Migogoro ya wenyewe yazidi kuathiri usalama wa chakula Duniani- FAO

Kusikiliza /

Wakulima kazini licha ya machafuko na mizozo nchini Nigeria. Picha: Sonia Nguyen

Ripoti ya shirika la chakula na kilimo duniani FAO inasema mavuno mazuri huko Amerika ya Kusini na ongezeko la uzalishaji wa kilimo kusini mwa Afrika vinaendela kuboresha usambazaji wa chakula duniani.

Hata hivyo ripoti hiyio ionasema migogoro  ya wenyewe kwa wenyewe na mabadiliko  ya tabianchi  katika maeneo kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na huko Somalia inakwamisha harakati za kupunguza njaa.

Ripoti hiyo imetaja pia vimbunga huko Karibea na mafuriko ya huko Afrika magharibi kuwa vinaweza kuharibu matokeo ya uzalishaji chakula japo bado  kuna matumaini katika uzalishaji wa chakula.

Kwa mujibu wa ripoti ya robo mwaka wa 2017, kati ya nchi 37 zilizohusishwa ,  28 ziko Afrika na zinahitaji msaada wa chakula kutoka nje kutokana na migogoro inayoendelea kuathiri kilimo na usalama wa  chakula.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031