Nyumbani » 03/10/2017 Entries posted on “Oktoba 3rd, 2017”

Suluhu ya mzozo dhidi ya warohingya itapatikana Myanmar- OCHA

Kusikiliza / Rohingya-3

Mratibu Mkuu wa masuala ya usaidizi wa kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa, OCHA, Mark Lowcock amesema chanzo cha mzozo dhidi ya wakimbizi wa Rohingya kiko Myanmar na lazima suluhu yake ipatikane nchini humo humo. Bwana Lowcock amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye wilaya ya Cox's Bazar nchini Bangladesh baada ya kujionea hali [...]

03/10/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR na Qatar Charity wakubaliana kuokoa maisha ya wakimbizi

Kusikiliza / Filippo Grandi(kulia), Kamishna Mkuu wa UNHCR na H.E. Sheikh Hamad bin Nasser bin Jassim Al Thani, Mwenyekiti wa Qatar Charity watia saini mkataba wa ushirikiano huko Geneva, Uswisi. Picha: © UNHCR / Jean-Marc Ferré

Shirika la Umoja wa mataifa la  kuhudumia wakimbizi, UNHCR na shirika la misaada la kujitolea la Qatar, Qatar Charity, leo wametia saini mkataba wa ushirikiano unaozingatia kuunga mkono shughuli za ulinzi na msaada wa UNHCR kwa wakimbizi duniani . Utiaji saini huo umefanyika huko Geneva Uswisi kati Kamishna Mkuu wa UNCHR, Filippo Grandi na  mwenyekiti [...]

03/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mapigano mapya yazuka Jonglei, Sudan Kusini- UNMISS

Kusikiliza / UNMISS inaokoa raia waliojeruhiwa katika mashambulizi ya silaha huko Jonglei, Sudan Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS umepokea ripoti za mapigano mapya katika mji wa Waat jimboni Jonglei kati ya jeshi la serikali  SPLA na vikosi vilivyojiengua kutoka jeshi hilo SPLA-IO pamoja na vijana wa kabila la Lou Nuer. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani msemaji wa Katibu mkuu [...]

03/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ubaguzi na unyanyapaa ni kikwazo cha vita dhidi ya ukimwi:UNAIDS

Kusikiliza / Uzinduzi wa ripoti mpya. Picha: UNAIDS

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS limeonya kwamba ubaguzi na unyanyapaa vinazuia watu walioathirika na ukimwi kupata huduma muhimu za afya. Ripoti mpya iliyochapishwa leo na shirika hilo inaonyesha jinsi gani unyanyapaa na ubaguzi ni vikwazo katika kuzuia, kupima, na kupata huduma ya tiba ya HIV na hivyo kuweka maisha [...]

03/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dkt. Kanem wa Panama ateuliwa Mkuu wa UNFPA

Kusikiliza / Kanem

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Dkt. Natalia Kanem wa Panama kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la idadi ya watu la umoja huo, UNFPA. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa uteuzi huo umefanyika baada ya mashauriano kati ya Bwana Guterres na bodi tendaji ya UNFPA. Dkt. Kanem akiwa ni [...]

03/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkakati mpya kuzindiliwa kupunguza vifo vya kipindupindu asilimia 90 -WHO

Kusikiliza / Harakati za kutokomeza kipindupindu Somalia. Picha: WHO

Watu Takriban milioni 3 huugua kipindupindu kila mwaka  huku watu laki moja wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo na kuigharimu dunia zaidi ya dola bilioni mbili. Hiyo ni kwa mujibu wa Dkt. Peter Salama, mkurugenzi mkuu wa kitengo cha afya ya dharura kwenye Shirika la afya ulimwenguni, WHO akizungumza na waandishi wa habari Geneva, Uswisi, [...]

03/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ndoa za utotoni na vitendo vya ukeketwaji kwa wasichana nchini Kenya.

Kusikiliza / Picha: UM/Video capture

Kusini mwa Janga la sahara imebainika kuwa ndoa za utotoni na vitendo vya ukeketwaji kwa wasichana vimeshamiri hivyo kuwakosesha wasichana fursa  ya kupata elimu. Josephine na cecilia ni wasichana kutoka kenya ambao walipambana na hali hii wakiwa wadogo sana.  Kwa undani zaidi, ungana na Patrick Newman kwa makala ifuatayo…..

03/10/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ufadhili zaidi watia nuru ujenzi wa maabara ya kisasa ya IAEA

Kusikiliza / Ukarabati wa maabara ya pili ya IAEA.(Picha:IAEA)

Shirika la nishati ya atomiki duniani, IAEA litaweza kukamilisha maabara yake ya pili ya kusaidia uendelezaji wa sekta ya afya duniani, kufuatia ufadhili wa dola zaidi ya milioni 4 uliopatikana hivi karibuni. Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Yukia Amano amesema mchango huo umetolewa na Ujerumani, Japan, Norway na Marekani na unafuatia ombi la shirika hilo la [...]

03/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ufadhili ukisuasua, mamilioni ya wakimbizi Mashariki ya Kati mashakani

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria katika msimu wa baridi. Picha: UM

Msimu wa baridi kali ukikaribia, mustakhbali wa wakimbizi na wakimbizi wa ndani huko Mashariki ya Kati uko mashakani kutokana na kupungua kwa ufadhili. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasema hali hiyo inatia wasiwasi kwa kuzingatia kuwa ni robo tu ya wakimbizi walioko kwenye ukanda huo ndio wanaweza kupata usaidizi wa kujiandaa [...]

03/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ghasia DRC zafurusha raia 3300 na sasa wanamiminika Zambia

Kusikiliza / Katika Kituo cha Transit cha Nchelenge mkoani Luapula, kaskazini mwa Zambia, wakimbizi wa Kongo wanapokea chakula kilichotolewa na mamlaka za mitaa na UNHCR. Picha: © UNHCR / Pumla Rulashe

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limeshtushwa na ongezeko la ghasia kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, ambazo zimesababisha wimbi la  wakimbizi zaidi ya 3,360   huko kaskazini mwa Zambia tangu Agosti 30.  Taarifa zaidi na Selina Jerobon. (Taarifa ya Selina) Msemaji wa UNHCR huko Geneva, Uswisi Andrej mahecic, amesema [...]

03/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua zachukuliwa kudhibiti kipindupindu miongoni mwa warohingya

Kusikiliza / Zulkhair, mwenye umri wa miaka 27, anabeba mtoto wake wa miezi 10, Mohammad, kambini Kutupalong. Mohammad ni mgonjwa na anahitaji matibabu. Picha: © UNHCR / Paula Bronstein

Zaidi ya wakimbizi 500,000 wa kabila la Rohingya kutoka Myanmar wakiwa wameingia Bangladesh, Umoja wa Mataifa na wadau wake wanahana kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na wakati huo huo kutibu wagonjwa. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema tayari kituo cha kutibu wagonjwa chenye vitanda 20 kimefunguliwa jana jumatatu kwenye kambi [...]

03/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake tunaweza hivyo tuchukue hatua- Inspekta msaidizi Annah

Kusikiliza / Chota2

Mshindi wa tuzo ya kimataifa ya polisi mlinda amani mwanamke, Annah Chota kutoka Zimbabwe amesema mtandao wa wanawake walioanzisha huko Abyei umeleta nuru katikati ya mazingira hatarishi. Chota ambaye ni mkuu wa kitengo cha usawa wa kijinsiana masuala ya watoto kwenye kikosi muda cha ulinzi cha Umoja wa Mataifa huko Abyei, UNISFA, eneo linalogombewa na [...]

03/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930