Nyumbani » 18/09/2017 Entries posted on “Septemba 18th, 2017”

Ukatili wa kingono hauna nafasi kwenye UM na dunia yetu:Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (wa pili kutoka kulia) akihutubia mkutano wa ngazi ya juu kuhusu unyanyasaji na ukatili wa kingono. Picha: UM/Evan Schneider

Unyanyasaji na ukatili wa kingono hauna nafasi katika dunia yetu,  ni zahma ya kimataifa na ni lazima utokomezwe. Kwa msisitizo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito huo mbele ya hadhira ya kimataifa hi leo wakati wa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu unyanyasaji na ukatili wa kingono kwenye Umoja wa Mataifa [...]

18/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukame waathiri usafiri wa majini kupitia Ziwa Albert Uganda

Kusikiliza / Wavuvi wa Uganda wakiwa kwenye boti zao ziwani Albert. Picha: UNHCR / M. Sibiloni

Mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri katika masuala mbalimbali ikiwemo huko nchini Uganda ambako mwaka huu nchi hiyo ya Afrika Mashariki ni miongoni mwa nchi ambazo zimekabiliwa na ukame wa muda mrefu. Kando na kusababisha njaa katika nchi za Afrika Mashariki pia moja ya athari ni kupungua kwa kiwango cha maji katika Ziwa Albert tangu Machi kulikokwamisha [...]

18/09/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhakika wa usalama eneo la Wau ni kichocheo cha watu kurejea nyumbani-Shearer

Kusikiliza / Ukarabati katika kambi eneo la Wau nchini Sudan Kusini.(Picha:UNMISS)

Usalama ndio kitu ambacho wakazi wa Wau, Kaskazini Magharibi mwa Sudan Kusini wanahitaji ili kuweza kurejea nyumbani. Hiyo ni kauli ya Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, David Shearer katika mahojiano maalum na radio ya ujumbe wa umoja huo nchini humo UNMISS. Akizungumza baada ya ziara yake katika kambi ya [...]

18/09/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mustapha kutoka Nigeria ndiye mshindi wa tuzo ya Nansen 2017

Kusikiliza / Mustapha

Zannah Mustapha, kutoka Nigeria ndiye mshindi wa tuzo ya mwaka huu ya Nansen inayotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kufuatia harakati zake za kuchagiza haki za watoto kwenye vurugu Kasakazini Mashariki mwa Nigeria kuhakikisha wanapata elimu bora. Mustapha alianzisha shule yake mwaka 2007, huko Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno nchini [...]

18/09/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tabianchi isipodhibitiwa ajenda 2030 itakuwa ni ndoto- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia kikao cha ngazi ya juu kilichofanyika kuhusu mjadala wa mabadiliko ya tabianchi. Picha: UM/Kim Haughton

Ajenda ya maendeleo endelevu, SDGs itasalia ndoto kwa nchi ambazo kila wakati zinakabiliwa na mafuriko na ujenzi wa miundombinu iliyosambaratishwa na majanga hayo ya asili. Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kwenye kikao cha ngazi ya juu kilichofanyika makao makuu ya Umoja huo jijini NewYork, Marekani kikiangazi dhoruba Irma [...]

18/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Safari ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza NCDs ni ndefu-WHO

Kusikiliza / Wanafunzi wa shule ya msingi wakikimbia. Picha: WHO/S. Becker

Serikali ziimarishe juhudi za kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs ili kufikia malengo yaliyowekwa ikiwemo kuzuia vifo vinavyoweza kuzuilika, imesema ripoti mpya ya shirika la afya ulimwenguni, WHO iliyotolewa leo. WHO imesema ni hatua kidogo tu zimepigwa ikiwemo katika magonjwa ya moyo, magonjwa sugu ya kupumua, saratani na kisukari ambayo yanasababisha vifo vingi zaidi na kuua takriban watu [...]

18/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mlinda amani kutoka Tanzania auawa DRC

Kusikiliza / FIB vikosi maalum vya Tanzania ambao wanahudumu katika sehemu ya MONUSCO, huko Sake, North Kivu (Maktaba). Picha: © MONUSCO / Sylvain

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mlinda amani kutoka Tanzania aliyekuwa anahudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO ameuawa huko Mamundioma jimbo la Kivu Kaskazini. Taarifa  ya Umoja wa Mataifa imesema mauti yalimfika mlinda amani huyo ambaye hadi sasa jina lake halijatajwa huku mwenzake mmoja akijeruhiwa, kufuatia mapigano kati ya kikosi [...]

