Nyumbani » 20/09/2017 Entries posted on “Septemba 20th, 2017”

Bila utashi wa kisiasa ajenda 2030 itaendelea kusuasua- Zuma

Kusikiliza / Rais Jacob Zuma  wa Afrika Kusini akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. (Picha:UNWebTV Video Capture)

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema mfumo wa sasa wa uchumi duniani unazidi kuongeza pengo la utofauti kati ya nchi maskini na zile tajiri. Zuma amesema hayo akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea kwenye makao makuu ya chombo hicho jijini New York, Marekani. Amesema wakati watu wachache wanafurahia [...]

20/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuwekeza katika elimu ndio jawabu kwa dunia na mustakabali bora- Guterres

Kusikiliza / Wanafunzi wainua vitabu ili kuonyesha umuhimu wa elimu yao katika mkutano wa Elimu 2030. Picha: UM/Rick Bajornas

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amesema dunia inakabiliwa na janga la kielimu na bila juhudi hivi sasa, zaidi ya vijana milioni 825 kati ya vijana bilioni 1.6 wataachwa nyuma ifikapo ukomo wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs, mwaka 2030. Akizungumza kwenye kikao kuhusu ufadhili kwa ajili ya elimu kandoni mwa mjadala wa [...]

20/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kusaidia wakimbizi na wahamiaji sio wajibu ni mshikamano:Guterres

Kusikiliza / Guterres_Uganda

Mwaka mmoja tangu kupitishwa kwa kauli moja azimio la New York kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji bado kuna changamoto kubwa katika suala hilo ingawa pia matumaini yapo. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres kwenye mkutano maalumu kuhusu wakimbizi na wahamiaji uliofanyika leo kandoni na kikao cha baraza kuu kinachoendelea [...]

20/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa utekeleze majukumu bila upendeleo- Kagame

Kusikiliza / Rais Paul Kagame wa Rwanda mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Picha: UM/Cia Pak

Mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiingia siku ya pili, Rais Paul Kagame wa Rwanda ametaka chombo hicho kitekeleze majukumu yake bila kuegemea upande wowote. Akihutubia viongozi wa nchi wanachama, Rais Kagame amesema ingawa kila mwaka Umoja wa Mataifa unatumia mabilioni ya fedha kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu kule kwenye [...]

20/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kupitia kampeni ya #He4She viongozi 30 wasongesha usawa wa jinsia

Kusikiliza / Wasichana-Malawi

Kando wa mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, viongozi 30 wameweka bayana kile walichofanya kufanikisha usawa wa kijinsia kwenye nchi zao kupitia wakiwa ni mabingwa wa kampeni ya He4She inayotaka wanaume kusimama kidete kutetea haki za wanawake. Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UNWomen, [...]

20/09/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanaochagiza machafuko Sudan Kusini lazima wawajibishwe

Kusikiliza / Raia wakimbia kusaka hifadhi kufuatia machafuko nchini Sudan Kusini. Picha: UNHCR/Rocco Nuri

Wito umetolewa leo na jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kuhakikisha kwamba wanaochochea machafuko ya Sudan kusini wanawajibishwa lakini pia misaada ya kibinadamu inawafikia walenga. Grace Kaneiya na taarifa kamili. (TAARIFA YA GRACE) Wito huo umetolewa kwenye mkutano maalumu kuhusua hali ya kibinadamu na usaidizi Sudan kusini ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada [...]

20/09/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Dunia yakabiliwa na uhaba wa viua vijasumu- WHO

Kusikiliza / Msaidizi wa maabara anapima damu na kuandika matokeo. Picha: WHO/C. Tephava

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema kuna uhaba mkubwa wa dawa mpya za viua vijasumu au antibayotiki wakati huu ambapo kuna usugu wa dawa za kutibu magonjwa kama vile Kifua Kikuu au TB. Ripoti ya WHO iliyotolewa hii leo imesema hali hiyo imebaini baada ya kuonekana kuwa hata dawa aina ya viua vijasumu ambazo ziko [...]

20/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

FAO na Unilever washikamana kupunguza upotevu wa chakula

Kusikiliza / Ushirikiano unaweza kusaidia kupambana na upotevu wa chakula. Shughuli za kusafisha kwenye Soko la Mboga la Kalimati huko Kathmandu, Nepal. Picha: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani FAO limeingia katika ubia wa mkakati bunifu na kampuni ya Unilever kwa lengo la kuzisaidia nchi katika juhudi zao za kupunguza taka na upotevu wa chakula, na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDG's. Mkurugenzi mkuu wa FAO Jose Graziano da Silver na [...]

20/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hedhi salama ni muarobaini katika kumuokoa msichana- Rebecca

Kusikiliza / Rebecca Gyumi, muasisi na mwenyekiti wa Msichana Initiative. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Vijana ndio tegemeo kubwa hivi sasa la Umoja wa Mataifa katika kusaka suluhu za changamoto zinazokumbwa ulimwengu. Ni kwa kutambua hilo chombo hicho chenye nchi wanachama 193 kinatumia uthabiti wa kundi hilo kuleta mabadiliko mashinani kwa kutambua uwezo wa vijana katika kuelewa na kuabdili maisha yao na ya wenzao. Kwa mantiki hiyo kando ya mjadala [...]

20/09/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kujikita na watu, amani na usalama ndio ajenda yetu Uganda:Museveni

Kusikiliza / Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akihutubia katika mjadala wa baraza kuu. Picha: UM/Cia Pak

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amesema kauli mbiu ya mjadala wa baraza kuu mwaka huu, kujikita na masuala ya watu, amani, usalama na mustakhbali bora kwa wote ni muafaka kwa sasa na ndio ajenda ya Uganda pia ikizingatia kwamba dunia imeghubikwa na machafuko, na majanga ya asili. Akihutubia katika mjadala huo wa wazi kwenye [...]

20/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031