Nyumbani » 05/10/2017 Entries posted on “Oktoba 5th, 2017”

Watoto 8000 waliuawa kwenye mizozo mwaka 2016- Ripoti

Watoto waliokuwa wametumikishwa na vikundi vilivyojihami

Zaidi ya watoto 8,000 walioko kwenye maeneo yenye migogoro ya kivita, waliuawa mwaka 2016 pekee. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2016 kuhusu watoto kwenye maeneo yenye migogoro ya kivita, ripoti ambayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekabidhi leo kwa Baraza la Usalama. Miongoni mwa nchi zilizotajwa na ripoti hiyo [...]

05/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utekelezaji wa makubaliano ya amani Mali wasuasua- Annadif

Kusikiliza / secco Mali 2

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani kujadili hali ya usalama na amani nchini Mali. Akihutubia kikao hicho kwa njia ya video Bamako, Mali, Mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA, Mahamat Saleh Annadif amesema hali ya amani na usalama inasuasua kutokana [...]

05/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampeni ya kutokomeza Malaria ishirikishe wananchi- Dkt. Winnie

Kusikiliza / Dkt. Winnie Mpanju Shumbusho, mwenyekiti wa ubia wa kutokomeza Malaria duniani, RBM akihijiwa na Idhaa ya Kiswahili. Picha: UNNews Kiswahili/Assumpta Massoi

Nchi 8 zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, zimechukua hatua za kipekee ili kuondokana na ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030. Nchi hizo kupitia wakuu wa  nchi zao wameazimia kwa kufanya yale ambayo yanaonekana ni magumu. Mathalani kutenga bajeti ili kukidhi mahitaji ya kukabiliana na Malaria. Halikadhalika, kwa kuzingatia kuwa ni nchi jirani, basi wana [...]

05/10/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ustawi wa wasomali unazidi kudorora- Ripoti

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani nchini Sommalia kufuatia ukame uliokithiri. Picha: UM/Stuart Price

Benki ya Dunia hii leo imezindua ripoti ya kina kuhusu hali ya ustawi ya wananchi wa Somalia ikionyesha kuwa hali ya umaskini inakithiri kadri muda unavyosonga. Ripoti hiyo inasema kila sekunde moja ya msomali ni maisha ya dhiki, kaya zikiendelea kukabiliwa na umaskini na uwezo wa kupata ajira ukipungua. Kiwango cha umaskini kinachoainishwa na uwezo [...]

05/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku ya walimu duniani, walimu wanena

Kusikiliza / kisojo-primary-school-kyenjojo-district-uganda-unicef-shehzad-noorani

Ikiwa leo ni siku ya walimu duniani, yenye kuli mbiu ya kufundisha kwa uhuru huwezesha walimu. wanataaluma hao wameeleza maoni yao siku hii ikiadhimishwa ambapo pia wamezungumzia wajibu wa jamii katika kutimiza lengo lao. Selina Jerobon na taarifa kamili. (Taarifa ya Selina) Mashirika ya Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, la kazi [...]

05/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafuta ya mbogamboga yapiga jeki bei ya vyakula-FAO

Kusikiliza / Uvunaji wa zao la alizeti nchini Pakistan.(Picha:FAO/Farooq/Naeem)

Bei ya vyakula imepanda kwa mwezi Septemba kwa mujibu wa orodha ya bei ya vyakula ya shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO. Orodha hiyo inaonyesha ongezeko la asilimia 0.8 ikilinganishwa na mwezi Agosti  na asilimia 4.3 ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka jana. FAO inasema mafuta ya mbogamboga ndio yaliyochangia ongezeko [...]

05/10/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IAEA yaungana na WHO na UNICEF kupambana na utapia mlo

Kusikiliza / Watoto wa shule moja huko Thai wanafurahia chakula cha mchana ambacho kinajumuisha mchele kilichowekwa vitamini A, iron na  zinc kupitia mbinu za za nyuklia  (Picha: IAEA)

Shirika la Umoja wa Mataifa la nguvu za atomic IAEA, shirika la afya ulimwenguni WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wanafanya warsha ya pamoja wiki hii ili kubaini pamoja na mambo mengine jukumu la teknolojia ya nyuklia katika kukabiliana na mzigo mara mbili wa utapia mlo, ambapo lishe duni inaenda [...]

05/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNDP yaongeza nguvu katika kuratibu ujenzi upya wa Dominica

Kusikiliza / Dominica baada ya Kimbunga Maria tarehe 3 Oktoba 2017. Picha: Luca Renda / UNDP

Jopo la watendaji waandamizi kutoka shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP limewasili katika visiwa vya Dominica ili kuratibu jitihada za muda mrefu za ujenzi wa kisiwa hicho baada ya kimbunga Maria kupiga nchi hiyo mwezi uliopita na kusambaratisha miundombinu. Hatua hiyo inafuatia ombi la serikali ya Dominica ambapo UNDP pamoja na [...]

05/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanaume wana nafasi kubwa kufanikisha elimu kwa mtoto wa kike- Malala

Kusikiliza / malala Interview

Mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa Malala Yousafzai amesema wanaume wana nafasi kubwa katika kusaidia watoto wa kike kufanikisha ndoto yao ya kupata elimu. Flora Nducha na ripoti kamili. (Taarifa ya Flora) Malala ambaye ni alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka jana wa 2016, ameiambia Idhaa ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuwa [...]

05/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930