18/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ufadhili ni kiini cha ufanikishaji wa agenda ya 2030: Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika mkutano wa ngazi ya juu wa ufadhili wa ajenda ya 2030 ya SDGs. UM/Ariana Lindquist

Watu wengi duniani wamesalia katika umasikini uliokithiri, na hali isiyokubalika ya kutokuwepo kwa usawa inaendelea. Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika mkutano wa ngazi ya juu wa ufadhili wa ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu unafanyika hapa kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa New york. Guterres [...]

18/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM utajikita na vitendo zaidi ili kupunguza gharama na kuzaa matunda: Guterres

Kusikiliza / President Trump arrives at UNHQ

Umoja wa Mataifa umejizatiti kuhakikisha kwamba unafanya marekebisho yanayohitajika ikiwemo kuepuka ukiritimba na kuzingatia misingi ya katiba ya Umoja huo.  Flora Nducha na tarifa kamili (TAARIFA YA FLORA) Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika mkutano maalumu wa ngazi ya juu kuhusu marekebisho ya Umoja wa Mataifa uliofanyika leo hapa [...]

18/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki ipatikane kwa wahanga wa mauaji huko Kamanyola – Sidikou

Kusikiliza / Wakimbizi wa Burundi wanaandaa chakula juu ya moto ulio wazi katika makazi ya Kamanyola huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Picha: UNICEF / Seck(maktaba)

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC MONUSCO umetaka uchunguzi ufanyike ili kubaini wahusika wa mauaji ya wasaka hifadhi 30 wa Burundi huko jimbo la Kivu Kusini. Joseph Msami na ripoti kamili. (Taarifa ya Msami) Maelfu ya wakimbizi wa Burundi walifika eneo la Kamanyola huko Walungu jimbo la Kivu Kusini [...]

18/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 9.9 zahitajika kukabiliana na kipindupindu Borno Nigeria

Kusikiliza / WFP wanapatia chakula, maji na misaada ingine watu zaidi ya milioni moja ili waweze kukabilia magonjwa ya kipindupindu na utapiamlo. Picha: WFP

Umoja wa Mataifa na washirika wake  wametoa  wito kwa wahisani  wakihiitaji msaasa dola milioni 9.9 kukabiliana na mplipuko wa  kipindipindi   uliozuka hivi  karibuni katika Jimbo la Borno, kaskazini-mashariki mwa Nigeria. Kwa mujibu wa shiriki la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA,  jitihada  za kuzuia na kukabiliana na mlipuko huo zimewekwa bayana [...]

18/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaomba dola zaidi ya milioni 4 kusaidia waathirika wa vimbunga Irma na Jose

Kusikiliza / Wafanyakazi wa IOM wanasambaza misaada ya kibinadamu Fort Liberté, Haiti. Picha: (IOM) 2017

Mapema mwezi huu vimbunga Irma na Jose vilipiga na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa katika visiwa vya Caribbean, ukanda wa Bahamas, Cuba na Marekani. Leo shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limetoa ombi la dola milioni 4.95 kwa jumuiya ya kimataifa ili kuzisaidia haraka jamii  hizo zilizoathirika katika ujenzi mpya. Fedha hizo zitalisaidia [...]

18/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ushirikishaji wananchi DRC wasaidia kupunguza ukatili wa kingono

Kusikiliza / Bango linalosisitiza umuhimu wa kupinga na kutokomeza unyanyasaji na ukatili wa kingono. (Picha:ConductUnmission)

Leo alasiri katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kutafanyika kikao cha ngazi ya juu kuhusu unyanyasaji na ukatili wa kingono, SEA, kwenye mizozo ambapo Umoja wa Mataifa pamoja na mambo mengine unaelezea hatua zinazochukuliwa kukabiliana na vitendo hivyo dhalimu ambako kuna operesheni za ulinzi wa amani. Miongoni mwa maeneo ambako vitendo hivyo vimeripotiwa kufanywa [...]

18/09/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031