititiswa kuwa ni jamaa zilizoandaliwa na waasi ili kuwafukuza Warohingya nje ya mipaka ya  Myanmar na kuwazuia kutorudi tena katika nchini hiyo. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo [...]

11/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Utipwatipwa miongoni mwa watoto na barubaru unaongezeka:WHO

Kusikiliza / Chakula ambacho kinasababisha utipwatipwa. Picha: WHO

Idadi ya watoto na vijana barubaru wa kati ya umri wa miaka 5 hadi 19 walio na tatizo la utipwatipwa imeongezeka kote duniani katika miongo minne iliyopita, na endapo hali ya sasa itaendelea basi watoto na barubaru wengi watakuwa na utipwatipwa wa kupindukia au uzito mdogo kuliko kawaida imeonya leo ripoti mpya ya shirika la [...]

11/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mbinu za kisasa za utabiri wa hali ya hewa kubainishwa Iceland

Kusikiliza / Mbinu za kisasa za utabiri wa hali ya hewa kubainishwa Iceland. Picha: WMO

Shirika la hali ya hewa duniani, WMO litatumia mkutano wa jumuiko la ncha ya kaskazini, Artic Cirle kuonyesha mipango yake ya kuimarisha jinsi ya kutabiri hali ya hewa kama njia mojawapo ya kukabili mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya ncha ya kaskazini na ile ya kusini duniani. Mkutano huo utaanza Ijumaa huko Iceland ambapo [...]

11/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya mtoto wa kike duniani yaadhimishwa leo

Kusikiliza / Mtoto-3

Leo ni siku ya mtoto wa Kike duniani ambapo ujumbe unajikita kwenye kuwezesha mtoto wa kike kabla, wakati na baada ya majanga, matukio mbali mbali yakifanyika ulimwenguni kuangazia siku hii adhimu. Selina Jerobon na taarifa kamili. (Taarifa ya Selina) Nats.. Kibao hicho cha Kate Perry, balozi mwema wa shirika la la Umoja wa Mataifa la [...]

11/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930