Nyumbani » 21/09/2017 Entries posted on “Septemba 21st, 2017”

Hakuna mtoto anayezaliwa akiwa gaidi, vichocheo vitatuliwe – Mohammed

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akizungumza katika mkutano wa mawaziri kuhusu Nigeria na Ziwa Chad. Picha: UM/Video capture

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amesema kwa kipindi cha miaka minane dunia imeshuhudia madhila ya watu wa Cameroon, Chad, Niger na Nigeria katika mikono ya kundi la Boko Haram ambapo ghasia kutokana na kundi hilo zimewaacha watu milioni kumi katika ukanda wa Ziwa Chad wakihitaji msaada wa kibinadamu. Bi. Mohammed [...]

21/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tutapataje amani kama twawekeza kwenye silaha? – Mugabe

Kusikiliza / Mugabe-3

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amehoji ni amani inaweza kufanikiwa duniani ilhali serikali zinawekeza kila uchao kwenye silaha. Ametoa hoja hiyo wakati akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani siku ya Alhamisi akisema ni dhahiri kuwa mtu huvuna kile anachopanda. (Sauti ya Mugabe) "Katika ajabu na kweli, [...]

21/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ufisadi ni sumu ya maendeleo Haiti :Moise

Kusikiliza / Rais Jovenel Moise, wa Haiti akihutubia mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa. Picha: UM/Cia Pak

Haiti ni kisiwa ambacho kinakabiliwa na changamoto nyingi, kuanzia umasikini, ufisadi, masuala ya afya, majanga ya asili na hata mabadiliko ya taibia nchi. Lakini kwa kulitambua hilo imejizatiti kuzikabili  kama taifa na kuhakikisha hakuna atakayesalia nyumba. Hakikisho hilo limetolewa na Rais Jovenel Moise, wa Haiti akihutubia mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa hii [...]

21/09/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ADD International yachukua hatua kufanikisha SDGs

Kusikiliza / Jimmy Innes, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika shirika lisilo la kiserikali la ADD International. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Malengo ya maendeleo endelevu SDGs yamewekewa ukomo wa kutekelezwa ambao ni mwaka 2030. Kwa mantiki hiyo Umoja wa Mataifa unataka kila mtu ashiriki ipasavyo ili asiachwe nyuma. Kwa kusema kila mtu, ina maana bila kujali rangi, jinsia au muonekano wake. Ni kwa mantiki hiyo shirika lisilo la kiserikali la ADD International ambalo linachukua hatua za [...]

21/09/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Swaziland kutokomeza Malaria ifikapo 2020

Kusikiliza / Mfalme Mswati wa III akihutubia kikao cha ngazi ya juu kilichojadili dhima ya uongozi katika kutokomeza Malaria barani Afrika. Picha: UM/Cia Pak

Swaziland imesema iko kwenye mwelekeo wa kutokomeza ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2020, ikiwa ni miongoni mwa nchi 8 kwenye ukanda wa Kusini mwa Afrika zilizo katika hatua za kuondokana na ugonjwa huo hatari. Mfalme Mswati wa III amesema hayo hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani wakati wa kikao [...]

21/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Migogoro ya wenyewe yazidi kuathiri usalama wa chakula Duniani- FAO

Kusikiliza / Wakulima kazini nchini Nigeria. Picha: Sonia Nguyen

Ripoti ya shirika la chakula na kilimo duniani FAO inasema mavuno mazuri huko Amerika ya Kusini na ongezeko la uzalishaji wa kilimo kusini mwa Afrika vinaendela kuboresha usambazaji wa chakula duniani. Hata hivyo ripoti hiyio ionasema migogoro  ya wenyewe kwa wenyewe na mabadiliko  ya tabianchi  katika maeneo kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo [...]

21/09/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Nchi 15 tu ndizo zenye sera tatu muhimu kwa ajili ya malezi ya watoto-UNICEF

Kusikiliza / Siku 1,000 za kwanza zina athari kubwa kwa maisha ya baadaye ya kila mtoto. Tunayo nafasi moja tu ya kuhakikisha matokeo halisi. Picha: UNICEF

Ni nchi 15 tu kote duniani ambazo zimeweka sera za kimsingi kitaifa kuwezesha wazazi,  raslimali na muda unaohitajika kwa ajili ya malezi ya watoto ili kuhakikisha ubongo wao unanakua na afya inayostahili kwa ajili ya ukuaji na mustakhbali wao, imesema ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF. Flora Nducha na tarifa [...]

21/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Warsha ya kujadili imani za kishirikina na haki za binadamu yaanza Geneva

Kusikiliza / Mtoto2

Imani za kishirikina zinakwamisha haki za binadamu na ni vyema kuangazia chanzo chake ili kupata suluhu la kudumu. Hiyo ni kauli ya Naibu Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Kate Gilmore aliyotoa leo huko Geneva, Uswisi wakati akifungua warsha ya siku mbili inayoangazia uhusiano kati ya imani za kishirikina na haki [...]

21/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ajali za barabarani zimefurutu ada lazima zikome:UM

Kusikiliza / Maafisa wa usalama barabarani wanapima kiwango cha mwendo kasi barabarani. Picha: UM/Martine Perret

Kila mwaka watu zaidi ya milioni 1.2 wanauawa katika ajali za barabarni , lakini juhudi zinafanyika ili kupunguza kiwango hicho kwa kiasi kikubwa amesema afisa wa Umoja wa Mataifa. Jean Todt mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu usalama barabarani ameyasema hayo wakati wa kongamano la kimataifa kuhusu kanuni za Magari ambalo limesisitiza kwa nchi kutekeleza [...]

21/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watoto na barubaru milioni 617 hawana ujuzi wa kusoma na hisabati:UNESCO

Kusikiliza / Wanafunzi darazani. Picha: UNICEF

Twakimu mpya kutoka taasisi ya data ya shirika la Umoja wa mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO (UIS) zinaonyesha kwamba watoto na barubaru milioni 617 kote duniani hawafikii kiwango cha chini cha ujuzi katika kusoma na hisabati. Kwa mujibu wa UIS hiyo ni ishara ya mtafaruku katika elimu ambao unaweza kutishia hatua zilizopigwa [...]

21/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

#KilimoniMaendeleo ndio kaulimbiu ya miaka 40 ya FAO Kenya

Kusikiliza / FAO_Kenya_40years 4

Shirika la chakula na kilimo duniani FAO limesema miaka 40 ya shughuli zake nchini Kenya imeleta mafanikio katika sekta mbali mbali ikiwemo umwagiliaji na ufugaji. Mwakilishi wa FAO Kenya Gabriel Rugalema akihojiwa na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo, UNIC wakati wa kilele cha siku hiyo iliyobeba kaulimbiu kilimo na maendeleo. (Sauti [...]

21/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031