Nyumbani » 02/10/2017 Entries posted on “Oktoba 2nd, 2017”

UNESCO yamteua Sumaya kuwa mjumbe wa sayansi kwa amani

Kusikiliza / Binti mfalme wa Jordan Sumaya Bint El Hassan ateuliwa na UNESCO kuwa mjumbe wake maalum wa sayansi kwa amani. Picha: UM

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO limemteua binti mfalme wa Jordan Sumaya Bint El Hassan kuwa mjumbe wake maalum wa sayansi kwa amani. Hafla maalum ya kumtangaza imefanyika leo kwenye makao makuu ya UNESCO huko Paris Ufaransa ambapo atashika wadhifa huo kuanzia mwaka huu hadi mwaka 2019. Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bolova amesema [...]

02/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM yahitaji kufanya mengi kuhamasisha kanuni ya kupinga machafuko- Lajčák

Kusikiliza / "Komesha Ukatili," Sanaa iliyochongwa na Karl Fredrik Reutersward ikiwa nje ya Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York Marekani. Picha: UM

Umoja wa Mataifa unahitaji kuchukua hatua zaidi ili kuchagiza kanuni ya kupinga machafuko ambayo inaambatana na maisha ya mwanaharakati wa haki wa India, hayati Mahatma Gandhi. Hiyo ni kauli ya rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Miroslav Lajčák wakati akihutubia hafla la kuadhimisha siku ya kupinga machafuko duniani leo Oktoba pili kwenye makao [...]

02/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yahitaji dola milioni 76.1 Kusaidia watoto wa Rohingya

Kusikiliza / Mama na mtoto wake mchanga, moja kati ya familia mpya za Rohingya ambao waliwasili Banglades mnamo tarehe 5 Septemba 2017. Picha: UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetoa ombi la zaidi ya dola milioni 76 ili kusaidia watoto walioathiriwa na janga linalokumba watu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar ambao sasa wanakimbilia kusini mwa Bangladesh. Ufadhili huo utawezesha kukabiliana na mahitaji ya dharura kwa watoto 720,000 wa Rohingya wanaowasili ikiwemo wale waliowasili awali [...]

02/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Zama za kidijitali lazima zihakikishe manufaa kwa wote: UNCTAD

Kusikiliza / Zama za kidijitali lazima zihakikishe manufaa kwa wote. Picha: UNCTAD

Matumizi ya kidijitali yanaathiri kila upande wa uzalishaji na biashara , kuanzia katika makampuni makubwa hadi kwa wafanyabiashara wadogowadogo, lakini kuna hatari kwamba zama hizi zikaongeza pengo na kutokuwepo usawa wa kiuchumi. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya uchumi ya mwaka 2017 ya kamati ya kimataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD iitwayo “matumizi [...]

02/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM waahidi misaada baada ya kuzuru jimbo la Rhakine

Kusikiliza / Baadhi ya wafanyakazi wa WFP wakielekea Myanmar. Picha: WFP

Umoja wa Mataifa umeishukuru Serikali ya Myanmar kwa mwaliko wa kushiriki katika ziara  ya kukagua maeneo ya kaskazini mwa Rakhine, ziara  iliyoandaliwa na serikali kwa ajili ya jumuiya ya kidiplomasia na ujumbe Umoja wa Mataifa. Wawakilishi watatu wa Umoja wa Mataifa walioshiriki  ziara hiyo ni pamoja na Mratibu wa Makazi wa Umoja wa Mataifa Renata Lok-Dessallien; Mwakilishi wa shirika la [...]

02/10/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Matunda ya mradi wa maji Darfur ni dhahiri kwa wakaazi

Kusikiliza / ?????????????

Eneo la Darfur  nchini Sudan kwa muda mrefu limekabiliwa na ukame wa mara kwa mara ambao husababisha uhasama katika jamii kwa ajili ya kupigania raslimali mbali mbali. Athari za mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri katika eneo hilo ambalo linakabiliana na changamoto mseto ikiwemo mizozo. Ni kwa muktadha huo ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira, [...]

