Nyumbani » 05/09/2017 Entries posted on “Septemba 5th, 2017”

Wanawake wakabiliwa na vikwazo wakijikwamua kiuchumi Uganda.

Kusikiliza / Wanwake waliofurushwa makwao kufuatia uchimbaji wa dhahabu. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili_John Kibego

Nchini Uganda wakati wanawake wakikabiliana na umasikini kwa kufanya kazi mbalimbali wanakabiliwa na vikwazo vinavyowazuia kutekeleza miradi kama vile uchimbaji wa dhahabu. John Kibego ameangazia vikwazo hivyo wilayani Mubende nchini humo na kuandaa makala ifuatayo. (MAKALA YA JOHN KIBEGO)

05/09/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Baraza la Usalama ni muhimu kwa suluhu DPRK- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani Picha: UM/Evan Schneider

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amesema umoja ndani ya Baraza la Usalama la chombo hicho ni muhimu ili kupata suluhu ya amani ya tishio la nyuklia kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK. Bwana Guterres amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New [...]

05/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni mijini ambako SDGs zitatimizwa au la- Amina

Kusikiliza / Amina-dsg-4page

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili utekelezaji wa ajenda ya miji kwa ajili ya maendeleo endelevu, amani na usalama. Akihutubia mkutano huo unaolenga kuhakikisha pia kwamba mustakabali wa shirika la makazi la Umoja wa Mataifa UN-Habitat unachagiza utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs,  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina [...]

05/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICRC yashukuru waliotekwa nyara kuachiwa huru

Kusikiliza / ICRC Logo

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu, ICRC limeshukuru kufuatia kuachiwa huru kwa wafanyakazi wake wawili waliotekwa  nyara tarehe 8  mwezi februari mwaka  huu  huko Jawzjan nchini Afghanistan. Mwakilishi wa  ICRC nchini Afghanistan Monica Zanerelli amesema wana furaha kubwa kwani wafanyakazi hao waliotekwa na waasi wamechiwa huru wakiwa na afya njema. Ameshukuru kwa  ushirikiano kutoka vyombo [...]

05/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wako hatarini zaidi kujiua- WHO

Kusikiliza / Kuna ongezeko la kiwango cha watu kujiua. Picha: Desa

Shirika la afya duniani, WHO linasema kuwa kuna ushahidi zaidi unaodokeza kuwa wakimbizi wako hatarini zaidi kujiua. Dkt. Alessandra Fleischmann ambaye ni mwanasayansi wa WHO katika idara ya afya ya akili na matumizi holela ya dawa amesema hayo wakati dunia inaelekea kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuzuia kujiua tarehe 10 mwezi huu. Amesema miongoni mwa [...]

05/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamii ya kimataifa iingilie kati kunusuru watu wa Yemen-Zeid

Kusikiliza / Wayemeni wanakagua kijengo liloporomoshwa na mlipuko wa kombora katika mji mkuu wa Sana'a Agosti mwaka huu. Piccha: EPA-EFE/Yahya Arhab

Hali ya kibinadamu nchini Yemen inaendelea kuzorota kila uchao huku vitendo vinavyokiuka haki za binadamu na ukatili dhidi ya sheria za kimataifa vikiendelea na raia wakiendelea kuteseka. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa kufuatia ombi la Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kutathmini ukiukwaji wa haki kwa kipindi [...]

05/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maelfu wanaokimbia machafuko Myanmar shakani: UNHCR

Kusikiliza / Familia geni ya wakimbizi kutoka Myanmar wanasimama kwenye matope nje ya kambi ya wakimbizi ya Kutupalong. Picha:UNHCR

  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, linasema zaidi ya wakimbizi 120,000 wamewasili nchini Bangladesh, tangu kulipuka kwa machafuko jimboni Rakhine Kaskazini mwa Myanmar, mapema mwezi uliopita. Patrick Newman na ripoti kamili. (Taarifa ya Patrick) UNHCR imeeleza wasiwasi wake kuhusu kuendelea kwa machafuko nchini Myanmar, na taarifa kwamba raia wanafariki dunia wakati [...]

05/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Janga la njaa Ethiopia kuongezeka iwapo hakuna miradi sahihi- UM

Kusikiliza / Viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la chakula na kilimo, FAO, maendeleo ya kilimo, IFAD na mpango wa chakula, WFP ziarani Ethiopia. Picha: FAO_IFAD_WFP_Petterik Wiggers.

Uwekezaji wa kina unahitajika ili wakazi wanaokabiliwa na njaa kutokana na ukame uliokithiri huko jimbo la Somali nchini Ethiopia waweze kustahimili ukame wa mara kwa mara unaosababishwa na athari za mabadiliko ya tabianchi. (Taarifa ya Grace) Kauli hiyo imetolewa mjini Addis Ababa, Ethiopia na viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la chakula na [...]

05/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031