Nyumbani » 14/09/2017 Entries posted on “Septemba 14th, 2017”

Sasa tuna 'meno' ya kudhibiti madawa ya kulevya Tanzania- Dkt. Nyandindi

Kusikiliza / Kilimo cha afyuni hushamiri Afghanistan na ni moja ya maeneo yanakotoka madawa hayo. (Picha:UNODC/Zalmai)

Hii leo Umoja wa Mataifa umeadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa ofisi yake inayohusika na udhibiti wa madawa ya kulevya na uhalifu, UNDOC. Ofisi hii kupitia nchi wanachama imechagiza udhibiti wa aina mbalimbali za uhalifu bila kusahau mbinu za kukabiliana na madawa ya kulevya ambayo yanatishia mustakhbali wa wananchi. Tanzania ni moja ya nchi ambazo [...]

14/09/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Muungano kusaidia wanawake na wasichana katika sekta ya teknolojia-UN Women

Kusikiliza / Wasichana ambao walishiriki katika Jukwaa la kimataifa la elimu ya wasichana katika sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) Bangkok, Thailand, Agosti 28, 2017. Picha:UNESCO (Maktaba)

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women na viongozi wa teknolojia wamezindua leo muungano wa ubunifu wa kimataifa kwa ajili ya mabadilko, (GICC) utakaofanya kazi kwa miaka miwili kwa ajili ya kuchagiza hatua kwenye viwanda, kuhakikisha ubunifu na teknolojia vinasaidia wanawake na wasichana. Akizungumzia uzinduzi huo mkuu wa kitengo cha [...]

14/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwelekeo wa biashara duniani ni tofauti na ajenda 2030- UNCTAD

Kusikiliza / UNCTAD imezindua ripoti ya biashara na maendeleo kwa mwaka 2017. Picha: UNCTAD

Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imezindua ripoti ya biashara na maendeleo kwa mwaka 2017 ambayo pamoja na mambo mengine inaonyesha utofauti mkubwa katika ukuaji wa uchumi duniani. Katibu Mkuu wa UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi amenukuliwa akisema kuwa tofauti na malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanayotaka kujenga usawa, uchumi wa dunia [...]

14/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO ni chimbuko la shughuli za umwagiliaji Kenya- Rugalema

Kusikiliza / Gabriel Rugalema, mwakilishi wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO nchini Kenya. Picha: Gabriel Rugalema

Nchini Kenya, shirika la chakula na kilimo duniani, FAO wiki ijayo litaadhimisha miaka 40 tangu kuanza kwa shughuli zake nchini humo. Miradi mbalimbali imetekelezwa ikiwa ni sambamba na ajenda za Umoja wa Mataifa za kuhakikisha kuna maendeleo na ustawi wa wananchi wa nchi wanachama. Je ni nini kimefanyika? Benard Kiziri wa kituo cha habari cha [...]

14/09/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu Maskini wanalipa gharama ya mabadiliko duniani : Mtaalam UM

Kusikiliza / Familia wanaoishi katika makazi duni ya mijini huko Sonagachi, Kolkata, India. Picha. UM / Park ya Kibae

Watu maskini kote ulimwenguni wanakabiliwa na hatari mbali mbali ikiwemo mabadiliko ya tabianchi na majanga ya kiuchumi, lakini dhamira ya kisiasa ya kukabiliana na maswala hayo haipo. Hii ni kwa mujibu wa mtaalamu wa haki wa Umoja wa Mataifa wakati akihutubia Baraza la haki za binadamu kwa mara ya kwanza mjini Geneva Uswis Saad Alfarargi, [...]

14/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watalaam wa UM wapendekeza mazungumzo badala ya vikwazo

Kusikiliza / Mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa  Idriss Jazairy. UN Photo/Eskinder Debebe

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki,  Idriss Jazairy ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuacha kutumikia vikwazo vya moja kwa moja badala yake watumie majadiliano. Bw Jazairy  ameleza kuwa matumaini yake ni kuona jamii ya kimataifa ikitelekeza sheria kulingana na utawala wa sheria,  ambayo hufikiwa kwa njia ya mazungumzo. Ameyasema hayo mbele [...]

14/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taka za sumu kutishia mabilioni kwa maradhi na kifo: UM

Kusikiliza / Mfanyakazi katika sehemu ya taka ya Lagluja, eneo kubwa linalopwa taka za kemikali huko Georgia. Picha: UNDP

Kuwepo katika mazingira yenye taka za kemikali yawezekana ndio chanzo kikubwa cha maradhi na vifo duniani kote na huathiri zaidi watoto na vikundi vya walio wachache amesema leo mtaalamu, wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Selina Jerobon na taarifa kamili. (TAARIFA YA SELINA) Mtaalamu huyo Baskut Tuncak, ambaye ni mwakilishi maalumu kuhusu taka [...]

14/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNODC inaleta nuru kwenye ajenda 2030- Guterres

Kusikiliza / Umoja wa Mataifa ya kudhibiti uhalifu na madawa ya kulevya, UNODC waadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa ofisi hio. Picha: UNODC

Leo ni miaka 20 tangu kuanzishwa kwa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti uhalifu na madawa ya kulevya, UNODC ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema uwepo wa ofisi hiyo unaleta nuru kwenye utekelezaji wa ajenda 2030. Patrick Newman na ripoti kamili. (Taarifa ya Patrick) Katika ujumbe wake wa video kwenye [...]

14/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNFPA yachukua hatua kulinda afya ya uzazi kwa warohingya

Kusikiliza / UNFPA-2

Kufuatia ripoti kwamba miongoni mwa maelfu ya waislamu wa kabila la Rohingya kutoka Myanmar wanaokimbilia Bangladesh ni wajawazito na wanawake wanaonyonyesha, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA limechukua hatua kukidhi mahitaji yao ya afya ya uzazi. UNFPA imesema tayari imepeleka makumi kadhaa ya wakunga wenye mafunzo maalum ya kuhudumia watu walio [...]

14/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031