Zeid apongeza kufutwa kwa sheria zinazolinda wabakaji

Kusikiliza /

Wanawake waokumbwa na ubakaji husalia na msongo. Picha: UM/Albert González Farran

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Zeid Ra'ad Al Hussein amekaribisha kitendo cha Lebanon, Tunisia na Jordan kufutilia mbali sheria ambazo zinalinda wabakaji dhidi ya mashtaka kwa kuwaruhusu kuwaoa wale waliowabaka.

(Taarifa ya Assumpta)

Zeid amesema kitendo cha wabunge katika nchi hizo kufuta sheria hizo kinadhihirisha azma yao ya kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake.

Amesema kumuadhibu mtu aliyebakwa kwa kumuoza kwa mtu aliyembaka ni uhalifu mkubwa dhidi yake na hauna nafasi katika zama za sasa.

Kamishna Zeid ametaja uamuzi huo kuwa ni ushindi mkubwa akipongeza kampeni za miaka kadhaa zilizoendeshwa na watetezi wa haki za binadamu hususan wanawake huko Tunisia, Lebanon na Jordan.

Ametoa wito kwa serikali na wananchi kwenye nchi zilizo ukanda wa mashariki ya kati na kwingineko kuiga mfano huo ili kufuta sheria zinazolinda ukatili wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930