Nyumbani » 12/09/2017 Entries posted on “Septemba 12th, 2017”

Suluhu na matokeo yanayoonekana vyahitajika kwa ajili ya watu: Lajčák

Kusikiliza / Miroslav Lajčák, Rais mpya wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 72 akihutubia waandishi wa habari. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Rais mpya wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 72, amesema anatarajia kutoa ufumbuzi halisi na matokeo kwa watu wakati wa muhula wake wa kusimamia kazi za wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa. Miroslav Lajčák, mwanadiplomasia mkongwe kutoka Slovakia Ulaya Mashariki  akizungumza na UN News kabla ya kuanza rasmi jukumu la kuongoza kikao [...]

12/09/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kimbunga Irma chaacha rekodi ya uharibifu

Kusikiliza / Baadhi ya uharibifu uliosababishwa na Kimbunga Irma. Picha: WMO

Tahadhari kuhusu kimbunga Irma iliyotolewa na kituo cha kitaifa cha  hali ya hewa cha Marekani, na kituo cha dhoruba cha kitaifa  kuhusu mafuriko, upepo wa mvua  kalina dhoruba, inaonyesha kuwa Irma  imesababisha uharibifu mkubwa katika maeneo mengi huko Florida. Kituo hicho kimesema kimbunga Irma tayari kimesababisha  uharibifu katika visiwa vya Caribean  vilivyoko kwenye  usawa wa bahari kama vile Kuba , uharibifu ulitokana [...]

12/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Miaka 50 ya ukaliwaji Palestina imeleta umasikini na kudumaza maendeleo:UNCTAD

Kusikiliza / Mvulana anatazama jengo lililoporomoshwa na makombora ya vita.  Picha: UNCTAD

Mwaka huu inatimia miaka 50 tangu Israel ianze kulikalia eneo la Wapalestina huko Ukanda wa Gaza na ukingo wa Magaribi ikiwa ni pamoja na eneo la Jerusalem Mashariki . Ukaliwaji huu ni wa muda mrefu zaidi katika historia ya karibuni na kwa Wapalestina ni miongo mitano iliyoghubikwa na kutokuwa na maendeleo, kukandamizwa kwa watu na [...]

12/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yahaha kusaidia warohingya waliokimbia Myanmar

Kusikiliza / Wananchi wa kabila la Rohingya kutoka Myanmar wakiwasili nchini Bangladesh na virago wanavyoona ni muhimu na sasa wanahitaji misaada ya dharura ikiwemo maji safi, chakula, huduma za afya na ulinzi.
(PICHA: IOM/Saikat Biswas )

Idadi ya warohingya ambao wanakimbia mateso na mauaji huko Myanmar ikiongezeka kila uchao, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wao wanaendelea kuhakikisha wanafikisha misaada ya dharura kwa wakimbizi hao ambao wengi wao ni waislamu. Hivi sasa inaelezwa kuwa idadi yao walioingia huko Cox Bazar nchini Bangladesh tangu tarehe 25 mwezi uliopita imefikia zaidi ya [...]

12/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Juddy, mwanamke aliyekataa jinsia na ulemavu kumwacha fukara

Kusikiliza / Juddy Wairimu kutoka Kenya ambaye baada ya kupata ulemavu mumewe alimkimbia. Picha: UN Women/Video capture

Yaelezwa kuwa kuzaliwa mwanamke katika baadhi ya nchi duniani ikiwemo Afrika ni changamoto kubwa, na hali inakuwa mbaya zaidi ukiwa mwanamke tena una ulemavu.  Shuhuda wa kauli hiyo ni Juddy Wairimu kutoka Kenya ambaye baada ya kupata ulemavu mumewe alimkimbia. Hata hivyo hakukata tamaa na alijitambua na sasa ni shuhuda wa harakati za Umoja wa [...]

12/09/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Jukwaa kuhusu utatuzi wa changamoto za tabianchi lazinduliwa Addis Ababa

Kusikiliza / Mafuriko yanayochangiwa na mabadiliko ya tabianchi. Picha: WMO

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo WMO, UNDP, AFD, WFP kwa kushirikiana na banki ya maendeleo Africa  na Banki ya Dunia leo hii mjini Addis Ababa wamezidua jukwa la kwanza   la AMCOMET Africa Hydromet. Jukwa hilo la aina yake  limewajumuisha  wajumbe 500 toka serikalini, sekta binafsi na asasi za kiraia za  mataifa  mbalimbali Africa [...]

12/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Takriban robo tatu ya watoto na vijana wanakabiliwa na ukatili na usafirishaji haramu :IOM, UNICEF

Kusikiliza / Kikundi cha watu katika kituo cha kizuizini kinachosimamia wakimbizi na wahamiaji huko Tripoli, Mei 2017. Picha: © UNHCR / Iason Foounten

Takriban robo tatu ya watoto na vijana wanakabiliwa na ukatili, unyanyasaji na usafirishaji haramu wa binadamu katika safari za wahamiaji kupitia bahari ya Mediterranea, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa, la uhamiaji IOM na la kuhudumia watoto UNICEF . Flora Nducha na taarifa kamili… (TAARIFA YA FLORA) Ripoti hiyo "safari [...]

12/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shehena ya usaidizi kwa warohingya yawasili Bangladesh

Wakimbizi wa Rohingya huko Cox's Bazar wapata misaada ya kibinadamu ikiwemo ya afya. . Picha: Azam Sheikh Ali Haider / UN Migration Agency (IOM) 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limefikisha shehena ya kwanza ya misaada ya dharura kwa warohingya wa Myanmar waliosaka hifadhi nchini Bangladesh. Ndege mbili zilizosheheni zaidi ya tani 91 za misaada hiyo ikiwemo vifaa vya malazi zimewasili mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka, moja ikiwa imekodishwa na UNHCR ilhali nyingine imekodishwa na falme [...]

12/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres apongeza Baraza la Usalama kwa azimio dhidi ya DPRK

Kusikiliza / Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Picha: UN Photo/Mark Garten

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha hatua ya Baraza laUsalama la umoja huo la kupitisha kwa kauli moja azimio dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK. Azimio hilo lililoopitishwa Jumatatu pamoja na mambo mengine linapanua wigo wa vikwazo dhidi ya nchi hiyo kufuatia kitendo chake cha kufanya jaribio la [...]

12/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukimbizi wakosesha mamilioni ya watoto haki ya elimu- UNHCR

Kusikiliza / Deputy headteacher of Yangani progressive primary school, Mr Patric Abale, teaches pupils

Zaidi ya wakimbizi watoto milioni 3.5 wenye umri kati ya miaka mitano hadi 17 hawakuwa na fursa ya kwenda shule muhula uliopita wa masomo. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR iliyotolewa leo ikipatiwa jina "Walioachwa nyuma: Elimu kwa wakimbizi kwenye mkwamo." Kamishna Mkuu wa wakimbizi [...]

12/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031