Nyumbani » 08/09/2017 Entries posted on “Septemba 8th, 2017”

Natathmini hali ya chakula Afrika-Da Silva

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva rais wa Tanzania John Magufuli.(Picha:FAO)

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva ambaye amezuru bara la Afrika ikiwemo Tanzania amesema ametumia fursa hiyo kutathimini hali ya uhakika wa chakula barani humo. Katika mahojiano na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, da Silva amesema bara la Afrika linakabiliwa na changamoto ya mabadiliko [...]

08/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanyoro wa Uganda wahaha kuhifadhi asili yao

Kusikiliza / Michezo ya kitamaduni kwenye kumbukumbu ya wahanga wa ukatili wa wakoloni kwenye kaburi la pamoja la Nalweyo. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili_John Kibego

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO linahimiza umuhimu wa kulinda tamaduni kwa ajili ya kuendeleza jamii na kukuza maelewano. Aidha manufaa ya ulinzi wa utamaduni ni zaidi ya hapo kama inavyojitokeza katika makala hii kuhusu juhudi za kubaini maeneo ya kihistoria kwa ajili ya kuimarisha utalii sambamba na harakati za [...]

08/09/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mizani ya utekelezaji wa SDGs sio sawa- Thompson

Kusikiliza / Rais wa Baraza Kuu Peter Thompson akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo kuhusu hatua zilizopigwa katika SDGs. Picha:  UM/Evan Schneider

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekutana leo kujadili hatua zilizopigwa katika utekelezaji wa Malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs yaliyopitishwa mwaka 2015 na ukomo wake ni 2030. Akihutubia  mkutano huo, Rais wa Baraza Kuu Peter Thompson amesema kwa pamoja kumekuwa na mwamko na kwamba uchagizaji wa Ajenda 2030 jijini New York umehakikisha kwamba SDGs zinasalia kuwa [...]

08/09/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vijana ndio tumaini langu kwa mustakhbali bora duniani- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.(Picha:Jean-Marc Ferré/maktaba)

Wakati viongozi wa dunia wakijiandaa kushiriki mjadala wa wazi wa kikao cha 72 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, kuanzia tarehe 19 mwezi huu, Katibu Mkuu wa umoja huo António Guterres amesema chombo hicho kinapaswa kuchagiza diplomasia ili kusuluhisha mizozo inayokumba maeneo mbalimbali ya ulimwengu hivi sasa. Akihojiwa na Idhaa ya [...]

08/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki : Mtagusano

Kusikiliza / Neno la wiki_MTAGUSANO

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno "Mtagusano" Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Nuhu anasema neno Mtagusano ni ushirikiano wa watu wawili au zaidi katika kujadili jambo fulani au katika kitendo chochote, watu hawa wakiwa na [...]

08/09/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Kambi za kuhifadhi warohingya Bangladesh zazidiwa uwezo- UNHCR

Kusikiliza / Kambi ya Kutupalong, ambayo imepokea wageni zaidi ya 16,000 ndani ya wiki moja. Wakimbizi wajaribu kupata hata nafasi ya kusimama. Picha: UNHCR

Huku warohingya kutoka Myanmar wakiendelea kumiminika nchini Bangladesh wakikimbia mauaji nchini mwao, maeneo ambamo kwayo wanahifadhiwa ugenini yamezidiwa uwezo. Patrick Newman na ripoti kamili. (Taarifa ya Patrick) Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasema hali hiyo inatokana na kwamba katika wiki mbili zilizopita zaidi ya warohingya 270,000 wameingia Bangladesh. Safari zao za [...]

08/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakazi wa Florida wafuate ushauri kukabiliana na Irma- WMO

Kusikiliza / Dhoruba Irma yaelekea Florida. Picha: WMO

Shirika la hali ya hewa duniani, WMO limetaka wakazi wa jimbo la Florida nchini Marekani kuzingatia ushauri wakati huu ambapo dhoruba kali Irma inapoelekea kupiga eneo hilo. Dhoruba hiyo iko sambamba na dhoruba nyingine mbili zilizopatiwa majina Jose na Katia, ambazo ziko ukanda wa bahari ya Atlantiki na tayari imeleta madhara makubwa kwenye visiwa kadhaa [...]

08/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijiji vyachomwa moto Kasai huku shule zikisambaratishwa- UNHCR

Kusikiliza / Watoto wakimbizi wa ndani wako kwenye mlango wa duka ambalo kwa sasa haina bidhaa za kuuzwa katika Mkoa wa Kasai. Picha: © UNHCR / Andreas Kirchhof

Mapigano kati ya jeshi la serikali na vikundi vilivyojihami kwenye eneo la Kasai huko Jamuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC yamesababisha mauaji ya raia, uharibifu mkubwa wa mali huku ukosefu wa sheria ukitamalaki. Assumpta Massoi na na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Ujumbe wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR uliotembelea eneo [...]

08/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 750 ni wajinga wa kutojua kusoma na kuandika duniani-UNESCO

Kusikiliza / Watu milioni 750 ni wajinga wa kutojua kusoma na kuandika duniani. Picha: UNSCO

Leo Septemba nane ni siku ya kimataifa ya kupinga ujinga wa kutojua kusoma na kuandika ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni 'kusoma na kuandika katika dunia ya kidijitali'. Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO linasema teknolojia za kidijitali zinapenya katika nyanja zote za maisha na kuathiri namna watu wanavyoishi, [...]

08/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031