Nyumbani » 23/09/2017 Entries posted on “Septemba 23rd, 2017”

Warundi mliokimbilia nje karibuni mrejee nyumbani:Nyamitwe:

Kusikiliza / Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Alain Aimé Nyamitwe akihutubia mjadala wa wazi wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani. Picha na UN Web TV.

Hali ya Burundi imetengamaa na ni wakati muafaka kwa raia waliokimbilia nchi jirani na nchi za nje kurejea nyumbani. Wito huo umetolewa leo na waziri wa mambo ya nje wa Burundi Alain Aimé Nyamitwe akihutubia mjadala wa wazi wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa New York Marekani. Nyamitwe amesema pamoja na changamoto zingine za [...]

23/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mshikamano wahitajika kutatua matatizo ya usalama na wakimbizi:Sudan

Kusikiliza / SUDAN GA

Mshikamano wa kimataifa wahitajika ili kutatua changamoto za usalama, suala la wakimbizi na ugaidi. Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya nje wa Sudan Ibrahim Ahmed Abd al-Aziz akihutubia mjadala wa wazi wa baraza kuu hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Bwana Al-Aziz amesema Sudan bado inakabiliwa na changamoto [...]

23/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usaidizi wa kibinadamu Sudan Kusini uende sambamba na maendeleo- Deng

Kusikiliza / Deng2

Sudan Kusini imesema inaendelea kushirikiana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS ili kufanikisha kupelekwa kwa kikosi cha kikanda cha ulinzi wa amani, RPF. Makamu Rais wa Sudan Kusini Taban Deng Dai amesema hayo akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani hii leo. Amesema tayari [...]

23/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchaguzi DRC Hakuna kurudi nyuma na tusiingiliwe- Kabila

Kusikiliza / Kabila

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC itatangaza siku chache zijazo ratiba ya uchaguzi mkuu nchini humo kufuatia mashauriano ya utatu yaliyofanyika baina ya mamlaka ya kitaifa ya ufuatiliaji wa makubaliano ya uchaguzi, serikali na tume ya taifa ya uchaguzi. Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amesema hayo [...]

23/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031