02/10/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ghasia Catalonia zamsumbua Kamishna Zeid

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein akihutubia waandishi wa habari. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein amesema  ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na ghasia zinazoendelea huko Catalonia nchini Hispania kufuatia kura ya wakazi wa jimbo hilo kutaka kujitenga na nchi  hiyo. Kamishna Zeid amenukuliwa akitaka mamlaka nchini humo kuhakikisha uchunguzi wa kina na huru ufanyika ili kubaini wahusika. [...]

02/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Yemen iko katika hatihati ya zahma ya kibinadamu-IOM

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uhamiaji wa Umoja wa Mataifa William Lacy Swing anazungumza na baadhi ya wafanyakazi wa IOM huko Sana'a, Yemeni. Picha: Shirika la Uhamiaji wa Umoja wa Mataifa / Saba Malme 2017

Wakati baa la njaa na mlipuko wa kipindupindu vinatishia kuighubika Yemen , mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM William Lacy swing anayezuru nchi hiyo leo ameutaka uongozi wa taifa hilo kutoa fursa mara moja ya kuwafikia watu na misaada ya kibinadamu ili kuokoa maisha. Amesema ingawa hali inaonekana kuwa shwari [...]

02/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makazi bora kwa kila mtu- UM

Kusikiliza / Ushirikiano katika Maendeleo huko Dhiggaru, Maldives. Picha: UN_Habitat/Veronica Wijaya

Leo ni siku ya makazi duniani ambapo Umoja wa Mataifa unatumia kauli mbiu Sera za makazi:Nyumba kwa gharama nafuu ili kuhakikisha kila mkazi wa dunia ana makazi bora na salama.  Kupitia siku hii Umoja wa Mataifa unatoa changamoto kwa serikali na watu  kutafakari juu ya hali ya usalama mijini na haki ya msingi ya wote [...]

02/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tauni yatikisa Madagascar, WHO yachukua hatua

Kusikiliza / Tauni na jinsi inavyoenezwa. Picha: WHO

Shirika la afya ulimwenguni, WHO linaongeza kasi ya kukabili ugonjwa wa tauni uliotikisa Madagascar ambao umesababisha vifo vya watu 21 na wengine 114 wameambukizwa tangu kisa cha kwanza kiripotiwe mwezi Agosti mwaka huu. Ugonjwa huo wa tauni umeripotiwa katika mji mkuu Antananarivo na miji mingine ya bandari ambapo serikali imethibitisha aliyefariki dunia hivi karibuni ni [...]

02/10/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP kukata mgao wa chakula kwa wakimbizi 420,000 Dadaab na Kakuma nchini Kenya

Kusikiliza / Wakimbizi kambini Dadaab nchini Kenya. Picha: UNHCR/Siegfried Modola

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WPF, litapunguza kwa asilimia 30 mgao wa chakula kwa wakimbizi 420,000 walio kwenye kambi za Daadab na Kakuma nchini Kenya. Selina Jerobon na taarifa kamili (Taarifa ya Selina) Uamuzi huo umetangazwa na mwakilishi mkazi wa shirika hilo nchini Kenya Bi Annalisa Conte , akisema wanakabiliwa na upungufu mkubwa [...]

02/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa haki za binadamu ziarani Guyana kuchunguza ubaguzi

Kusikiliza / Bendera ya Guyana. Picha: UM/Loey Felipe

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wenye asili ya  kiafrika  watatembelea kisiwa cha Guyaha kuanzia tarehe 2 hadi 9 mwezi ujao wa Oktoba ikiwa ni hatua ya kujifunza hali ya haki za binadamu kwa watu wenye asili ya  Afrika waishio katika visiwa hivyo. Msemaji wa msafara huo Sabelo Gumeze amesema wakati wa ziara hiyo watakusanya taarifa [...]

02/10/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

MINUSTAH yazindua sanamu ya amani

Kusikiliza / Sanamu2

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Haiti, MINUSTAH umezindua sanamu ya amani iliyoundwa kwa kutumia masalia ya silaha zilizopokonywa kutoka kwa magenge yaliyokuwa yamejihami. Taarifa kamili na John Kibego. (Taarifa ya Kibego) Uzinduzi huo umefanyika ikiwa imesalia wiki mbili hadi MINUSTAH ihitimishe kazi zake nchini humo ambapo silaha hizo zilipokonywa kutoka kwa [...]

02/10/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930