Nyumbani » 22/09/2017 Entries posted on “Septemba 22nd, 2017”

Saidieni AMISOM ili idhibiti vitisho vya usalama- Balozi Amina

Kusikiliza / Amina-1

Kenya imesihi  jumuiya ya kimataifa iongeze zaidi  usaidizi wake kwa ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia, AMISOM ili uweze kushughulikia kwa kina vitisho vya usalama kabla ya kuanza kutekelezwa kwa mpango wa kupunguza idadi ya askari wake. Ombi hilo limo katika hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Amina Mohammed wakati [...]

22/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nilikuwa muathirika wa FGM lakini sasa mimi ni mshindi- Inna Modja

Kusikiliza / Balozi mwema wa UNFPA Inna Modja, ambaye ni mwanamuziki kutoka Mali katika mkutano wa ngazi ya juu wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. Picha:

Ukatili wa aina yeyote dhidi ya wanawake na wasichana hauna nafasi katika dunia hivi sasa kwani unakwamisha mendeleo. Yaelezwa kuwa ili kukabiliana na ukatili huo ni lazima kufahamu sura ambazo unachukua ili kuweza kukabiliana nao. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii ambapo mwanamuziki Inna Modja kutoka Mali anatuma ujumbe kutumia muziki akisema kwamba yeye [...]

22/09/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Utesaji wa washukiwa ni kinyume cha maadili, sheria na hauna ufanisi:Zeid

Kusikiliza / Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'aad al-Hussein. UN/Jean-Marc Ferré

Utesaji wakati wa kuhoji washukiwa wa makossa mbalimbali ni ukiukaji wa sheria za haki za kimataifa, ukiukaji wa maadili na ni mbinu isiyo na ufanisi. Hayo yamesemwa leo na Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'aad al-Hussein katika kikao maalumu kuhusua suala la utesaji kilichofanyika kandoni mwa mjadala wa baraza [...]

22/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WaYemeni hawana uwezo wa kukomesha vita, ni zaidi ya uwezo wao- McGoldrick

Kusikiliza / Mama mkimbizi na mtoto wake akitizama mji mkuu wa Sana'a kutoka juu ya jengo liloharibika. Picha: Giles Clarke/UN OCHA

Hali ya kiusalama nchini Yemen inaendelea kudororo kila uchao wakati mzozo ukiendelea kutokota, mfumo wa afya umesambaratika, uchumi umeporomoka na hali ya kibinadamu inasikitisha. Kauli hiyo ni kwa mujibu wa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Jamie McGoldrick ambaye ameshiriki mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Yemen uliosimamiwa na Shirika la Umoja wa [...]

22/09/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tusaidiane kudhibiti utoroshaji wa fedha kutoka nchi maskini- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia kikao cha kundi la nchi 77 na China kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New YorkPicha: UM/Rick Bajornas

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema uwezo wa nchi kujipatia mapato yake yenyewe ni moja ya mambo ya msingi katika kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu. Amesema hayo wakati wa kikao cha kundi la nchi 77 na China kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani akisema nchi maskini zinahaha [...]

22/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki: Utengamano na Utengano

Kusikiliza / Neno la wiki

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno “Utengamano” na “Utengano”.  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Nuhu anasema utengamano ni hali kuwa kwa pamojan au kushirikiana, na utengano ni kinyume cha utengamano, yaani hali ya kutokuwepo pamoja, [...]

22/09/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yasaka fedha kusaida warohingya nchini Bangladesh

Kusikiliza / Wafanyakazi wa IOM wanatoa huduma za dharura na huduma za afya kwa watu wa Rohingya na wenyeji. Picha: (IOM) 2017

Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM, linasaka zaidi ya dola milioni 26 ili kukidhi mahitaji ya haraka ya wakimbizi wapatao 313,000 wa Rohingya kutoka Myanmar. Wakimbizi hao wanaishi katika maeneo saba ya wilaya ya Cox Bazar mpakani mwa Bangladesh na Myanmar. IOM imesema msaada huu wa dharura wa miezi mitatu unahitajika sana ambapo [...]

22/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNAMID yatoa wito wa utulivu kufuatia machafuko baina ya majeshi ya serikali na wakimbizi wa ndani

Kusikiliza / Sehemu ya kambi ya wakimbizi wa ndani ya Kalma, karibu na Nyala, Kusini mwa Darfur. Picha: UNAMID / Albert González Farran

Mpango wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur nchini Sudan UNAMID, umetoa wito wa kuwepo utulivu na kujizuia na machafuko zaidi katika mapambano yaliyozuka leo kati ya majeshi ya serikali na wakimbizi wa ndani kwenye kambi ya Kalma huko Darfur Kusini. UNAMID inasema inatiwa hofu na machafuko hayo ambayo yameshakatili [...]

22/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yasaidia usafirishaji wa vifaa vya kuandikisha wapiga kura DRC

Kusikiliza / MONUSCO yasaidia usafirishaji wa vifaa vya kuandikisha wapiga kura DRC. Picha: MONUSCO

Huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO umesaidia tume ya taifa ya uchaguzi kusafirisha vifaa vya kuandikisha wapiga kura hadi jimbo la Lomami. Taarifa ya MONUSCO imesema operesheni hiyo imefanikishwa kwa usaidizi pia wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP [...]

22/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Rohingya wakaribia nusu milioni Bangladesh-UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wa Rohingya katika kambi ya Kutupalong ambapo makaazi ya muda yamejengwa kwenye ardhi iliyotengwa na Serikali ya Bangladesh. Picha: © UNHCR / Keane Shum

Wakati idadi ya wakimbizi wa Rohingya wanaoingia Bangladesh kutoka Myanmar ikikaribia nusu milioni, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeongeza juhudi za kufikisha msaada wa kuokoa maisha  kwa maelfu ya watu katika kambi mbili za wakimbizi Kusini Mashariki mwa Bangladesh. Kwa ombi maalumu la serikali ya Bangladesh UNHCR inasema imeharakisha ugawaji wa [...]

22/09/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Jopo la tathimini ya haki za binadamu Sudan Kusini lapata mjumbe mpya

Kusikiliza / Andrew Clapham kutoka taifa la Uingereza. Picha: UM/Jean-Marc Ferré

Rais wa Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa balozi Joaquín Alexander Maza Martelli wa El Salvador, leo ametangaza uteuzi wa Andrew Clapham wa Uingereza kuwa mjumbe mpya wa jopo lililoundwa na baraza la haki za binadamu kufuatilia na kutathimini hali ya haki za binadamu nchini Sudan Kusini. Profesa Clapham atajiunga na Yasmin [...]

22/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Upimaji afya na uzazi wa mpango vitaisaidia kutimiza lengo la afya Uganda

Kusikiliza / Bi. Sarah Opendi waziri wa afya wa Uganda. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Serikali ya Uganda imesema imepiga hatua katika masuala ya afya lakini bado kuna changamoto nyingi . Joseph Msami na tarifa kamili. (TAARIFA YA MSAMI) Kauli hiyo imetolewa na waziri wa afya wa nchi hiyo Bi Sarah Opendi akizungumza na idhaa hii kandoni mwa mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York. Amesema [...]

22/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Amani yahitaji diplomasia na si vitisho- Tanzania

Kusikiliza / Mahiga-2

Tanzania imesema itatumia hotuba yake kwenye mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi kutanabaisha masuala kadhaa ikiwemo umuhimu wa diplomasia katika kutatua mzozo hususan ule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK ikijulikana pia Korea Kaskazini. Waziri wa Tanzania wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika [...]

22/09/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031