Nyumbani » 25/09/2017 Entries posted on “Septemba 25th, 2017”

Malaysia ilinde utamaduni wake wa stahamala-Mtaalam UM

Kusikiliza / Mtaalam maalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Karima Bennoune. Picha: UM/Amanda Voisard

Mtaalam maalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema Malaysia iko katika hatari ya kupoteza mengi iwapo mamlaka haitachukulia kwa uzito viashiria vya tishio la kupotea kwa desturi ya stahamala nchini humo. Mtaalam maalumu katika haki za utamaduni, Karima Bennoune amesema Malaysia imeibuka katika kipindi cha miaka mingi cha changamoto ya kujenga jamii jumuishi [...]

25/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la UM #UNGA72 watamatishwa

Kusikiliza / Rais wa baraza Kuu Miroslav Lajčák akihutubia Baraza Kuu. Picha: UM/Video capture

Katika hotuba yake ya kufunga mjadala wa wazi wa kikao cha 72 cha Baraza Kuu la Umoja wa mataifa, Rais wa baraza hilo Miroslav Lajčák ametilia mkazo mambo muhimu ambayo baraza lake limejikita kuyatekeleza wakati wa uongozi wake. Mambo hayo ambayo ni mapendekezo yaliyotolewa na nchi wanachama wakati wa mjadala wa wazi ni pamoja na kipaumbele katika [...]

25/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guteress alaani mauaji ya walinda amani wa Mali

Kusikiliza / Maafisa wa UNPOL wa kikosi cha Senegal wanapiga doria katika barabara za Gao, Mali. Picha MINUSMA / Marco Dormino

Mauaji ya walinda amani watatu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA yaliyotokea jumapili yamelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Shambulio hilo lilitokea wakati walinda amani hao walipokuwa kwenye msafara kuelekea eneo la Gao, ambapo  walinda amani wengine watano walijeruhiwa vibaya. Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za [...]

25/09/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Azimio namba 2334 kuhusu Mashariki ya Kati linazidi kusiginwa- Mladenov

Kusikiliza / Ufuatiliaji na ulinzi wa OHCHR katika kijiji cha Khirbet Tana, kusini magharibi mwa Nablus, Mei 2016. © OHCHR

Israel imeendelea kukiuka azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 2334 ambalo pamoja na mambo mengine linataka nchi hiyo kusitisha ujenzi wa makazi mapya kwenye eneo inayokalia la wapalestina. Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani  huko Mashariki ya Kati Nikolay Mladenov amesema hayo leo wakati akihutubia kikao cha [...]

25/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tukihifadhi mazingira leo tunaepuka gharama kubwa Kesho

Kusikiliza / Shida Magunda na Katana Ngala Hinzano katika mahojiano na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Wana mradi wa kuruwitu kutoka Kilifi Mombasa nchini Kenya, wametoa wito wa kuhifadhi mazingira leo ili kuepuka athari zake katika kizazi kijacho. Shida Magunda na Katana Ngala Hinzano wako katika mradi wa kuhifadhi mazingira ya bahari Mombasa kwa kutumia uzalishaji wa samaki. Mradi wao ambao ni wa kwanza nchini Kenya pi umetunukiwa tuzo ya mazingira [...]

25/09/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwezeshaji wa vijana ni ajenda muhimu Comoro

Kusikiliza / Comoro

Ukipata wazazi waliosoma sio budi na wao wahakikishe watoto wao wanasoma na kujiendeleza kimaisha. Patrick Newman na ripoti kamili.  (Taarifa ya Patrick) Hilo ni tamko la Waziri wa Afya, Jinsia na Masuala ya Jamii kutoka Visiwa vya Comoro, Dkt.. Fatma Rashid Mohamed Mbarak ambaye alihojiwa na Idhaa hii kando mwa mjadala wa wazi wa Baraza Kuu [...]

25/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Urusi yabinya haki za binadamu huko Crimea- Ripoti

Kusikiliza / Mfanyakazi wa UNHCR amhoji raia wa Kiukreni aliyehama makazi yake kufuatia vurugu katika eneo lake la Donetsk. Raia huyu amerejea kwake na anasafisha nyumba yake. Picha: © UNHCR / I.Zimova

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeweka bayana vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwenye eneo la Crimea huko Ukraine ambalo linakaliwa na Urusi. Joseph Msami na ripoti kamili. (Taarifa ya Msami) Tangu mwezi Machi mwaka 2014, Urusi ilijitwalia eneo la Crimea nchini Ukraine na kulishikilia hadi hii leo, ambapo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja [...]

25/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yawasaidia watu wapya wanaotawanywa Hawija Iraq

Kusikiliza / Wakimbizi waliotawanywa hivi karibuni kutoka Hawija, Kirkuk na Shirqat, Salah al-Din. Picha: (IOM) 2017

Watu zaidi ya 2400 wametawanywa kwenye mji wa Hawija jimbo la Kirkuk na majimbo ya  Shirqat na salah al-Din, katika operesheni ya kijeshi ya kutaka kuikomboa wilaya ya Hawija. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM watu hao walioanza kutawanywa tangu septemba 21 wengi wao wanakimbilia katika jimbo la Ninewa wakiwemo [...]

25/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Keating akaribisha tathimini ya sheria ya vyombo vya habari Somalia

Kusikiliza / Somalia kufanya marekebisho sheria ya vyombo vya habari Picha: UM/Video capture

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating amesema anafahamu kuhusu kuanzishwa kwa sheria ya hivi karibuni katika bunge la Shirikisho la Somalia ambayo litafanyia marekebisho sheria ya vyombo vya habari ya 2016 nchini humo. Baraza la mawaziri la Rais Mohamed Abdullahi Farmaajo lilipitisha kifungu cha marekebisho ya sheria ya vyombo vya habari [...]

25/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindupindu ni tishio kubwa kwa wajawazito Nigeria: UNFPA

Kusikiliza / Yana Duka ni mmoja wa waathirika 35 wa cholera katika kituo cha afya cha muda mfupi kambini Muna. Alipoteza mimba yake baada ya kuwa mgonjwa. Picha: © UNFPA/Anne Wittenberg

Machafuko yaliyosababishwa na kundi la Boko Haram yamevuruga mfumo wa afya na usafi nchini Nigeria na kutawanya watu milioni 1.7 Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo kwenye majimbo ya Borno, Adamawa na Yobe. Kwamujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA, wengi wa watu hao wanaishi makambini au kuhifadhiwa katika jamii. [...]

25/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031