Nyumbani » 04/10/2017 Entries posted on “Oktoba 4th, 2017”

Changamoto za wanafunzi wenye ulemavu na juhudi za kujikwamua

Kusikiliza / Mwanaharakati wa elimu aliye pia mwasisi wa taasisi ya kujenga mustakhbali wa Afrika BAF, na mwanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo, Sauli Mwame(kushoto) akihoji mwanafunzi. Picha: Sauli Mwame_Video capture

Licha ya kuwa na ulemavu wa kutoona, wanafunzi wa shule ya sekondari DCT Mvumi mkoani Dodoma, Tanzania, wameweza kuendelea na masomo huku wakikabiliana na vikwazo na changamoto kadhaa ikiwamo ukosefu wa vitendea kazi. Katika mahojiano na mwanaharakati wa elimu aliye pia mwasisi wa taasisi ya kujenga mustakhbali wa Afrika BAF, na mwanafunzi wa kidato cha [...]

04/10/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushauri na lishe bora kusaidia kukabiliana na utipwatipwa-WHO

Kusikiliza / Mama analisha mtoto wake. Picha: WHO

Takriban watoto milioni 41 walio chini ya umri wa miaka mitano wana uzito wa kupindukia au utipwatipwa kwa mujibu wa ripoti ya 2016 ya shirika la afya ulimwenguni, WHO. WHO imesema hayo wakati wa uzinduzi wa muongozo mpya wa kukabiliana na janga hilo la kimataifa ambalo linaathiri watoto kote ulimwenguni huku likiripotiwa kuongezeka kwa kasi [...]

04/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres kuzuru Caribbea mwishoni mwa wiki kutathimini athari za vimbunga:

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Picha: UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametangaza leo kwamba mwishoni mwa wiki atazuru maeneo yaliyoathirika na vimbunga ya visiwa vya Antigua, Barbuda na Jamhuri ya Dominica ili kutathimini athari zilizosababishwa na vimbunga hivyo na kuona ni jinsi gani Umoja wa Mataifa unaweza kuwasaidia watu wa maeneo hayo kujikwamua baada ya zahma. Akizungumza na [...]

04/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaomba dola milioni 120 kusaidia wakimbizi wa Rohingya

Kusikiliza / IOM wasafirisha msaada wa kibinadau kueleke Bangladesh kwa ajili ya wakimbi WaRohingya. Picha: IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji limetoa ombi la dola takriban milioni 120 kwa ajili ya kuwasilisha misaada ya dharura kwa wakimbizi zaidi ya laki tano wa kabila la Rohingya kutoka Myanmar ambao wamewasili wilaya ya Cox’s Bazar nchini Bangladesh. Kumiminika kwa wakimbizi kwa makumi ya maelfu wa jamii ya warohingya walioanza kukimbia machafuko jimbo la [...]

04/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watoto waliotawanywa na volkano Ambae wanahitaji msaada haraka:UNICEF

Kusikiliza / Tamanu atazama vyombo vya upishi akitafakari maisha yake ya baadaye baada ya kuhamishwa. Picha (maktaba): © UNICEF Vanuatu/2015/Metois

Watu takribani 12,000 wako katika hatari kubwa ya volkano nchini Vanuatu wakiwemo maelfu ya watoto waliohamishwa kutoka  kisiwani Ambae na sasa wanahitaji msaada wa haraka kwenye vituo vya muda vilivyowekwa kwenye visiwa vya jirani. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambapo mwakilishi wake kwenye eneo la Pacifiki [...]

04/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano wa kikanda husongesha biashara kimataifa- Ripoti

Kusikiliza / Mariana Masias katika sekta ya biashara ya mavazi. Picha: ITC

Huko Geneva, Uswisi hii leo, kituo cha biashara cha Umoja wa Mataifa, ITC kimezindua ripoti ya mwaka huu kuhusu mwelekeo wa kampuni ndogo na za kati, SMEs na matumizi ya majukwaa ya kikanda ili kupenya soko la kimataifa. Selina Jerobon na ripoti kamili. (Taarifa ya Selina) ITC ambayo ni kituo tanzi cha kamati ya biashara [...]

04/10/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNCHR yaonya kuhusu ukiukwaji wa haki za wakimbizi

Kusikiliza / UNHCR yaonya kuhusu ukiukwaji wa haki za wakimbizi kama hawa.(Picha:UNHCR)

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limeonya vikali kuhusu  Ukiukwaji wa sheria za kimataifa za wakimbizi, unaofanywa  na askari kushambulia familia zinazokimbia katika hali ya kuokoa maisha yao mipakani.  Onyo hilo lipo katika ripoti ya leo iliowasilishwa  huko Genevia Uswisi na Bw.Volker Türk ambae ni Kamishina mkuu msaidizi  wa UNHCR kuhusu ulinzi wa wakimbizi , kwenye mkutano [...]

04/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM wanakutana kumjengea mwanamke uwezo katika sayansi

Kusikiliza / Rubani wa kwanza Capt. Irene Koki na Vanessa Chilunda na msomaji wa masomo ya Sayansi.(Picha:Idhaa ya Kiswahili)

Wanaanga, wanadiplomasia, watunga sera na wataalam kutoka kote ulimwenguni wanakutana kuanzia leo kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa hapa New York Marekani kwa lengo la kujadili njia za kuongeza idadi ya wanawake na wasichana katika masuala ya sayansi, teknolojia uhandisi na hisabati au kwa kifupi masomo ya STEM hususani katika nchi zinazoendelea. Patrick Newman [...]

04/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya waRohingya huenda ukawa ukiukaji wa haki za binadamu-Wataalam

Kusikiliza / Raia jijini Rackhine, Myanmar. Picha: UNHCR

Kamati ya kuondoa unyanyasaji dhidi ya wanawake CEDAW, na kamati ya haki za mtoto CRC zimetoa wito kwa mamlaka nchini Myanmar kumaliza mara moja ukatili katika jimbo la Rakhine Kaskazini na kufanya uchunguzi wa haraka na kuwashitaki wale wanaotekeleza ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Taarifa ya wataalam wa Umoja wa Mataifa imeelezea masikitiko yao [...]

04/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mradi wa dola milioni 36 kuimarisha jamii nchini Yemen

Kusikiliza / yemen2

Benki ya Dunia na shirika la chakula na kilimo duniani wamezindua mradi wenye thamani ya dola milioni 36 ili kusaidia harakati za kuondokana na njaa nchini Yemen. Fedha hizo ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia, zitawezesha wakazi 630,000 wa maeneo ya vijijini nchini Yemen wakiwemo wanawake kuongeza uzalishaji wa kilimo na [...]

04/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930