Nyumbani » 09/10/2017 Entries posted on “Oktoba 9th, 2017”

Idadi ya wasio na ajira duniani yavuka milioni 200- Ripoti

Kusikiliza / ILO-3

Zaidi ya watu milioni 200 duniani kote hawana ajira ikiwa ni ongezeko kwa asilimia 3.4 kutoka mwaka jana. Shirika la kazi duniani, ILO limetoa takwimu hizo katika ripoti yake iliyochapishwa leo ikisema kuwa chanzo kikubwa ni kudorora kwa biashara za kampuni ndogo na za kati, SME. Ripoti hiyo inasema maeneo yaliyoathirika zaidi ni nchi maskini [...]

09/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalam wa UM akaribisha hatua ya Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya Sudan

Kusikiliza / Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na vikwazo vya kimataifa Idriss Jazairy. Picha: UN Photo/Eskinder Debebe

Mtaalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amepongeza maamuzi ya Marekani ya kuondoa vikwazo dhidi ya Sudan vilivyoanza kutekelezwa miongo miwili iliyopita. Mtaalam maalum huyo kuhusu haki za binadamu na vikwazo vya kimataifa, Idriss Jazairy amesema hatua hiyo ya Marekani ya mnamo Oktoba 6 2017, inafuatia hatua mujarabu zilizochukuliwa na serikali ya Sudan [...]

09/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Jamii yachukua jukumu kulinda vyanzo vya maji Tanga, Tanzania

Kusikiliza / Utekaji maji nchini Tanzania.(Picha:World Bank/Video Capture)

Athari za mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri katika jamii kufuatia matukio mbali mbali yanayoshuhudiwa. Ni kwa mantiki hiyo ambapo baadhi ya jamii ya watu wa muheza mkoa wa Tanga nchini Tanzania wameamua kutunza mazingira kwa sababu hali ya kilimo, ufugaji na maji si nzuri kwao, na katika kulifahamu hilo wameunda umoja wao ujulikanao kwa jina [...]

09/10/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UM washtushwa na kutekwa kwa mfanyakazi wa misaada Darfur:

Kusikiliza / Eneo la Baru Darfur Kaskazini, wafanyakazi wa misaada wa Umoja wa Mataifa wakizungumza na wakimbizi wa ndani. Picha na :UNAMID

Mratibu mkazi na masuala ya kibinadamu wa Umoja wa mataifa nchini Sudan amesema ameshtushwa sana na kitendo cha kutekwa nyara kwa mfanyakazi wa misaada ya kibinadamu kutoka Uswis mnamo Jumamosi ya Oktoba 7 kwenye jjimbo la Darfur Kaskazini. Bi Marta Ruedas ameelezea hofu yake baada ya kutekwa kwa Bi Margaret Schenkel akisema kuwalenga wahudumu ambao [...]

09/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM yatoa msaada wa dharura kwa wahamiaji Sabratah Lybia

Kusikiliza / IOM lybia mpya

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM, limetoa  msaada wa dharura huko Sabratah Libya, kilometa 80 magharibi mwa mji mkuuTripoli kwa wakimbizi 4000  wanoajaribu safari za hatari za kwenda Ulaya kutipitia Bahari ya Mediterania Othman Belbeisi ambaye ni mkuu wa IOM Libya amesema baada ya migogoro ya wenyewe kwa wenyewe nchini  humo kusababisha  kutokua [...]

09/10/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

ICRC yapunguza shughuli zake Afghanistan

Kusikiliza / Moja ya huduma za ICRC. Picha/ICRC

  Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC, imeamua kupunguza shughuli zake nchini Afghanistan  baada ya mfululizo wa mashambulizi  dhidi ya wafanyakazi wake  kaskazini kwa nchi hiyo.  Hii  ni mujibu wa Monica Zanareli ambaye ni mkuu wa ujumbe wa ICRC nchini Afghanistan ambaye amesema tangu mwezi Disemba mwaka 2016 vituo vya ICRC kaskazini mwa Afghanistan, [...]

09/10/2017 | Jamii: Hapa na pale, Jarida | Kusoma Zaidi »

Maeneo ya vijijini yana mchango mkubwa katika maendeleo:FAO

Kusikiliza / Sekta ya kilimo imeelezwa kuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa mujibu wa ripoti ya FAO. Picha na FAO

Mamilioni ya vijana wanaotarajiwa kuingia katika soko la ajira kwenye nchi zinazoendelea katika miongo ijayo, wameaswa kutokimbia umasikini vijijini badala yake wasaidie kuinua sekta ya kilimo. Flora Nducha na tarifa kamili (TAARIFA YA FLORA) Wito huo upo katika ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo FAO iliyochapishwa leo ikisema maeneo ya vijijini yana mchango [...]

09/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinda amani wauawa DRC, MONUSCO yaonya ADF

Kusikiliza / Walinda amani wa UM wapiga doria baada ya mashambulizi na mauaji wa wenzao. Picha; MONUSCO

Walinda amani wawili wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO wameuawa na wengine wamejeruhiwa kufuatia shambulio la hivi karibuni kwenye kitongoji cha Mamundioma, karibu na mji wa Beni, jimbo la Kivu Kaskazini. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC na mkuu [...]

09/10/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Sayansi ya nyuklia ina dhima muhimu katika maendeleo- Amano

Kusikiliza / IAEA-2

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la atomiki, IAEA Yukiya Amano amesisitiza dhima ya shirika lake katika kuimarisha usalama wa nyuklia duniani kwa maendeleo. Amano amesema hayo mjini Roma, Italia hii leo wakati wa mkutano wa 20 wa Edoardo Almadi ukiangazia ushirikiano wa kimataifa katika kuimarisha usalama wa nyuklia na kudhibiti kuenea kwa [...]

09/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Warohingya zaidi wazama baharini wakikimbia ghasia Myanmar

Kusikiliza / Warohingya2

Zahma inazidi kukumba waislamu wa kabila la Rohingya wanaokimbia ghasia nchini mwao Myanmar ambapo katika tukio la karibuni zaidi watu 13 wengi wao wakiwa watoto wamekufa maji baada ya boti yao kuzama. Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM limesema boti waliyokuwa wanatumia ilikuwa ya uvuvi na hali ya hewa wakati wa safari yao [...]

09/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zahma ya lishe yaongezeka kwenye machafuko Mali: UNICEF

Kusikiliza / UNICEF ikiendelea na harakati za kuwatimu maelfu ya watoto walioathirika na utapia mlo nchini Mali. Picha na Luthi:UNICEF Mali.

Mgogoro wa lishe unaochochewa na machafuko yanayoendelea, kutokuwepo usalama na watu kutawanywa nchini Mali unatishia maisha na mustakhbali wa maelfu ya watoto katika taifa hilo la Afrika ya Magharibi limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Takwimu mpya zilizochapisha lleo na kitengo cha ufuatiliaji na tathimini ya misaada kwa mwaka huu 2017 [...]

09/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ndoto yangu ni kuona Botswana ikijikita anga za mbali-Basuti

Kusikiliza / Botswana

Teknolojia ya anga za mbali hususan ile ya kuangalia sayari dunia inaweza kutumika katika kukabliana na magonjwa kwani inawezesha kufuatilia maeneo ambayo yamesambaa maji ambako kuna hatari ya ugonjwa huo kuzuka. Hiyo ni kauli ya Basuti Geti Bolo mwanafunzi wa shahada ya uzamivu katika chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia nchini Botswana baada ya kushiriki [...]

09/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930