Nyumbani » 11/09/2017 Entries posted on “Septemba 11th, 2017”

Kikao cha 71 cha baraza Kuu kimefunga pazia:

Kusikiliza / Katibu Mkuu Antonio Guterres akizungumza kwenye ufungaji wa kikao cha 71 cha baraza kuu. Picha na UM

Kikao cha 71 cha baraza kuu la Umoja wa Mataiofa leo kimefunga pazia kwenye makao makuu ya Umoja huo hapa New york Marekani. Akizungumza katika mkutano wa ufungaji wa kikao hicho Katibu Mkuu wau moja wa Mataifa Antonio Guterres amemshukuru Rais wa kikao cha 71 Peter Thompson kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa mwaka mzima   [...]

11/09/2017 | Jamii: Habari za wiki, Kikao cha 71 cha Baraza Kuu | Kusoma Zaidi »

Uvuvi haramu na juhudi za kuukabili Tanzania.

Kusikiliza / Boti za wavuvi kandoni mwa bahari. Picha: FAO

Lengo namba 14 la malengo ya maendeleo endelevu SDGs, linapigia upatu matumizi ya bahari, mito na maji na matumizi ya rasilimali hizo, kwa ujumla kwa maendeleo endelevu. Miongoni mwa mambo yanayokwaza maendeleo endelevu ya bahari ni uvuvi haramu unaotajwa kukwaza uzalishaji mkamilifu wenye tija kwa jamii na huchangia uharibifu wa mazingira baharini na kuhatarisha viumbe [...]

11/09/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu mpya wa OCHA ajionea madhila ya wakimbizi wa ndani Niger

Kusikiliza / Bw. Mark Lowcock ametembelea makazi ya wakimbizi wa dani huko N'Gagam kusini mashari mwa Niger. Picha: OCHA

Mkuu mpya wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA Mark Lowcock yuko ziarani kwenye maeneo ya bonde la ziwa Chad ili kupazia sauti madhila yanayokumba zaidi ya watu milioni 17 kwenye eneo hilo. Mathalani tayari ametembelea kambi ya wakimbizi wa ndani ya N'Gagam kusini-mashariki mwa Niger ambako amekutana na wanawake [...]

11/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wanakabiliwa na hatari kubwa ya kutoweshwa: UM

Kusikiliza /

Kuna uhusiano kati  ya watu kutoweshwa na uhamiaji, lakini serikali na jumuiya ya kimataifa hawatilii maanani suala hili, limeonya leo kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa katika ripoti yao mpya waliyoiwasilisha kwenye baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi. Kikosi kazi kinachohusika na watu kutoweshwa kwa lazima au pasi [...]

11/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Idadi ya vifo na uharibifu wa tetemeko la ardhi Mexico umenishtua:Guterres

Kusikiliza / Mnamo tarehe 9 Septemba 2017 huko Oaxaca, Mexiko, vijana kutoka San Blas Atempa walijitolea kusaidia kusafisha mitaa ya San Mateo del Mar walioathirika na tetemeko la ardhi. Picha: © UNICEF / UN0120076 / Solís

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na idadi ya vifo na uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi la mwishoni mwa juma kwenye majimbo ya Oaxaca, Chiapas na Tanasco nchini Mexico na kusema Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada endapo utahitajika. Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake Guterres ametuma salamu za [...]

11/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yasaka fedha kusaida warohingya nchini Bangladesh

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Myanmar wapanga foleni kupokea misaada ya kibinadamu nchini  Bangladesh. Picha: IOM

Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM, linasaka zaidi ya dola milioni 26 ili kukidhi mahitaji ya haraka ya wakimbizi wapatao 313,000 wa Rohingya kutoka Myanmar. Wakimbizi hao wanaishi katika maeneo saba ya wilaya ya Cox Bazar mpakani mwa Bangladesh na Myanmar. IOM imesema msaada huu wa dharura wa miezi mitatu unahitajika sana ambapo [...]

11/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kinachoendelea Myanmar ni mauaji ya kikabila- Zeid

Kusikiliza / Raia Rakhine nchini Myanmar wahofia maisha yao kwa ukatili unaoendelea nchini humo. Picha: ocha/P. Peron

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein amesema kinachoendelea Myanmar hivi sasa dhidi ya waislamu wa kabila la Rohingya ni sawa na mauaji ya kikabila. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Bwana Zeid amesema hayo akifungua kikao cha 36 cha Baraza la Haki za binadamu la [...]

11/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtoto 1 kati ya 5 wanahitaji msaada Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini:UNICEF

Kusikiliza / Mtoto mvulana mwenye ugonjwa wa upuni anapokea matibabu katika Hospitali ya Al-Jumhouri, Sa'ada, Yemen Sa'ada, Yemen, Alhamisi 21 Julai 2016. Picha: © UNICEF/UN050316/Farid

Karibu mtoto mmoja kati ya watano Mashariki ya Kati na Afrika ya Kasakazini wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu kwa mujibu wa takwimu na uchambuzi wa karibuni wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Patrick Newman na taarifa kamili (TAARIFA YA PATRICK) Takwimu hizo zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimi 90 ya watoto [...]

11/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031