Nyumbani » 10/10/2017 Entries posted on “Oktoba 10th, 2017”

Bado kuna changamoto za kiafya kwa wanawake Uganda, ingawa juhudi zinafanyika-Opendi

Kusikiliza / Bi. Sarah Opendi waziri wa afya wa Uganda. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Changamoto za kiafya kwa wanawake nchini Uganda ni nyingi, kuanzia maambukizi ya HIV, kutozingatia uzazi wa mpango na hata kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi ambao wengi ni wanawake na watoto. Hata hivyo waziri wa afya wa nchi hiyo Sarah Opendi amesema serikali ikishirikiana na mashirika ya kimataifa likiwemo la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto [...]

10/10/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukuaji wa kiuchumi duniani unatumainisha

Kusikiliza / Mkurugenzi wa kitengo cha utafiti, IMF Maury Obstfeld. Picha: UM/Video capture

Shirika la fedha duniani, IMF limetangaza leo ukuaji thabiti wa uchumi duniani lakini limesema doa katika ukuaji na wasiwasi kuhusu madeni inamaanisha kwamba watunga sera hawapaswi kubweteka. Akizungumza kuhusu utabiri huo Mkurugenzi wa kitengo cha utafiti Maury Obstfeld amesema IMF imeridhishwa na utabiri ulioimarika kwa asilimia moja katika ripoti yake ya hali ya kiuchumi duniani. [...]

10/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wachache Yemen wananufaika na vita ilhali wananchi wanafukarika- Ahmed

Kusikiliza / Mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Ismael Ould Cheikh Ahmed. Picha: UM /Manuel Elias

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeombwa litumie shinikizo lake la kiuchumi na kisiasa dhidi ya pande kinzani nchini Yemen ili kumaliza machungu yanayokabili wananchi kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo. Mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Ismael Ould Cheikh Ahmed amewasilisha ombi hilo hii leo wakati akihutubia Baraza [...]

10/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yasaidia kuwapa makazi waathirika wa kimbunga Dominica

Kusikiliza / Jumapili 8 Oktoba, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alijiunga na IOM na wadau wengine katika usambazaji wa misaada ya kibinadamu Dominika. Picha:
 (IOM) 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM linasaidia waathirika wa kimbunga Maria kilichopiga visiwa vya Jamhuri ya Dominica kupata makazi. IOM imesema wiki tatu tangu kimbunga Maria, kukumba visiwa vya Carribea wakaazi wanamahitaji ya muhimu ya maji, umeme, na mahitaji mengine. Hatahivyo mahitaji ya dharura ni makazi. Kulingana na ripoti za IOM asilimia 23 [...]

10/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mataifa ridhieni mkataba unaopinga hukumu ya kifo -OHCHR

Kusikiliza / Utekelezaji wa adhabu ya kifo waendelea kupungua. Picha: UM (Cropped)

Leo Oktoba 10 ni siku ya kupinga hukumu ya kifo , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa nchi kote duniani kukomesha ukatili. Selina Jerobon na taarifa kamili. (TAARIFA YA SELINA) Bwana guterres katika ujumbe wake wa siku hii amesisitiza kwamba hukumu ya kifo haina nafasi katika karne 21, kwani ni [...]

10/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinda amani 2 wa Tanzania wauawa DRC, Guterres alaani

Kusikiliza / FIB vikosi maalum vya Tanzania ambao wanahudumu katika sehemu ya MONUSCO, huko Sake, North Kivu (Maktaba). Picha: © MONUSCO / Sylvain

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mauaji ya walinda amani wawili wa Tanzania huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC yaliyotokea kufuatia mashambilizi yaliyofanywa na kikundi cha waasi cha ADF. Katika mashambulizi hayo huko jimbo la Kivu Kaskazini, walinda amani wengine 18 ambao wako kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini [...]

10/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kamisheni yaundwa kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza, NCDs

Kusikiliza / Wanafunzi katika riadha. Picha: WHO

Shirika la afya duniani, WHO limeunda kamisheni ya ngazi ya juu ya kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs. Mgurugenzi Mkuu wa WHO  Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, ametangaza jopo hilo leo wakati wa mkutano wa 64 wa kamati ya shirika hilo la ukanda wa Mediteranea ya Mashariki huko Islamabad, Pakistan. Kamisheni hiyo itaongozwa na Dkt. Sania [...]

10/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Chanjo dhidi ya Kipindupindu yaanza kutolewa Cox Bazar

Kusikiliza / Cholera Vaccinatio in Cox Baza

Huko wilaya ya Cox Bazar nchini Bangladesh, leo imeanza kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu kwa maelfu ya wakimbizi wa Rohingya kutoka Myanmar. Patrick Newman  na maelezo zaidi. (Taarifa ya Patrick) Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la afya WHO na lile la kuhudumia watoto, UNICEF yamesema awamu hii ya kwanza iliyoanza [...]

10/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO kukabili uwindaji haramu , ili kuimarisha uhakika wa chakula

Kusikiliza / Wanyama pori. Picha: FAO

Mradi wa euro milioni 45 unaohusisha wadau mbalimbali umezinduliwa leo na shirika la chakula na kilimo FAO kwa lengo la kusaidia nchi za Afrika, Caribbea na Pacific kudhibiti uwindaji haramu , kulinda mali asili na kuimarisha Maisha ya watu na uhakika wa chakula. Mradi huo wa miaka saba unaofadhiliwa na tume ya Muungano wa Ulaya [...]

10/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wimbi la Warohingya latarajiwa tena Bangladesh:UNHCR

Kusikiliza / Maelfu ya wageni wapya wa wakimbizi wa Rohingya wavuka mpaka karibu na kijiji cha Anzuman Para, Palong Khali, Bangladesh. Picha: © UNHCR / Roger Arnold

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, kwa kushirikiana na serikali ya bangladesh wanajiandaa kupokea umati mkubwa wa wakimbizi wanaokimbia mauaji ya wenyewe kwa wenyewe  yanayolenga kabila la wa Rohingya nchini Myanmar. UNHCR, imethibitisha taarifa kutoka kwa vikosi vya ulinzi vya Bangladesh mpakani kuhusu wimbi la warohingya 11000 waliovuka mpaka jana wakisaka hifadhi [...]

10/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Msongo wa mawazo hugharimu dola trilioni 1 kila mwaka- WHO

Kusikiliza / Mazingira bora pahala pa kazi huchochea afya bora ya akili na hivyo kuongeza tija. (Picha:WHO)

Leo ni siku ya afya ya akili duniani ambapo maudhui ni afya njema ya akili pahala pa kazi ili kuongeza tija. Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema kiwewe na msongo wa mawazo husababisha kupungua kwa tija na hivyo kuleta hasara ya dola trilioni moja kila mwaka duniani. Takwimu za WHO zinaonyesha kwamba zaidi ya watu milioni 300 ulimwenguni [...]

10/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930