Nyumbani » 01/09/2017 Entries posted on “Septemba 1st, 2017”

Guterres asikitishwa na madhara kufuatia mafuriko nchini Bangladesh, India na Nepal

Kusikiliza / Floods-4page (1)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  António Guterres ameelezea kusikitishwa kwake na vifo na madhila wanayokumbana nayo watu nchini Bangladesh, India na Nepal kufuatia mvua kali zilizosababisha mafuriko. Guterres kupitia taarifa ya msemaji wake ametuma salamu za rambi rambi kwa serikali na watu wa Bangladesh, India na Nepal na kupongeza serikali hizo kwa uongozi katika kukabiliana [...]

01/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mamlaka Myanmar ina wajibu katika kuzuia janga-Guterres

Kusikiliza / Mtoto wa kabila la Rohingya, katika kambi ya wakimbizi, magharibi mwa wilaya ya Rakhine, Myanmar. Picha ya David Swanson/IRN (MAKTABA)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameelezea kusikitishwa sana na ripoti za operesheni katili za kiusalama zinazotekelezwa dhidi ya raia katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar, wakati huu ambapo maelfu ya watu wa kabila la Rohingya wakikimbilia nchi jirani ya Bangladesh. Kupitia taarifa ya msemaji wake Guterres amesema watu wanahitaji kujizuia ili kuepukana [...]

01/09/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Somalia yaweza kuinua ustawi wa wakimbizi wa ndani: Kalin

Kusikiliza / Mshauri mwandamwizi wa moja wa Mataifa Mkuu kuhusu masuala ya ukimbizi Bwana Walter Kalin ziarani Somalia. Picha: UN/Video capture

Mshauri mwandamwizi wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukimbizi wa ndani Walter Kalin amesema Somalia yaweza kuanzisha mfumo bora na pia ufumbuzi wa kudumu nchini kwa kushirikiana na uongozi wa serikali, ambao utahamasisha zoezi la upatikanaji fedha za kusaidia kuinua  viwango vya maisha ya  wakimbizi wa ndani. Akiwa katika ziara ya juma moja nchini Somalia Bwana [...]

01/09/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Idadi ya waliouawa Iraq yapungua- UNAMI

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani nchini Iraq wanaokimbia vita kusaka hifadhi. Picha:  UNHCR

Idadi ya raia waliouawa au kujeruhiwa nchini Iraq imeshuka kwa viwango vya chini kabisa , kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq (UNAMI) Jumla ya raia 125 waliuawa mwezi Agosti huku wengine 188 walijeruhiwa kwa sababu ya visa vya ugaidi na mapigano kote nchini. Hii inalinganishwa na vifo 241 vilivyoripotiwa mwezi [...]

01/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shairi 'Head over heels' latoa taswira ya madhila ya wakimbizi wa Sudan Kusini

Kusikiliza / Emmy Mahmoud. Picha: UNHCR/Video capture

Takriban wakimbizi milioni moja wa Sudan Kusini wamekimbilia nchi jirani ya Uganda, hii ikiwa ni nchi inayowahifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Sudan Kusini. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema fedha zaidi zinahitajika kwa ajili ya kusaidia wakimbizi hao wa Sudan Kusini na serikali ya Uganda inayowahifadhi. Mbinu mbali mbali zinatumika kupaza [...]

01/09/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Msaada wa dharura sio muoarubaini wa janga la njaa Ethiopia-FAO

Kusikiliza / Ukame nchini Ethiopia.(Picha:FAO/Tamiru Leggese)

Takriban watu milioni 8.5 nchini Ethiopia wanahitaji msaada wa chakula katika nusu ya mwaka huu wa 2017 lakini uhaba wa chakula unaoshuhudiwa hauwezi kutatuliwa na msaada wa dharura pekee. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Hii ni kwa mujibu wa shirika la chakula duniani FAO likiongeza kuwa suluhu ya kudumu ni kuimarisha uwezo [...]

01/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Operesheni za kunasua miili baada ya maporomoko Sierra Leone yaendelea

Kusikiliza / Juhudi za kunasua miili nchini Sierra Leone.(Picha:UNICEF/Twitter)

Nchini Sierra Leone wakati harakati za usaidizi kwa wahanga wa maporomomo ya udongo yaliyotokea zaidi ya wiki mbili zilizopita zikiendelea, juhudi nazo zinaendelea kuopoa miili ya watu waliopoteza maisha. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema baadhi ya sehemu za miili ya binadamu zinapatikana kwenye mto Juba karibu na mji mkuu Freetown [...]

01/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wiki ya maji ikihitimishwa, watoto waeleza ukosefu wa maji unavyowaathiri kielimu

Kusikiliza / Mtoto akiwa amebeba maji.(Picha:UM/Tim McKulka)

Wiki ya maji duniani ikihitimishwa leo, Umoja wa Mataifa unasema suala la maji na huduma za kujisafi ni muhimu katika kutekeleza ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu, SDGs. Patrick Newman na tarifa kamili. (TAARIFAYA PATRICK) Maudhui ya wiki ya maji mwaka huu ni “Maji na taka: Punguza na tumia tena” kauli inayochagiza uhifadhi wa maji [...]

01/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki – Matamata

Kusikiliza / Neno la wiki_MATAMATA

Wiki hii tunaangazia neno “Matamata” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Bwana Sigalla anasema neno “Matamata” ni hali ya kupepesuka aliyo nayo mtoto anayejifunza kutembea, ama mtu mzima ambaye ni mgonjwa na anajipa mazoezi ya kutembea polepole.  Ameongeza kuwa neno hili haina uhusiano na [...]

01/09/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna uhusiano kati ya dhoruba Harvey na shughuli za binadamu- WMO

Kusikiliza / Mafuriko yaliyosababishwa na dhoruba Harvey Picha: WMO

Jopo la wataalamu kutoka shirika la hali ya hewa duniani, WMO limesema kuna uwezekano mkubwa kuwa athari za binadamu kwenye tabianchi zimesababisha dhoruba Harvey iliyopiga jimbo la Marekani la Texas. Katika taarifa yao, jopo hilo la wataalamu saba limesema uhusiano huo unaweza usiwe wa moja kwa moja lakini wamezingatia suala kwamba mvua kubwa iliyoambatana na [...]

01/09/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031