Nyumbani » 07/09/2017 Entries posted on “Septemba 7th, 2017”

Baraza Kuu lajadili utamaduni wa amani #CultureOfPeace

Kusikiliza / Mshauri mwandamizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera Ana María Menéndez(kushoto) akihutubia kwenye kikao hicho. Katikati ni Rais wa Baraza Kuu Peter Thomson. (Picha:UN/Eskinder Debebe)

Hii leo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeakuwa na kikao cha ngazi ya juu kikiangazia utamaduni wa amani, jambo ambalo linaelezwa kuwa hivi sasa linafifia. Akizungumza kwenye mkutano huo mshauri mwandamizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera Ana María Menéndez amesema mizozo inaongezeka kila uchao katika kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, sambamba [...]

07/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haikuwa rahisi,wakimbizi wa Burundi waanza kurejea nyumbani: UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wa Burundi. Picha: UNHCR

Hatimaye kundi la kwanza la wakimbizi wa Burundi walioko nchini Tanzania limewasili nchini mwao, hii ni baada ya sintofahamu iliyosababisha mkutano kati ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, serikali ya Tanzania na Burundi. Urejeshwaji wa wakimbizi hao kwa hiari umeanza kutekelezwa ambapo wakimbizi 300 wamewasili Burundi kurejelea maisha kwa kile kinachoaminika [...]

07/09/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Kenya inahitaji dola 106M kufuatia ukame unaokumba eneo la Kaskazini mwa nchi

Kusikiliza / Familia huko Garissa nchini Kenya wanatembea kuelekea sehemu ambayo wataweza kupata maji. Picha: UNICEFKenya/2017/Serem

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yametoa ombi la dola milioni 106 kwa ajili ya kupiga jeki shughuli za za dharura za kuokoa maisha kufuatia ukame unaokumba eneo la Kaskazini mwa Kenya. Akizungumza wakati wa kutoa ombi hilo Siddharth Chatterjee, mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya amesema jamii ya Umoja wa Mataifa na jamii ya [...]

07/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yazindua wavuti mpya kufuatilia wahamiaji

Kusikiliza / IOM limezindua wavuti mpya kwa ajili ya wahamiaji ambao hawajulikani waliko. Picha: IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM limezindua wavuti mpya kwa ajili ya wahamiaji ambao hawajulikani waliko. Mradi huo utafuatilia wahamiaji ikiwemo wakimbizi na waomba hifadhi ambao wamefariki dunia au ambao wametoweka wakati wakielekea katika nchi ya kigeni. Wavuti huo ambao umekarabatiwa upya unajumuisha jedwali jipya na ramani ambazo zitawezesha mtu kufuatilia takwimu kwa mwezi, mwaka au [...]

07/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yapendekeza mbinu za kudhibiti habari za uongo

Kusikiliza / Mtu anayepitia vyombo vya habari vya kijamii kwenye kompyuta (maudhui yalmefichwa ili kulinda faragha). Picha: World Bank

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limetoa mapendekezo 15 yenye lengo la kukabiliana na habari bandia au za uongo ambazo hivi zimeshamiri kwenye mitandao ya kijamii. Guy Berger ambaye ni Mkurugenzi wa UNESCO wa masuala ya uhuru wa kujieleza na maendeleo ya vyombo vya habari amewasilisha mapendekezo hayo mbele ya [...]

07/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa utawala bora ni sababu ya vijana Afrika kujiunga na misimamo mikali- UNDP

Kusikiliza / Vijana waKongomani. Picha: UM/BZ

Vijana wa Afrika wanajihususisha na vikundi vyenye misimamo mikali kutokana na sababu kadhaa ikiwemo kupuuzwa, kunyimwa fursa pamoja na ukosefu wa utawala bora. Patrick Newman na ripoti kamili. (Taarifa ya Patrick) Nats.. Mkutano  ulianza kwa onyesho la video ya kijana akizungumzia alivyojiunga na kikundi cha Al Shabaab akiwa na umri wa miaka 13 bila mama [...]

07/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi maarufu India

Kusikiliza / Unesco yalaani mauaji ya mwandishi maarufu India. Picha: UM

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa  la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO Irina Bokova amelaani vikali mauaji ya mwandishi wa habari maarufu nchini India Gauri Lankeshi aliyeuawa tarehe 5 mwezi huu akiwa nyumbani kwake huko Bangaluru  Kusini mwa India  na watu wasiojulikana. Katika taarifa yake, Bi. Bokova amesema kila shambulizi kwa  vyombo vya [...]

07/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi 300 wa Burundi warejea kutoka Tanzania

Kusikiliza / Mama mkimbizi na mtoto wake wakiwa na wakimbizi wengine nchini Burundi. Picha:UM

Licha ya changamoto kadhaa zilizojitokeza, hatimaye kundi la kwanza la wakimbizi 300 wa Burundi wanaorejea kwa hiari kutoka nchini Tanzania, limewasili hi leo. Joseph Msami na taarifa kamili. (TAARIFA YA MSAMI) Kwa mujibu wa Mwakilishi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Burundi, Abel Mbilinyi ameiambia idhaa hii kuwa wakimbizi [...]

07/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu kujadili utamaduni wa amani #CultureOfPeace

Kusikiliza / Mtazamo wa ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York, Marekani (Picha:UN /Ryan Brown)

Hii leo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa litakuwa na kikao cha ngazi ya juu kikiangazia utamaduni wa amani, jambo ambalo linaelezwa kuwa hivi sasa linafifia. Rais wa baraza hilo Peter Thomson amesema wakati wa kikao hicho wajumbe kwa kuzingatia mada hiyo watajadili jinsi ya kupanda mbegu ya utamaduni wa amani tangu utotoni. Amesema kwa [...]

07/09/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031