Nyumbani » 06/09/2017 Entries posted on “Septemba 6th, 2017”

Shambulizi dhidi ya walinda amani Mali lalaaniwa vikali

Kusikiliza / Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wapiga doria. Picha: MINUSMA/Sylvain Liechti

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani shambulizi dhidi ya msafara wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA liliotokea jana na kusababisha vifo vya walinda amani wawili na kujeruhi wengine wengi. Kupitia taarifa ya msemaji wake, Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga, serikali na [...]

06/09/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ingawa sikusoma nidhamu imenisaidia kufika nilipo- Kiba

Kusikiliza / Ali Kiba, mwanamuziki mashuhuri kutoka Tanzania. Pcha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Vijana! Umoja wa Mataifa unasema kuwa kundi hili ndilo linalopaswa kuwa mstari wa mbele kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Hii ni kwa kuzingatia siyo tu wingi wao hivi sasa bali pia uwezo wao wa kubuni na kugundua teknolojia bora na fanisi za kufanikisha malengo hayo. Lakini je nini kinatakiwa zaidi tu ya kuwa kijana? [...]

06/09/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindupindu chaua watu 23 Nigeria

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani wateka maji nchini Nigeria. Picha: UNICEF

Mlipuko wa kipindupindu umeripotiwa katika jimbo la Borno nchini Nigeria ambapo wizara ya afya nchini humo imesema hadi sasa watu 23 wamefariki dunia tangu kisa cha kwanza kiripotiwe tarehe 16 mwezi uliopita. Idadi hiyo ya vifo ni kati ya wagonjwa 530 walioripotiwa hadi jana kwenye kambi ya Muna Garage inayohifadhiwa wakimbizi wa ndani 20,000 katika [...]

06/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF yasema dhoruba Irma ni mwiba kwa watoto

Kusikiliza / Kimbunga Matthew ilipitia Jeremie, Haiti, Octoba 4, 2016, nchi huu inajitayarisha kukabiliana na Kimbunga Irma. Picha: UM/Logan Abassi

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limetoa tahadhari kuhusiana na  dhoruba  Irma ambayo inakumba ukanda wa Karibea. Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Amerika Kusini Marita Perceval  amesema  dhoruba hiyo ikiambatana na upepo mkali inatarajiwa kupiga eneo kubwa  la ukanda huo ikihusisha nchi za visiwani kama vile Antigua na Barbuda, Dominica, St. Maarten, [...]

06/09/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Katika kulinda raia tuzibe ufa badala ya kujenga ukuta- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kushoto) akihutubia Baraza Kuu kuhusu ulinzi wa raia na rais wa Baraza Kuu Peter Thompson.(Picha:UM/Kim Haughton)

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili ulinzi wa raia ambapo Katibu Mkuu António Guterres amewasilisha ripoti yake ya kwanza kuhusu mada hiyo. Akihutubia kikao hicho mjini New York, Marekani,  Bwana Guterres amesema ripoti hii inakuja wakati kunahitajika juhudi za pamoja kwa ajili ya kuzuia mauaji ya halaiki, ukatili wa kivita, mauaji yanayolenga [...]

06/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

China mwachieni huru mwanaharakati Jiang Tianyong

Kusikiliza / UNHRC Logo

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa serikali ya China imuachie huru mwanasheria na mkereketwa  wa haki za binadamu nchini humo Jiang Tianyong ambaye ameshtakiwa kwa makosa ya uchochezi dhidi ya serikali. Wito wa wataalamu hao umekuja wakati Jiang anasubiri hukumu yake baada ya kile kinachodaiwa kukiri kupitia televisheni tarehe [...]

06/09/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi 300 kuanza kuwasili Burundi kesho: Mbilinyi

Kusikiliza / Wakimbiz wa Burundi katika kituo cha muda cha UN Makamba wakielekezwa kwa ajili ya warejea nyumbani. Picha: UNHCR

Awamu ya kwanza ya wakimbizi wa Burundi wanaorejea kwa hiari kutoka Tanzania wanatarajiwa kuwasili nchini mwao kesho, hii ni baada ya maafikiano ya juma lililopita kati ya shirika la Umoja wa Mataifa lakuhudumia wakimbizi UNHR, serikali ya Tanzania na Burundi. Joseph Msami na taarifakamili. ( TAARIFA YA MSAMI) ( Sauti ya Mbilinyi) Huyu ni Abel [...]

06/09/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WFP yasaidia wanaokimbia ukatili Myanmar

Kusikiliza / Wakimbizi wa Myanmar wapanga foleni kupokea msaada huko Cox's Bazar. Picha: WFP/Sunee Singh

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linapatia msaada watu waliokimbilia Bangladesh kufuatia vitendo vya ukatili vinavyofanyika jimbo la Rakhine nchini Myanmar. Tayari WFP imetoa msaada kwa zaidi ya watu 28,800 kwenye wilaya ya Cox’s Bazaar mpakani na Myanmar ambapo wamepatiwa vyakula kama vile biskuti zilizorutubishwa, wali na mbaazi. WFP inasikitishwa na hali ya kiafya ya wanawake na watoto [...]

06/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Syria ilitumia gesi ya Sarin dhidi ya raia- Ripoti

Kusikiliza / Mkuu wa kamisheni huru ya uchunguzi kuhusu Syria, Paulo Pinheiro.(Picha:UNIfeeed/video capture)

Tume ya uchunguzi kuhusu uovu unaofanyika Syria imethibitisha kuwa vikosi vya serikali vilitumia silaha za kemikali dhidi ya raia kwenye maeneo yanayoshikiliwa na upinzani. Patrick Newman na ripoti kamili. (Taarifa ya Patrick) Mwenyekiti wa tume hiyo Paulo Pinheiro [PINYERO] amesema hayo wakati akiwasilisha mbele ya waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi, ripoti yake ya 14 [...]

06/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Chanjo dhidi ya Kipindupindu zapelekwa Sierra Leone

Kusikiliza / Wahudumu wa afya wanawapa matibabu waathirika wa maporomoko ya ardhi nchini Sierra Leone, ikiwa ni pamoja na chanjo dhidi ya Kipindupindu. Picha: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema nusu ya wananchi wa Sierra Leone watapatiwa chanjo dhidi ya Kipindupindu ili kuwakinga na ugonjwa huo baada ya mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyokumba nchi hiyo mwezi uliopita. WHO imenukuu wizara ya afya nchini humo ikisema kuwa hatua hiyo inafuatia mfuko wa chanjo duniani, GAVI kupeleka zaidi ya chanjo [...]

06/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jitihada za kuhakikisha watoto wanakwenda shule zagonga mwamba- UNICEF

Kusikiliza / Harakati za kupunguza idadi ya watoto wanaokosa fursa ya kupata elimu zakumbwa na changamoto nyingi. Picha: Ripoti_UNICEF

Ripoti mpya ya shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF imesema harakati za kupunguza idadi ya watoto wanaokosa fursa ya kupata elimu bado hazijaweza kuzaa matunda ya kutosha. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ni watoto milioni 123 wenye umri wa kati ya miaka 6 hadi 15 ndio wanaokosa fursa ya elimu mwaka huu, [...]

06/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031